Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ungefanya nini !? Usiombe hawa MADHALIM wakakugeukia wewe.. Nchi hii wao ni above the lawZanzibar kila uchaguzi askari kutoka bara wanakuja wanaua ndugu zenu mpo mpo tu!
Wazanzibari waliouawa atawafufua?
Nani alivuruga muafaka wa 2010? Si ninyi wenyewe? Sasa unatarajia na kupongeza nini tena wakati nyie ndie wabomoaji?
Umesomeka mkuuSina hakika kama uliweza ona hii kwenye mada;
Zipo njia nyingi za kushughulikia waliouawa zikiwamo;
"Kwa hakika hao wote hawakuumia wala kupotea bure. Wote hao ni muhimu kuwepo katika hadidu rejea za maridhiano."
1. Fidia stahiki
2. Kuwawajibisha wote waluohusika
3. Nk, nk.
Au wewe ulikuwa na nyongeza zipi mkuu?
Good observation. Mwinyi is just a toothless 🐕Your are just hypothetical. All decisons are made in Dodoma. He is just a puppet. He can change nothing. All power is with Magufuli. Akileta fyoko, Kamati Kuu ya CCM inamwondoa kabla jua halijachomoza.
HAKUNA cha maana chochote utafanya Kama upande mmoja wapo CCM. CCM Ni Wahuni kuliko wahuni wenyewe wa Stand. CCM wanataka maridhiano ya kuvuka daraja la muda tu, sio maridhiano ya kudumu. Kwa vile CCM wao hawaumii, hivyo hawajutii. Wangelikuwa wanaumia na kujutia ya Mkapa yangewafundisha somo, hivyo wangeheshimu mwafaka uliopelekea maridhiano baadaye. CCM wanaweza wakaichezea Zanzibar wanavyotaka. Suruhu ya kudumu ya Zanzibar haitatokea chini ya CCM, yahitajika external force.Katika sasa milango ya maridhiano huwa haifungwi.
Labda basi wewe ulikuwa na maoni gani ya nini kifanyike labda ambacho kitakuwa bora zaidi?
HAKUNA cha maana chochote utafanya Kama upande mmoja wapo CCM. CCM Ni Wahuni kuliko wahuni wenyewe wa Stand. CCM wanataka maridhiano ya kuvuka daraja la muda tu, sio maridhiano ya kudumu. Kwa vile CCM wao hawaumii, hivyo hawajutii. Wangelikuwa wanaumia na kujutia ya Mkapa yangewafundisha somo, hivyo wangeheshimu mwafaka uliopelekea maridhiano baadaye. CCM wanaweza wakaichezea Zanzibar wanavyotaka. Suruhu ya kudumu ya Zanzibar haitatokea chini ya CCM, yahitajika external force.
We wacha wazoee tu kuna siku watarudi vichwa tu.Zanzibar kila uchaguzi askari kutoka bara wanakuja wanaua ndugu zenu mpo mpo tu!
Ndo manaake, sifahamu maridhiano ya nini wakati wao wana jeshi. Washaleta ubabe wa kunyakua madaraka, sasa walete maendeleo tuu! Maridhiano ya nini tena ? Nina 100% akili za hawa watu zilipanga ubabe wa kunyakua madaraka na kusahau kama ukishakaa madarakani kwa njia izo za kizushi hakutakuwa na maendeleo.Maalim anaouthubutu wa kukomaa nao.
Muda unapaswa kuwa mfupi na defined.
Mabibi na mabwana pana taarifa za upepo mwema kuanza kuvuma kule pande za Zanzibar.
Tulikotoka, tulikopita na tulipo kote kunafahamika. Kwamba uchaguzi ule ulikuwa na mzengwe usiofaa kurejewa? Hata mtoto mdogo anajua.
Kwa bahati mbaya pana watu wameumia na hata wengine kupoteza maisha kwenye harakati hizi huko Zanzibar.
Kwa hakika hao wote hawakuumia wala kupotea bure. Wote hao ni muhimu kuwepo katika hadidu rejea za maridhiano.
Pana nafasi kubwa ya Dk. Mwinyi katika maridhiano ya namna hii kujiweka katika nafasi muafaka ya kukubalika zaidi kote visiwani na hata bara iwapo tu atatanguliza haki mbele.
Amani Karume kupitia maridhiano aliiacha Zanzibar ikiwa moja na yeye kuweza kukubalika zaidi kama kiongozi aliyekuwa mwenye busara haswa.
Mwinyi kuridhiana na upinzani na hata ikibidi kuendesha uchaguzi mpya utakaokuwa huru, wa haki na wenye kuaminika hakutampunguzia lolote. Zaidi ya kuwa kwa matokeo yeyote yale, yeye ndiye atakayekuwa mshindi.
Mwinyi anaweza hata kushinda tena na sasa ikiwa katika uchaguzi utakaokuwa wenye uwazi unaokubalika.
Wamepata zawadi za nobeli kwenye jitihada kama hizi wengi. Baadhi yao ni kina De Clerk na kina Mandela. Kina Aung San Suu Kyi, na wengine wengi.
Mwinyi sasa hivi ndiye rais. Mustakabala mwema wa wanzibari upo mikononi mwake zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.
Aungwe mkono Mwinyi na wapenda amani wote ili kumwezesha kufanya maamuzi hata kama yatakuwa magumu mno kwa mustakabala mwema wa watu wa Zanzibar.
"Shime Dk. Mwinyi historia iko upande wako kuitendea mema nchi hii."
Walisema waungwana mwanzo wa ngoma ni lele na mwanzo wa safari ndefu ni ile hatua ya kwanza.