Hongera Kenya , Hongereni wakenya , Nakulilia Tanzania

Hongera Kenya , Hongereni wakenya , Nakulilia Tanzania

TZ mpira ulikufa toka miaka ya 1970 kilichobaki ni ubishi na mazoea tu. We umeona wapi mtu kama Mze Akilimali asiye na mchango wowote ndani ya timu eti anaogopewa na kama abugiii ugoro basi timu haiendi kucheza.

Sisi ni mabingwa wa kuua kila kitu
  • viwanda tumeua
  • elimu tumeua
  • michezo tumeua
  • reli tumeua
  • shirika la ndege tumeua
  • NASACO likewise
  • ...
 
Mpira Tanzania hakuna ni kelele tu, hii mechi bora hata ingepelekwa tu Kenya uwanja wetu unatumiwa na wageni na kila siku tunajisifu eti tuna ligi bora upuuuuzi mtupu.
 
Tatizo la Tanzania ni TFF na Siasa mpirani
 
Ni kwel mkuu..

Sent from my itel_it1503 using JamiiForums mobile app
 
Naangalia game ya Timu ya Gor-Mahia ya Kenya dhidi ya Timu kali ya Everton kutoka Uingereza kupitia EATV hapa kwenye uwanja wa maonesho wa sabasaba , Hakika mna kila sababu ya kutembea kifua mbele .

Timu yenu ni nzuri na kiukweli inastahili kuiwakilisha East Africa kwenye game hii , hongereni sana wakenya .

Huku kwetu Tanzania mpira unachezwa zaidi na viongozi , ndani ya uwanja , nje ya uwanja na mahakamani , kwetu kununua mechi ni jambo la kawaida sana ! Waamuzi kununuliwa siyo siri tena .

Soka la Tanzania limedumaa mithili ya MTOTO ALIYEBEMENDWA ! hivi ninavyoandika haya viongozi wa TFF wako mahakamani kwa sababu zinazofahamika kama FITNA ZA UCHAGUZI ! Yaani viongozi wa soka wanapangwa kutoka nje ya soka lenyewe , aibu sana !

Wakenya endelea kuongoza , sisi tutaendelea kuburuza mkia .
Wewe Nawe njiti wa mawazo, hebu mwambie huyo Gor mahia acheze na simba au yanga kama atapona

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Ungeangalia kupitia channeli nyingine si ndo ungechanganyikiwa zaidi... ITV/EATV walishindwa kabisa (kama timu zetu tu) minimum standards za kurusha mechi kubwa kama ile..!!
Everton Tv walikuwa live na ilibamba sana..

Anyway; kurudi kwenye hoja.. Tanzania sisi tunaweza kutumbuana, kuchongeana na bongofleva make ndo vitu tumebuni wenyewe..!!
 
Mpaka wale wazee, wajuaji wakina manara na wenzake watoke pale ndo mpira utaendelea,... Ii inchi ina vinara wa wajuaji wakati hamna kitu wanachojua,.. Mi nashangaa pale clouds ndo wajuaji kumbe hamna kitu kabisa
 
Michuano ya club bingwa Africa, Gormahia wanafikaga wapi? Vipi kuhusu timu ya taifa Kenya? Sisi wote ni wale wale tu mkuu
 
Wewe Nawe njiti wa mawazo, hebu mwambie huyo Gor mahia acheze na simba au yanga kama atapona

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
Sasa walishindwaje kucheza na everton ?
 
Kocha wa Gormahia ni yule liyetimuliwa na simba kwa kuonekana hajui
Maskini kumbe Simba ndo hawajui
Unapokuwa mwalimu darasani ukafelisha watoto hata kama wao ndo hawana akili lawama huenda kwa mwalimu. Sometimes mwl hata ufanyeje, kama shingo za wanafunzi zimebeba maboga yatabaki hvohvo.

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Nina super market Nairobi mjomba , usione tuko humu hatuna njaa hata chembe , tumejitolea tu kusaidia hawa masikini wanaoendelea kukamuliwa hadi damu .
Labda super market ya dangaa junia moja
 
Labda super market ya dangaa junia moja
Kwa hapa Tanzania nina kiwanda , ambacho lengo kuu la kuanzishwa kwake lilikuwa kutoa ajira kwa watanzania wenzangu wanaonyanyaswa na vijiajira uchwara ndani ya nchi yao.

Nachukua nafasi hii kukushauri hata wewe upeleke maomba kwa HR wetu , tutakusaidia .
 
Hahahaha.... mimi ukiniajiri nitakuibia ufirisike bure!
 
Michuano ya club bingwa Africa, Gormahia wanafikaga wapi? Vipi kuhusu timu ya taifa Kenya? Sisi wote ni wale wale tu mkuu
Ukiisoma nafsi ya mleta Uzi ....hakumaanisha kuwa Gor ndio timu bora Afrika Mashariki...

Lengo kuu ni kuwakosoa Simba na Yanga kwa kudharau michuano hii.

Ukiniambia Gor ni timu bora, ntakuuliza Mara ya mwisho wametinga Group Stage kwa CAF Champions League lini? Utagoogle kwanza na kupata jawabu.
 
Back
Top Bottom