Hongera Diamond kwa kupunguza maadui

Hongera Diamond kwa kupunguza maadui

kende

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
3,527
Reaction score
1,668
∆Tunaambiwa kilasiku tujitahidi kupunguza maadui na sio kuwaongeza, Diamond kafanya hivyo mwakahuu, na kilichonifurahisha zaidi kapatana na wale watu wote wenye mchango mkubwa kwenye mafanikio yake ya mziki.

Alianza kwa kumaliza tofauti zake na Bob Junior pale alipomualika kwenye 'Zari All White Party', alifanya jambo jema sana linaloweza kumzidishia baraka na kufanikiwa zaidi, huyu jamaa naweza sema ndiye aliyemtoa Diamond na kumtambulisha vyema kwa watanzania, ikumbukwe kwamba Diamond zamani alikuwa anarap, huyu ndo alimshawishi aachane na kurap aswitch kwenye kuimba baada ya kugundua ana kitu cha ziada, so ni kitu kizuri sana alivyopatana naye.

∆Pia amemaliza tofauti zake na MANECKY producer aliyemtengenezea ngoma kali kama Mawazo, Ukimwona,Nataka Kulewa,etc zilizomfanya ahit zaidi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo baadae kulitokea kutoelewana kwa kipindi kirefu, nimefurahi kusikia Diamond karudi tena kwa Manecky na anahitaji kufanya nae kazi tena.

∆Mwisho ni Davido ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa kumtambulisha kimataifa, Diamond mwenyewe alikiri kulikuwa na kutokuelewana kati yao na mda mrefu hawakuwahi kukutana, wamekuja kukutana wiki iliyopita MTV Mama, kitendo cha kukutana naye na kuonekana kwenye video wanafurahi pamoja kinaonyesha tofauti zao wamezimaliza, nikupongeze pia kwa hilo maana umepatana na wote waliohusika kwenye mafanikio yako kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa mmetofautiana, hii itakupa baraka utafanikiwa zaidi.

°°°Wale wengine waliobaki siamini kama ni mahasimu wako, mi nawachukulia kama HATERS tu, so sio mbaya ukiendelea kuwanyoosha.
 
Nasikia haters wanasema walishanyooka, yeye akainama eti.
 
Ni jambo jema ila sasa aache ule uswahili swahili na utandale wa kujiboshana na wale ma ex coz haimsaidii..sana ni kupoteza muda na kuwapa umaarufu bureee..
 
Ni vizuri sana kumaliza bifu,mabishano na majibizano na watu hasa waliompa sapoti,safi na hongera diamond.

Kuhusu wale wanawake wawili J na W ni bora tu ulivyowaonyesha kwamba hukupenda kile walichokua wamekifanya KTMA na binafs nimefurahi sana!Suala la nyota,nguvu binafsi + urembo na jinsia vilitumiwa vibaya na hao ma X wake na nina imani wamejifunza.
 
Ni jambo jema ila sasa aache ule uswahili swahili na utandale wa kujiboshana na wale ma ex coz haimsaidii..sana ni kupoteza muda na kuwapa umaarufu bureee..

Sometimes inatakiwa mjinga ajibiwe ili apate uerevu!Wema alishajiona yeye ndio yeye na bila yeye bongo hii hakuna wa kuwika!Mungu amemjibu kwa ushindi wa diamond MTV,na kushindwa kwa aliowaombea kura!

Jana amehitimisha safari yake SINGIDA na kila mtu amepata jibu dhidi yake,Heshima na ukimya ni muhimu kwa watu wote
 
Kweli saana.....
 
sometimes inatakiwa mjinga ajibiwe ili apate uerevu!wema alishajiona yeye ndio yeye na bila yeye bongo hii hakuna wa kuwika!mungu amemjibu kwa ushindi wa diamond mtv,na kushindwa kwa aliowaombea kura!

Jana amehitimisha safari yake singida na kila mtu amepata jibu dhidi yake,heshima na ukimya ni muhimu kwa watu wote
like ndogo ningekupa hata 1,000,000 ndo zingekufaa
 
Nasikia haters wanasema walishanyooka, yeye akainama eti.
6407723fc10823ce75f73947e556d988.jpg
 
Sometimes inatakiwa mjinga ajibiwe ili apate uerevu!Wema alishajiona yeye ndio yeye na bila yeye bongo hii hakuna wa kuwika!Mungu amemjibu kwa ushindi wa diamond MTV,na kushindwa kwa aliowaombea kura!

Jana amehitimisha safari yake SINGIDA na kila mtu amepata jibu dhidi yake,Heshima na ukimya ni muhimu kwa watu wote

Like like like like like like like♥♥
 
Back
Top Bottom