kende
JF-Expert Member
- Dec 2, 2013
- 3,527
- 1,668
∆Tunaambiwa kilasiku tujitahidi kupunguza maadui na sio kuwaongeza, Diamond kafanya hivyo mwakahuu, na kilichonifurahisha zaidi kapatana na wale watu wote wenye mchango mkubwa kwenye mafanikio yake ya mziki.
Alianza kwa kumaliza tofauti zake na Bob Junior pale alipomualika kwenye 'Zari All White Party', alifanya jambo jema sana linaloweza kumzidishia baraka na kufanikiwa zaidi, huyu jamaa naweza sema ndiye aliyemtoa Diamond na kumtambulisha vyema kwa watanzania, ikumbukwe kwamba Diamond zamani alikuwa anarap, huyu ndo alimshawishi aachane na kurap aswitch kwenye kuimba baada ya kugundua ana kitu cha ziada, so ni kitu kizuri sana alivyopatana naye.
∆Pia amemaliza tofauti zake na MANECKY producer aliyemtengenezea ngoma kali kama Mawazo, Ukimwona,Nataka Kulewa,etc zilizomfanya ahit zaidi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo baadae kulitokea kutoelewana kwa kipindi kirefu, nimefurahi kusikia Diamond karudi tena kwa Manecky na anahitaji kufanya nae kazi tena.
∆Mwisho ni Davido ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa kumtambulisha kimataifa, Diamond mwenyewe alikiri kulikuwa na kutokuelewana kati yao na mda mrefu hawakuwahi kukutana, wamekuja kukutana wiki iliyopita MTV Mama, kitendo cha kukutana naye na kuonekana kwenye video wanafurahi pamoja kinaonyesha tofauti zao wamezimaliza, nikupongeze pia kwa hilo maana umepatana na wote waliohusika kwenye mafanikio yako kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa mmetofautiana, hii itakupa baraka utafanikiwa zaidi.
°°°Wale wengine waliobaki siamini kama ni mahasimu wako, mi nawachukulia kama HATERS tu, so sio mbaya ukiendelea kuwanyoosha.