Hongera Daniel Chongolo kwa kuwa muwazi na kuukataa mfumo dhalimu

Huo upuuzi wenu wa hisia zenu kwanini mnatuletea huku? Mnawashwa na nini, si msubiri taarifa rasmi km kweli amejiuzulu? Acheni ramli za kipuuzi.
 
Kama kweli anaukataa Udhalimu, alipaswa kuukataa Uteuzi wa awali wa nafasi yake ya Ukatibu Mkuu aliyonayo hivi sasa.
 
Hata hivyo na yeye amekusanyakusanya, kama vi hati miliki vya ardhi, hakosi 100 na zaidi, bado vipesa
Dah! Alafu ukomae upewe kasumu ufe😝

Bora kung'atuka ukaviendeleza hivyo vipande vya ARDHI
 
Wakati wenye akili timamu wakiwakataa kwa vitendo,wale ambao walikuwa karibu na Adolf Hitler,chini ya utawala wa kinazi na baadhi yao kuwakataa hata wale walio karibu nao,uku katika mataifa ya myopic leaders,wanawapa vyeo watu ambao walistahili kuwa jela.
 
Sema asingeweza kufanya kazi na Makonda, mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kufanya kazi na Makonda
Aseme Makonda amewa outsmart ndani ya dakika chache. Utendaji wa Makonda umewatikisa hadi mawaziri na wakuu wote.

Huyu Chongolo hajawahi hata kukemea maovu ya watendaji, walau hata Bashiru na Kinana walikuwa wanafoka. Kumbe Chongolo yupo toka 2021? Sasa huo ukatibu mkuu wake ulikuwa kusoma ripoti tu na kuandaaa vikao vya chama au?

Kwa nyakati hizi ukiwa na katibu mkuu wa aina ya Chongolo lazima chama kichungulie shimo. Magu alishatibua akili za wananchi kuhusu hawa viongozi. Watu wanataka kuona moto na mambo yakienda. Sio kuoneana aibu, sijui kuogopa kuvunjiana heshima na nidhamu za kinafiki huku jitu linaiba na kuharibu.



Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Eti ni wa toka 2021. Mi nilidhani kateuliwa hivi karibuni.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Katibu mchangamfu
 
Amwombea mwenzie laana,hulaaniwa yeye na kizazi chake,na kazi ya kuhukumu ni kazi ya muumba peke yake.
 
Kwamba hakujua Chama kipo vipi wakati anaingia na anaendelea kuwemo kwenye Chama mpaka sasa alipoona kwamba anayekufukuza hakwambii toka ? :

Kwamba ameacha kuwa Mwana-CCM au bado ni ccm kindakindaki Chama unachosema wewe amekiona ni dhalimu...

Anyway sishangai hizi discussion of people and events ndio watu wanapenda kuzijadili badala ya Ideas....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…