G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Mimi binafsi na watu kama kina Pascal Mayalla ni watu ambao tulijiweka kando kabisa na mada za kisiasa baada ya uchaguzi mkuu 2020. Hata hivyo nilikuwa nikipita ndani ya jukwaa hili kimya kimya na ilibidi tuchangie pale tunapojisikia. Mimi ni moja wa watu humu ambaye huenda ningepotea kabisa kama mwendazake angebaki hadi 2025 na kisha kuongeza muda kama ilivyokuwa imepangwa.
Nina furaha jukwaa letu pendwa limerudisha afya. Nilipokuwa napita humu kimyakimya na kuangalia mada zilizopo siyo sawa na sasa. Tumepta afya na tujipongeze kwa hilo.
Aidha ni furaha sana pia hata wale MATAGA wameanza kurudi kwenye mstari na hivyo mada za kuchangamsha jukwaa zimewadia upya. Leo tunashuhudia hata kina Kigwangala wameamua kutema ndoano ya kuabudu, wananena ukweli.
Itoshe kusema ukweli kuwa Mungu anaipenda Tanganyika, anawaonea huruma watu wake ambao walilala na kuamkia vitisho vya "Ole wenu mjaribu" Ninasema Mungu ashukuriwe.
Kuimaliza 2025 na giza lillilokuwa linafuatia kabla ya muda wenyewe ni muujiza. Lolote litakalonenwa sasa ni kuwa ukweli ni kwamba kuna "relief" na inaonekana wazi wazi.
Hutaki unaacha!