Mabibi na mabwana pana taarifa za upepo mwema kuanza kuvuma kule pande za Zanzibar.
Tulikotoka, tulikopita na tulipo kote kunafahamika. Kwamba uchaguzi ule ulikuwa na mzengwe usiofaa kurejewa? Hata mtoto mdogo anajua.
Kwa bahati mbaya pana watu wameumia na hata wengine kupoteza maisha kwenye harakati hizi huko Zanzibar.
Kwa hakika hao wote hawakuumia wala kupotea bure. Wote hao ni muhimu kuwepo katika hadidu rejea za maridhiano.
Pana nafasi kubwa ya Dk. Mwinyi katika maridhiano ya namna hii kujiweka katika nafasi muafaka ya kukubalika zaidi kote visiwani na hata bara iwapo tu atatanguliza haki mbele.
Amani Karume kupitia maridhiano aliiacha Zanzibar ikiwa moja na yeye kuweza kukubalika zaidi kama kiongozi aliyekuwa mwenye busara haswa.
Mwinyi kuridhiana na upinzani na hata ikibidi kuendesha uchaguzi mpya utakaokuwa huru, wa haki na wenye kuaminika hakutampunguzia lolote. Zaidi ya kuwa kwa matokeo yeyote yale, yeye ndiye atakayekuwa mshindi.
Mwinyi anaweza hata kushinda tena na sasa ikiwa katika uchaguzi utakaokuwa wenye uwazi unaokubalika.
Wamepata zawadi za nobeli kwenye jitihada kama hizi wengi. Baadhi yao ni kina De Clerk na kina Mandela. Kina Aung San Suu Kyi, na wengine wengi.
Mwinyi sasa hivi ndiye rais. Mustakabala mwema wa wanzibari upo mikononi mwake zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.
Aungwe mkono Mwinyi na wapenda amani wote ili kumwezesha kufanya maamuzi hata kama yatakuwa magumu mno kwa mustakabala mwema wa watu wa Zanzibar.
"Shime Dk. Mwinyi historia iko upande wako kuitendea mema nchi hii."
Walisema waungwana mwanzo wa ngoma ni lele na mwanzo wa safari ndefu ni ile hatua ya kwanza.