Mleta mada, elewa ya kwamba muziki ni ajira na mwanamuziki hachagui wapi pa kuimba alimradi tu ufike dau analolitaka. Wasanii hawana uanachama wa hivyo vyama badala yake wao wanalipwa kuburudisha. JARIBUNI KUWA WAELEWA WATU WANATAFUTA MLO EBHO..!!
Kuna masupastaa wakubwa tu wanatumbuiza mpaka kwenye birthday party, wedding party nk wanachoangalia ni je umefika kwenye dau,, kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja ana vichenji vya kutingisha jiji ilikuwa 2016 alialikwa Christian Bella kuperform na akaja kupiga show thou kwa dakika ambazo hazikuzidi 20
Pia sio wote wamepata shavu la kusaini mkataba wa kutumbuiza kwenye kampeni, kuna wengi hawajapata dili hilo na wanatamani kweli kweli
Mwisho nakukumbusha tu, kampeni bado hazijaisha bado kuna wasanii wataperform kwenye maeneo ambayo yana influence kwao
na pía Diamond na Kiba walikula shavu kuperform 2015 karibia sehemu nyingi za kampeni ya CCM na bado wasanii hao kuanzia nyakati hizo mpaka hivi sasa wamezidi kujiongezea idadi kubwa ya mashabiki