Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Kwa maouvu aliyofanya Magufuli, si vema kuyafunmbia macho. Ameondoa freedom of speech, right to peaceful assembly, ameteka watu na wengine wamepotea hatuwaoni tena. Ameweka watu ndani kwa makosa ya uongo, ameua biashara n.k. Sasa utaachaje kumtaja?
Watu kama TBC, Polisi etc wanaotaka tushirikiane kuyanyamazia yabidi kuwatazama usoni kuona kama kweli hayo yatoka mioyoni mwao.

Kama yeye anaejiita msema kweli, hataki na analindwa asiambiwe ukweli kwa maovu anayotendea waTz wenzie, basi tuna dosari kubwa kama taifa.

Pia tukiendelea kuulea unafiki huo tutakuja ishia pabaya kama kule wajerumani waliolilea dubwana lililoitwa Hitler.
 
Nimesha subscribe ITV online. Kumbe ina mtangazaji kichwa namna hii. Yule Dada yupo Bright sana. Very cool and focused. Hongera ITV

Kiukweli huu ni mwaka wa tatu tangu niiangalie ITV. Nimeipenda bureeee
Ukweli kwa mahojiano hayo na umshiri wa mtangazaji ITV wamenirudisha. Nilishaanza kuitilia shaka wakati ilikuwa number one kwangu

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Zamani nilikuwa na utaratibu wa kusikiliza mijadala yote iliyokuwa ikirushwa na TVs zetu kuanzia kipindi cha Star TV 'Jicho Letu Ndani ya Habari'. Baadaye nilikosa 'interest' baada ya kuona kwamba baadhi ya washiriki wa mijadala hawakuonyesha kuwa na sifa au uwezo wa kujadili hoja na niliacha kufanya hivi kwa sababu kitu unachokiangalia au kukisikiliza mara kwa mara kinakuwa sehemu ya fikira zako. It's a pity kwamba msimamo wangu huu umefanya nikose mijadala mingi ya siku hizi, lakini kwa upande mwingine sipotezi sana has kwa kuzingatia aina ya michango baadhi yetu tuliyonayo hata humu jf. Lakini kitu ambacho ningeshauri kwa vijana wengi ni kujifunza namna ya kujenga hoja na kuwa 'independent/smart/intelligent thinkers'.
 
Well said and keep it up. 👍 👍👍
 
Paskali unajua ulichoandika kweli? Hivi ulifatilia kuapishwa kwa CAG baada ya Prof Assad? Magufuli alitamka wazi kama amepewa mamlaka ya kuteua basi anayo ya kutengua, na ndicho alichokifanya kwa Assad na ASSAD alithibitisha hilo alivyohojiwa na amka na bbc
 
Lissu ni kichwa, hataibiwa kura. Anaposema patachimbika kweli anamaanisha.
Hahaha Dah hi ni Tanzania Jamani Sio Nchi ya Kipuuzi kama wapuuzi mnavyofikili nyambafuu uchaguzi utaisha MAGU atashinda Sikh zitpita week zitapita na miaka itaenda na Mzee atastafuu Na nyie Msikwenda na uhalisia mtarudi JF kurujifurahisha
 
Nimesha subscribe ITV online. Kumbe ina mtangazaji kichwa namna hii. Yule Dada yupo Bright sana. Very cool and focused. Hongera ITV

Kiukweli huu ni mwaka wa tatu tangu niiangalie ITV. Nimeipenda bureeee

Exactly, she was cool and focused....

Lakini unajua ni kwanini?

Ni kwa sababu, kama angeanza kuleta za kuleta kama yule mtangazaji mwenzao Abdul Kambaya, angeanza kufundishwa kazi palepale...!

Kwa kifupi kumkaribisha mtu wa sampuli ya Tundu Lissu studio kwako ni lazima kituo kama kituo kijipange na zaidi sana mtangazaji anayeenda kumhoji...!!
 
Wewe NJAA ukiambiwa uthibitishe kwamba alichosema Lissu alikuwa anakisia tuu utaweza??? Sit down and drink your coffee,,acha kubwabwaja kaka.
 
Aliowataja acha watajwe kama wana ubavu wa kujisafisha na hizo tuhuma waende mahakamani ili kweli idhihiri.
Kufichiana makosa, mjuano, kuoneana haya ndio vimefikisha taifa hapa tulipo.
 
