Hongera jukwaa la siasa kuinuka tena. Ama kwa hakika huu ni mwanzo mpya

Hongera jukwaa la siasa kuinuka tena. Ama kwa hakika huu ni mwanzo mpya

Afadhali wewe ni kuanzia 2020. Mimi tangu 2015 niliachana na haya mambo ya hili jukwaa. Kwa kipindi chote sikuwahi kununua wala kusoma gazeti, kusikiliza habari au TV wakati wa taarifa ya habari au kusikiliza radio za kimataifa kama BBC, VOA na DW...
Siasa kwa ujumla wake zitakuwa na mwamko mpya pale tu itakapopatikana Katiba Mpya, kinyume na hapo tutaendelea kujadili mambo yale yale, ni either "dhaifu" au "dikteta" till the end of time, nothing new here, tuna pass time tu.
 
Bado kidog of course, tutafika mahali haitakuwa danger ku reveal identity yako ukipenda. Kweli sasa hivi posts zinaachwa ambazo wakti wa mwendazake usingelithubutu.

Sabaya na wenzake wana kesi nyingi za kujibu...... wamefanya atrocities nyingi, Sarungi maria anapokea waliootea majina yao. Asingeliweza kuandka hivyo nyuma wanmgelimfuata kama Azory (RIP) au bado anaishi amefchwa which is quite unlikely
 
Siasa kwa ujumla wake zitakuwa na mwamko mpya pale tu itakapopatikana Katiba Mpya, kinyume na hapo tutaendelea kujadili mambo yale yale, ni either "dhaifu" au "dikteta" till the end of time, nothing new here, tuna pass time tu.
Uko sahihi. Tutakuwa tuna deal na mtu badala ya system
 
Mimi binafsi nilikuwa nishajiapiza km magufuli angeongezewa muda 2025 ningehama nchi na kuhamia nakuru kenya.
 
Hata mods waliingia woga kwa kufuta nyuzi nyingi sisizo mfuraisha farao/herode
 
napitia comments nikiwa na sahani yangu iliyosheni pilau na minyama ya kutosha mixer Pepsi baridi kabisa...maana hii ni moja kati ya sikukuu yangu bora kabisa ktk kipindi cha miaka mitano iliyopita!!!!!
We kama mimi tofauti yetu ni we we una Pepsi baridii mi Nina kachupa kadogo ka konyagi.
 
Najisifu kuwa mmoja wa watu tuliompinga jiwe humu jukwaani bila uoga hata kama natumia fake id tangu 2015 alipochukua fomu
 
Bora mwendazake aondoke tu, kunamfumo fulani wa kijinga sana alikua anataka kuutengeneza nashukuru Mingi katuepushia hilo. Ilifikia mahali hata polepole anakuwa na kauli za kipuuzi kwa Wananchi. Mama pangua sukuma gang yote washamba watupu waliotaka kutuingiza shimoni
Kauli kama hizi.
 
Huu ni upuuzi na kukosa hekima.
Hapa ni wale waliojeruhiwa na mnyama baada ya kuingia kwenye anga zake.
Yaani uibe tukuangalietu, uajiriwe kiundugu tukuangalietu, vyeti vyako havifai unataka uwe afisaa mkubwa lazima upigwetu.
 
Uko sahihi. Tutakuwa tuna deal na mtu badala ya system
Exactly, akili zimeshadumaa, ndio maana siku hizi humu ndani vinaibuka vikundi vya ku-support watu badala ya institutions, inshort tumeshaanza ku deal na watu.
 
Mimi siwezi kufurahia kifo cha mtu yeyote, lakini nilikuwa naomba sana tumpate kiongozi mkuu mwingine wa nchi. Kiongozi mwenye hekima, mwenye utu, anayetambua kuwa yeye ni hinadamu kama walivyo binadamu wengine, kiongozi anayejua kuwa hana mamlaka ya kuondoa uhai wa mtu, kuteka au kuwapoteza watu kwa vile tu wamekosoa. Tumpate kiongozi mwenye kupenda haki, anayeheshimu katiba na sheria, asiye mnafiki wala laghai. Asiyeweza kufanya ulaghai kwenye mifumo yetu ya uchaguzi.

Rais Magufuli ameondoka, imebakia historia. Aliyoyatenda, ni yeye ma aliye mkuu kuzidi sisi sote. Lakini tuendelee kuomba maana mifumo na sheria mbaya bado zimebakia vile vile. Waliochukua madaraka, wanaweza, kwa dhamira njema, kubadili ili watu waongozwe kwa haki:

Katiba ya wananchi
Tume huru ya uchaguzi
Sheria gandamizi

Tusiache kuomba kwaajili ya haki ya Watanzania. Mh. Samia, hayo mambo matatu ayafanyie kazi. Kutoyafanyia kazi, hasira ya Mungu haitakoma kwa wanaodhulumu haki za wananchi.

Marehemu ana utu na roho sawa kama Ben Saanane, kama Azory Gwanda, kama yule diwani kupitia CHADEMA wa Dar na Kilombero, sawa na Mdude na TL walioponea kwenye tundu la sindano. Kama tumeumizwa na kifo cha Rais Magufuli, tuumizwe sawa na vifo/kupotea kwa Saanane, Azory, Mawazo, na wale wote waliouawa kwa kuchinjwa kama kuku, huku baadhi ya wanaCCM shetani wakishangilia.

Utu wetu na uhai wetu vivuke hisia na ushabiki wetu wa kisiasa. Uhai na utu wa Mtanzania yeyote, bila ya kujali cheo chake, chama chake, dini yake, umri wake na hali yake, vina thamani sawa mbele za Mungu. Tunaweza kumpamba sana marehemu, kaburi lake, jeneza lake, na bendera nusu mlingoti, na nyimbo nyingi nzuri, lakini kama alikuwa na mkono katika vifo vya wasio na hatia, ni kazi bure - waliodhulumiwa watakuwa mbele yake wakimsuta kwa uovu mbele ya mahakama isiyo na upendeleo, ya Baba Mungu wetu.

Niliomba sana, tumpate kiongozi mwingine atakayerudisha amani ya mioyo kwa Watanzania wote. Kiongozi mwenye kutambua kuwa kwa yeye kuwa kiongozi haimaanishi anafahamu kila kitu kuwazidi Watanzania wote kwa umoja wetu. Kama Mwenyezi Mungu ameamua kujibu maombi yetu kwa namna hii, basi hatuna uwezo wa kuhoji hekima yake.

Mungu wetu atusaidie, tunyanyukapo na kupanda, iwe kwa vyeo, mali au namna nyingine yoyote, tusipungukiwe hekima, tukajisahau na kuamini kuwa ubinadamu wetu nao umepanda dhidi ya ubinadamu wa watu wengine.
 
Najiuliza hivi kwanini watu ni wabinafsi sana ?
kwanini watu hawana umoja?
Mfano mtu mmoja tu anatengeneza mtazamo wake binafsi wa kutawala watu milioni 60 na anafanikiwa kwa kutumia haohao watu anao watawala kuendelea kuwa na nguvu

Kama umewahi kuona simba mmoja katikati ya maelfu ya nyumbu na bado simba akawa ni shujaa kwa kufanya anavyotaka kwa mafanikio kabisa hiyo ikafanya uwadhara wanyama nyumbu inabidi waombe radhi kwa dhati kabisa kwa kuwa wale ni bora mara elfu kuliko sisi ambao kwa mamilioni yetu na utashi wetu lakini tumekuwa under control na kichwa kimoja tu
Nadhani utakuwa umesahau yaliyomkuta Lissu.
 
Back
Top Bottom