Zanzibar 2020 Hongera Dkt. Mwinyi panapo nia utaitibu Zanzibar

Wokovu unakuja pale unapojutia dhambi ulioitenda. Kujutia kitu ambacho unakifurahia kutokea ni ngumu sana. Halafu katika dhambi kubwa kwenye dini ya kiislam ni kutoa uhai wa mwenzako. Hii dhambi ukifa nayo, hata kama ulikuwa unaswali 24/7 unatoa zakka kila siku, unakwenda kuhiji kila sekunde, unakwenda kuishi motoni milele!

Hakuna haja ya maridhiano ikiwa walitia nia ya kutoa roho za watu tangu mwanzo. Waongoze serikali wenyewe mwanzo mwisho, ikiwezekana wabadilishe katiba iseme raisi hakuna kufa, na akifa basi ataendelea kuwa rais mpaka huko kaburini labda wadhifa huo anaona utamsaidia akikutana na Munkar na Nakir
 
Nani alivuruga muafaka wa 2010? Si ninyi wenyewe? Sasa unatarajia na kupongeza nini tena wakati nyie ndie wabomoaji?
 
Wazanzibari waliouawa atawafufua?

Sina hakika kama uliweza ona hii kwenye mada;


Zipo njia nyingi za kushughulikia waliouawa zikiwamo;

"Kwa hakika hao wote hawakuumia wala kupotea bure. Wote hao ni muhimu kuwepo katika hadidu rejea za maridhiano."

1. Fidia stahiki
2. Kuwawajibisha wote waluohusika
3. Nk, nk.

Au wewe ulikuwa na nyongeza zipi mkuu?
 
Nani alivuruga muafaka wa 2010? Si ninyi wenyewe? Sasa unatarajia na kupongeza nini tena wakati nyie ndie wabomoaji?

Katika sasa milango ya maridhiano huwa haifungwi.

Labda basi wewe ulikuwa na maoni gani ya nini kifanyike labda ambacho kitakuwa bora zaidi?
 
Umesomeka mkuu
 
Your are just hypothetical. All decisons are made in Dodoma. He is just a puppet. He can change nothing. All power is with Magufuli. Akileta fyoko, Kamati Kuu ya CCM inamwondoa kabla jua halijachomoza.
Good observation. Mwinyi is just a toothless 🐕
 
Katika sasa milango ya maridhiano huwa haifungwi.

Labda basi wewe ulikuwa na maoni gani ya nini kifanyike labda ambacho kitakuwa bora zaidi?
HAKUNA cha maana chochote utafanya Kama upande mmoja wapo CCM. CCM Ni Wahuni kuliko wahuni wenyewe wa Stand. CCM wanataka maridhiano ya kuvuka daraja la muda tu, sio maridhiano ya kudumu. Kwa vile CCM wao hawaumii, hivyo hawajutii. Wangelikuwa wanaumia na kujutia ya Mkapa yangewafundisha somo, hivyo wangeheshimu mwafaka uliopelekea maridhiano baadaye. CCM wanaweza wakaichezea Zanzibar wanavyotaka. Suruhu ya kudumu ya Zanzibar haitatokea chini ya CCM, yahitajika external force.
 

Mkuu kwamba wanaomba poo ni kwa sababu ya hiyo external force. Definitely si kuwa wanaomba poo kwa kupenda.

Kumbuka external force hii (nje ya CCM) ni bora zaidi kuliko nyingine yeyote ikiwamo ya Pompeo ambaye sasa hivi ni "no more.'
 
Namshauri M.Seif au upinzani uweke sharti la kurudiwa uchaguzi chini ya tume huru ndani ya miezi kadhaa kabla ya kukurupuka na maridhiano.

Tushafanya maridhiano miaka nenda miaka rudi, lakini tatizo liko pale pale mchakato wa uchaguzi hauna uwazi wa kuweza kuaminiana. Hii ni kutokana na upande mmoja kujaribu njia za ghilba kukaa madarakani.

Kama nia ipo, basi iwe ni ya tume huru na matokeo yake yakaheshimiwa. Hakuna asiefahamu kama CCM hawana nia ya kuheshimu demokrasia. Usanii wa mazungumzo na maridhiano uekwe pembeni.

Watu wametoza maisha na wengine wengi kuumia, halafu mnakuja hapa na usanii wa maridhiano! Tutizu chanzo cha tatizo kwanza, tujue kama uchaguzi unafanyika na referee/tume ni ya kuaminika.
 
Maalim anaouthubutu wa kukomaa nao.

Muda unapaswa kuwa mfupi na defined.
 
CCM ndo zenu baada ya kuapishana huwa mnakuja na maneno matamu na mazuri... kama ana ubavu aweke uchaguzi huru kura moja mtu mmoja... kila mwenye haki yake ya kupiga kura aruhusiwe kwa mujibu wa sheria na matokeo yasichakachuliwe tuone kama lile jengo pale Kisiwandui kama hawatoligeuza Gesti
 
Maalim anaouthubutu wa kukomaa nao.

Muda unapaswa kuwa mfupi na defined.
Ndo manaake, sifahamu maridhiano ya nini wakati wao wana jeshi. Washaleta ubabe wa kunyakua madaraka, sasa walete maendeleo tuu! Maridhiano ya nini tena ? Nina 100% akili za hawa watu zilipanga ubabe wa kunyakua madaraka na kusahau kama ukishakaa madarakani kwa njia izo za kizushi hakutakuwa na maendeleo.

Tukumbuke uchaguzi ukimaliza inakuja miaka 5 baada yake. Hakuna maana wala faida yoyote ya kufanya harakati za kunyakua madaraka kwa nguvu. Bila ya demokrasia na maendeleo pia tusahau, thats just a fact!
 
kwenye uchaguzi uliopita tuliona maiti nyingi za vijana wa Zanzibar waliouwawa kikatili kabisaa tena kwa kudhulumiwa haki zao za kikatiba na za msingi zikitapakaa mitaani, sasa basi ikitokea Maaalim Seif akakubali uteuzi wa aina yoyote kwenye hiyo kundi la wadhalimu kama alivyo wahi fanya huko nyuma umma wa wtanzania hatutamwelewa kwa namna yoyote ile, nasikia wameisha mtengea ndoano (umakamu wa raisi….)
 

Anaitibu ZANZIBAR na majeshi yake ya Tanganyika na ya kukodi kutoka Burundi.

Kijana huyo amepigwa risasi ya jicho, anasubiri kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…