Hahaha Dah hi ni Tanzania Jamani Sio Nchi ya Kipuuzi kama wapuuzi mnavyofikili nyambafuu uchaguzi utaisha MAGU atashinda Sikh zitpita week zitapita na miaka itaenda na Mzee atastafuu Na nyie Msikwenda na uhalisia mtarudi JF kurujifurahisha
Pole sana,
Yaonekana shibe iko mezani kwa Jiwe, unamtegemea kiasi kuwa unaogopa na huwezi kujifungua ukafikiria itakuwaje ikitokea akaondoka.
Aina zenu ndio tatizo kubwa la nchi hii.
Miaka ya 70, wakati afya ya Rais wa kwanza waKenya, inaonyesha dalili za kuporomoka kutokana na umri mkubwa, Sir Charles Njonjo (Attorney General), kwa hasira alisimama bungeni na kuzuia mjadala wa kuandaa taratibu za kumpata wa kumrithi, uliyokuwa umeanza.
Bila ya aibu aliita ni uhaini hata kufikiria kifo cha Mzee Kenyata.
 
Huo mradi wa umeme wa upepo Singida umeanza lini?
 
Hapo kwenye Ukada ndiyo maana unaona kuwa ukweli hautakiwi kusemwa hadharani,ila unasahau vifungu vya Katiba yetu ya sasa vinavyoruhusu hilo.Wewe kama Mwandishi wa Habari&Mwanasheria unadhani ni sawa hayo yanayofanyika?Je,hufikirii kusimama uhesabiwe upande wa Haki na kuukataa Ukandamizaji(Udikteta)?Mwanataaluma kama wewe na wengine waliojisalimisha kwa watawala wakatili tuwaweke katika kundi gani la raia?Je,faida ya elimu mliyopewa na Taifa hili lilofanywa maskini na hawa hawa wanaowatesa wanyonge walipa kodi ni kuwa waoga?
Tunawasaidiaje Watanzania wenzetu ambao hawakupata nafasi ya kusoma elimu rasmi kama mimi na wewe kuufahamu Ukweli wa jinsi watawala wanavyoiharibu nchi hii kwa kasi ya mwanga?Watanzania wote wamejaa Hofu ya kushughulikiwa na watu wasiojulikana huku serikali ikiwa kimya,hali hii ni sawa kufanyiwa wananchi wa Taifa hili?Kunyimwa Haki ya kusema ukweli ni Utumwa mbaya sana.Tunaweza kubadili hali hii kupitia sanduku la KURA endapo tutaamua na kusimamia kura zetu ili washindi halali wapatikane bila kujali wametokana na chama gani cha siasa.
 

Nimekusoma na nimejaribu kufikiri....

Kwamba, laiti wewe ungekuwa ndiye mtangazaji uliyekuwa unamhoji Tundu Lissu kwenye kipindi hiki na ukawa na tabia ya kudakiza, kumtoa kwenye reli jamaa na mambo kama hayo ili mradi umvuruge na asieleweke kwa hadhira yake ,..

For sure, msingeelewana na Tundu Lissu angekugeuka papo hapo na kuanza kukufundisha kazi yako ya uandishi/utangazaji....!!

By the way aliyetajwa kwa jina ni Jaji Francis Mutungi - Msajili wa Vyama vya siasa kwa sasa...

Sasa what's wrong with that? Na sheria si ni kweli inaelekeza hivyo kuwa Msajili wa vyama vya siasa ndiyo ataamua iwe "ndiyo" au "hapana" kwa kile vyama vinavyoungana vinavyoamua kuungana na kukubaliana?

Na je, si ni kweli kwa sasa Msajili vyama vya siasa ni Jaji Francis Mutungi kwa sasa?

Sometimes Pascal Mayallah huwa hueleweki kidogo au pengine huwa unaamua kuuvaa ujinga kwa makusudi tu, right?
 
Huwezi kusema Lissu amemhisi aliuemyaja unless nawe huenda huna ushahidi na unachokisema.

Unaconclude nini kitu Usichokijua Ndugu mwanahabari Nguli Pascal Mayalla . Lisu amemtaja, Je akikuletea ushahidi utasemaje? we ndo utaonekana umemhisi Lisu Hana ushahidi kumbe yeye anao ushahidi wa anachokiongea

Nini na Maanisha kwa mtu msomi you have to think very critical before arguing. Sio kila Jambo ni kulisemea na kutolea ufafanuzi Kama ni offensive action bila kusikiliza conflicting parts katika Jambo Hilo unalolisemea. Tujifunze kuwa na subra ya mambo

Kwahiyo nilitaka tu kuweka sawa kwamba usimhisi Kuwa Lissu hans ushahidi km Lisu anavyowahisi wateule kupata maelezo toka juu
 
Tz hakuna Amani kuna utulivu kidogo tu. Kwani nchi hii anaemiliki jeshi na vyombo vyote vya usalama nasilaha zote ni nani kama siyo CCM na serkali yake.Pakichimbika ni serkali imesababisha yote hayo.na ikibid pachimbike tuu ili angalao nchi hii tuheshimiane kidogo.upuuzi umezidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…