Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Nimewaangalia Rais Uhuru Kenyatta, Makamu wake William Rutto, Viongozi Wa upinzani mgombea urais toka NASA na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka.

Viongozi hawa Wa Wakenya, wameombana msamaha mbele ya wakenya, kwa yote walioshutumiana kwa kipindi chote cha uchaguzi na kuamua KUSAMEHEANA na kuungana kuipigania Kenya.

Nimefurahi kuona wanadamu wakisameheana, ila nimechukizwa kuona kwann Wakenya wamekuwa Wa kwanza kulifikiria hili.

Sisi tunakwamia wapi? Wakenya wanavyotamba kuwa wao ndo bora Afrika Mashariki, tukifuatia Tanzania kisha Uganda.

Nilikuwa mbishi sitaki kuamini kabisa nikiamini sisi ndo bora nikikiamini KISWAHILI lkn kumbe kina ujanjaujanja mwingi.

Naomba sana hili ni zuri saana japo tumetanguliwa ustawi Wa taifa huanzia hapo.

Mfumo Wa vyama vingi si uadui.
 

Attachments

Wewe nae umetoka kulala sijui. Hujawahi ona Lowasa na Magufuli wakiongelea maendeleo?

Kuombana msamaha inategemea jinsi gani mulikuwa mumekosana. Kenya watu wengi sana walikufa ndo maana wanaombana misamaha .. Pili kuna ukabila mkubwa sana usiombe ukaingia hapa TZ.
Endelea kubaki usingizini ..Wapinzani wakiunga mkono juhudi za raisi upizani unalia kufa.. Hilo la Uhuru na Odinga je? Linauwa upinzani Kenya?
 
Si umeona lugha yako, anyway ndivyo ulivyoumbwa na Mola wako, kuona kwamba binadamu wenzio ni Wa kukejeliwa.

Angalia clip, fungua ufahamu wako ,acha chuki. Huwezi kufananisha kukutana kwa Mh Rais JPM na MH EL ukafananisha na huu.

Sikiliza nn wanasema kisha oanisha ulichokisikia MH JPM na EL walichosema walipokuwa wanaagana.

Angalia wabunge wanavoparurana msikilize MH JPM kila siku anasisitiza yeye ndiye RAIS Wa nchi hii, maendeleo hayana vyama.

Fikiria.
 
Tanzania haina cha kujifunza Kenya ila Kenya wana cha kujifunza Tanzania

Full stop
 
Odinga was bought by uhuru.
Five years from now, Kenya will be divided again.

This happened after 2008 election war.
 

Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza. Haya ndio mambo ambayo nchi yetu ilikuwa inasifika sana. Tanzania ilikuwa ndio nchi ya Africa iliyokuwa kimbilio kwa wale wenye magomvi na kutokuelewana wakaja Tanzania kupatanishwa. Vyama vya wapigania Uhuru kama ZANU na ZAPU viliweza unganishwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere ikatoka Patriotic Front nakumbuka Mwalimu pia alijaribu sana kuweza kuunganisha ANC na PAC vyama vya ukombozi wa Afrika kusini kipindi kile lakini naona pale hakufanikiwa lakini juhudi zilifanyika. Na najua wako wengine wengi wanaweza kuja na mifano mingi ya kuonyesha jinsi gani nchi yetiu ndio ilikuwa muubiri na mtekelezaji wa dhana ya Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu. Tuliimba hizi nyimbo shule za msingi na kweli tulifanikiwa sana kujenga nchi moja yenye mshikamano usiojali dini, ukabila au rangi. Nafikiri hili tunahitaji kuliweka kama ndio msingi Mama kadri tunavyozidi kwenda mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania yetu. Leo Kenya wamegundua kuwa utengano ni udhaifu. Watanzania tufungue macho na masikio tunayaone na kuyasikia haya na bila kuyapuuzia, kwa sababu ukweli hata siku moja haupuuzwi kama una nia ya kweli ya kuboresha na kujifunza.
 
Ni kweli wamefanya vizuri lakini pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa siasa ni mchezo mchafu sana, wakenya wengi wamepoteza maisha kwa vuguvugu hizi, lakini leo kiurahisi tu watu wanashikana mikono eti wanasameheana, vipi kuhusu waliopoteza maisha? Ni siasa za maji taka hizo.
 
Uhuru Kenyatta ni rais ambae anajua nini maana ya uongozi amelelewa ikulu hana ushamba kuhusu uongozi.
Ameelewa somo baada ya kammpuni zake wanachama wa raila kususa kununua bidhaa zake Na kujikuta akila hasara ya uhakika kaona yaishe.Hapo Ni business interest zake zimeguswa akaona isiwe nongwa aombe msamaha yaishe ili wafuasi wa Raila waendelee kununua bidhaa za kammpuni zake
 
Nakubaliana na wewe kabisa, lakini pia kuna mbadala wake ambao ni kukaa na uadui na kila kundi kulinda kambi yake ambapo matokeo yake ni mabaya Zaidi. Tunaweza kujadili pia mantiki ya ile tume ya maridhiano ya Afrika Kusini (Truth and Reconciliation Commission ya Desmond Tutu), zote ni kazi binadamu hazina utimilifu. Ni katika jitihada ya kufanya lililo bora na lenye hekima na tumaini la Maisha bora ya kesho. Ni kuchagua kati ya shetani wa wawili yupi mwenye afadhari. Nafikiri..
 
Kwahiyo Bidhaa zitauzika kwelikweli
 
Nakala iwafikie wafuasi wa Lowasa aliyekutana Na Magufuli Na wale wapiga kura wa chadema kinondoni uchaguzi wa 2015 waliohangaika Na mbunge wa UKAWA Mtulia
 
Uhuru ni mwanasiasa mkomavu sana. Nahisi kuwa mtoto wa raisi wa zamani nako kumemfanya akakomaa tokea akiwa mtoto. Anajua maana ya demokrasia na mfumo wa vyama vingi.

Ingekuwa hapa kwetu akina babaa odinga siku mingi kama wasingerestishwa in peace basi labda wangekuwa kusikojulikana au jela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…