Hongera Joh Makini na Weusi kwa kutojishughulisha na kampeni

Hongera Joh Makini na Weusi kwa kutojishughulisha na kampeni

masare

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,791
Reaction score
1,830
Pongezi kwa kusimamia weledi wa fani yenu. Nakumbuka tangu Uchaguzi Mkuu wa 2010, 2015 na wa mwaka huu mmeendelea na msimamo wenu wa kutotumika kupiga kampeni kwenye upande wowote wa siasa.

Hii ni nzuri sana ili kutowagawa mashabiki wenu.

Keep it up
 
Kampeni hazijaisha mkuu, na kwa ubabe wa chama kile hao jamaa wakihitajika hawapindui, muda ni hakimu mzuri sana
 
Pongezi kwa kusimamia weledi wa fani yenu. Nakumbuka tangu Uchaguzi Mkuu wa 2010, 2015 na wa mwaka huu mmeendelea na msimamo wenu wa kutotumika kupiga kampeni kwenye upande wowote wa siasa.

Hii ni nzuri sana ili kutowagawa mashabiki wenu.

Keep it up
Watakufa njaa. Mwana Muziki ni sawa na mchezaji wa mpira, Leo yanga kesho simba. Yeye kikubwa maslahi upenzi baadaye. Hivyo hao unaowasifia ni wajinga
 
Hongera kwao! Ila nina ombi kwa Mgombea Urais wa CCM! baada ya uchaguzi mkuu, iwe mmeangukia pua au la! Mumkumbuke Peter Msechu kwenye ufalme wenu.

Yule jamaa anawapambania jukwaani aisee! Na kile kitambi, akiimba ule wimbo wake wa 'nyota na ing'ae' ! Utamuonea huruma.
 
Pongezi kwa kusimamia weledi wa fani yenu. Nakumbuka tangu Uchaguzi Mkuu wa 2010, 2015 na wa mwaka huu mmeendelea na msimamo wenu wa kutotumika kupiga kampeni kwenye upande wowote wa siasa.

Hii ni nzuri sana ili kutowagawa mashabiki wenu.

Keep it up
Nyie badae ndio mnaanza utasikia msanii fulani kumbe hana hata gari. Kipi bora akuangalie wewe shabiki ambaye huzijui hata digital platform zake anakouza nyimbo. Shout out kwa wasanii ambao wanafanya kazi waingize kipato
 
Watakufa njaa. Mwana Muziki ni sawa na mchezaji wa mpira, Leo yanga kesho simba. Yeye kikubwa maslahi upenzi baadaye. Hivyo hao unaowasifia ni wajinga
Wanaogopa kupigwa mawe huku chuga.

Chuga kila 'msela' ukimchanja kiwembe damu yake ni upinzani!

Hatutaki mbanga za kiduanzi!
 
Its all about pro and cons;

Kwahio kama pesa unayopewa inatosha kukuambia useme nyeusi ndio nyeupe chaguo ni lako, ila kumbuka faida yake ni short term..., ila kama unajua nyeupe kweli ni nyeupe basi hata bila malipo unasimamia kile unachokiamini....

Mara nyingi wasanii ni sauti za watu wa chini, watu wasiokuwa na sauti..., ndio maana mara nyingi wanakuwa upande wa upinzani, sababu asilimia kubwa ya watawala/walio madarakani huwa wanalewa madaraka na kuwasahau watu (na ukiangalia ni vigumu kukosa injustice ya kuongelea) sasa ukitumika kuwaambia watu kwamba hili ni sawa wakati sio sawa au hauna uhakika kama itakuwa sawa basi na wewe unakuwa ni kibaraka wa wenye madaraka....
 
Pongezi kwa kusimamia weledi wa fani yenu. Nakumbuka tangu Uchaguzi Mkuu wa 2010, 2015 na wa mwaka huu mmeendelea na msimamo wenu wa kutotumika kupiga kampeni kwenye upande wowote wa siasa.

Hii ni nzuri sana ili kutowagawa mashabiki wenu.

Keep it up

Mleta mada, elewa ya kwamba muziki ni ajira na mwanamuziki hachagui wapi pa kuimba alimradi tu ufike dau analolitaka. Wasanii hawana uanachama wa hivyo vyama badala yake wao wanalipwa kuburudisha. JARIBUNI KUWA WAELEWA WATU WANATAFUTA MLO EBHO..!!

Kuna masupastaa wakubwa tu wanatumbuiza mpaka kwenye birthday party, wedding party nk wanachoangalia ni je umefika kwenye dau,, kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja ana vichenji vya kutingisha jiji ilikuwa 2016 alialikwa Christian Bella kuperform na akaja kupiga show thou kwa dakika ambazo hazikuzidi 20

Pia sio wote wamepata shavu la kusaini mkataba wa kutumbuiza kwenye kampeni, kuna wengi hawajapata dili hilo na wanatamani kweli kweli

Mwisho nakukumbusha tu, kampeni bado hazijaisha bado kuna wasanii wataperform kwenye maeneo ambayo yana influence kwao

na pía Diamond na Kiba walikula shavu kuperform 2015 karibia sehemu nyingi za kampeni ya CCM na bado wasanii hao kuanzia nyakati hizo mpaka hivi sasa wamezidi kujiongezea idadi kubwa ya mashabiki
 
Back
Top Bottom