Hongera Diamond kwa release ya Utanipenda, umenishika Nifah!

Hongera Diamond kwa release ya Utanipenda, umenishika Nifah!

kuna thread aliileta Pasco kule jukwaa la siasa ambapo yeye alisema kama wewe nifah kuwa yeye kuanzia ile juzi amemkubali magufuli japo si shabiki wake..amekubali kile alichokifanya magufuli lakini si vinginevyo....na wewe umeonyesha hilo..hongera kwa kuzisikiliza hisia za ndani kabisa
Asante sana mkuu,sikuiona sababu ya kufa na hili rohoni.
Sijaona hiyo ya Pasco,ngoja nitaitafuta.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa naomba niwajuze wale wasiomfahamu nifah...
Mimi ni mkweli na mwenye msimamo mkali.
Huwa nasimamia katika kile ninachokiamini bila kuogopa wengine watapinga vipi au kunichukulia vipi.

Back to topic... Ni ukweli ulio dhahiri kuwa Diamond kafanya vizuri,na mimi kutokana na aya ya kwanza hapo juu sitaki kuwa mnafiki au kumung'unya maneno.....UMENISHIKA Diamond.
Nimependa Audio,video yaani kila kitu.
Tokea ulivyoutoa huu wimbo jumamosi nimekuwa nauangalia mara nyingi sana,na mara zote nimekuwa natikisa kichwa na kusema naam....hapa jamaa kaweza.

Ni unafiki na kuendeleza ubishani wa kipumbavu kwa kuponda vizuri kwa mwamvuli wa team, tuachane na huu ujinga na kuukubali ukweli.

Mimi kama mdau wa muziki mzuri,nasema huu wimbo wa Diamond ni mzuri sana.

#Note
Nimetoa hii post kwa mapenzi yangu mwenyewe,haina maana kwamba sasa nimekuwa team Diamond hapana,penye ukweli lazima niseme.
Sasa sitaki unafiki na kejeli kuwa nimesanda sijui na nini maana nawajua mashabiki wa Diamond vizuri tu.
Msilolijua ni kwamba nilikuwa shabiki mzuri tu Diamond, ila alikuja kunikera sehemu fulani (hata sasa simpendi ila nimeupenda wimbo wake).

Wale fans wa Kiba wenzangu bado nipo nanyi,ila tujifunze kusema ukweli.
Hata nyie majirani zetu pia....sio mnapenda wimbo lakini mnachokisema huku ni tofauti.
Period
Nifah katika pekua pekua mtandaoni nimekutana na post ya mtu kumdongoa "nifah wa jf", je mambo ya uteam yana maana yoyote kama anatukana vibaya vile au ni wewe mwenyewe katika kujitafutia kiki? samahani kwa umbea wangu
 
PesaNdogo hayo mambo yalikuwepo sana yametulia majuzi tu hapo wakati wa kampeni.
Na bila shaka ni huko kwa Sintah....
Nitake radhi mkuu,sina huo muda kabisa.
 
mmh ndo huyu nifah kweli? au akaunt yake ipo HACKED? haya bado K 4 LIFE nae atoe ushuhuda wake hapa.
 
tangu nione ule wimbo wa kingereza when am not strong, i sell cars..
.. will you honestly love me nkaona hizi pasting hizi jaman ni shidaa
 
Back
Top Bottom