Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza. Haya ndio mambo ambayo nchi yetu ilikuwa inasifika sana. Tanzania ilikuwa ndio nchi ya Africa iliyokuwa kimbilio kwa wale wenye magomvi na kutokuelewana wakaja Tanzania kupatanishwa. Vyama vya wapigania Uhuru kama ZANU na ZAPU viliweza unganishwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere ikatoka Patriotic Front nakumbuka Mwalimu pia alijaribu sana kuweza kuunganisha ANC na PAC vyama vya ukombozi wa Afrika kusini kipindi kile lakini naona pale hakufanikiwa lakini juhudi zilifanyika. Na najua wako wengine wengi wanaweza kuja na mifano mingi ya kuonyesha jinsi gani nchi yetiu ndio ilikuwa muubiri na mtekelezaji wa dhana ya Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu. Tuliimba hizi nyimbo shule za msingi na kweli tulifanikiwa sana kujenga nchi moja yenye mshikamano usiojali dini, ukabila au rangi. Nafikiri hili tunahitaji kuliweka kama ndio msingi Mama kadri tunavyozidi kwenda mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania yetu. Leo Kenya wamegundua kuwa utengano ni udhaifu. Watanzania tufungue macho na masikio tunayaone na kuyasikia haya na bila kuyapuuzia, kwa sababu ukweli hata siku moja haupuuzwi kama una nia ya kweli ya kuboresha na kujifunza.

Wengi wenu hamjui siasa za Kenya. Siasa za kenya ziko hivi hivi tangu wapate uhuru. Leo huyu anafanya ushirika na yule, Kesho wamekosana, keshokutwa aliyekuwa adui wa fulani ndiye mpiga debe wake mkubwa! Kwa kifupi wanajali matumbo yao na kila kitu wanachofanya wanakuwa wameweka maslahi ya matumbo yao mbele! Hivi nikikumbia kabla Uhuru hajachaguliwa kuna siku alienda nyumbani kwa Odinga wakiwa na familia yake na wakashinda wote huku wakila na kunywa utaamini? Siasa za Kenya siyo za kupigiwa mfano hata siku moja.
 
Pamoja na moyo wa upekee wa Rais Kenyatta bado siasa za Kenya ni ngumu sana kwasababu ya ukabila.Ndio maana Kenyatta anajaribu kwenda nao sawa.Bravo Kenyata,Bravo Kenya!
Kenyatta hajafanya lolote kupunguza ukabila. Nyie hamjui siasa za Kenya hata kidogo. Ndiyo mmeanza kuziona sasa hivi.
 
bora jiwe kuliko uhuni wa wakenya mkuu... hao hawajawai na hawatakuwa wapinzani.. watoto wa ikulu hao... wamekuwa pamoja.. ni wasanii tu... Wanatumia ujinga wa watu kuongoza Kenya... Bora ya jiwe kuliko uhuni wao
Raila mtoto wa Makamu wa Raisi Wa kwanza Kenya Odinga Odinga Kenyatta mtoto wa Raisi wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta wote watoto wa Ikulu wamezaliwa Ikulu Magufuli hajazaliwa Ikulu hatuna cha kujifunza kwa Hao watoto waliozaliwa Na kukulia Ikulu.masingasinga hujuana kwa vilemba Na rangi.Ya Kenya waachie wenyewe
 
Uhuru amekulia marekani na ameiona kwa macho jinsi democrasia halisi inavyofanya kazi. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa kenyata
 
Ukweli mtupu.....
 
Uhuru amekulia marekani na ameiona kwa macho jinsi democrasia halisi inavyofanya kazi. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa kenyata
ijue siasa ya kenya mkuu... Hao wa2 sio wapinzani.. wanalindana kwa kisingizio cha upinzani kanjanja...
Shukuru TZ tunamegana ukweli chadema na CCM (hata kama matokeo huwa yanakuwa edited na CCM)... Tafuta video ya kuapishwa Uhuru Raila alikuwa anacheza muziki kama kawa
 
Ni kweli wamefanya vizuri lakini pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa siasa ni mchezo mchafu sana, wakenya wengi wamepoteza maisha kwa vuguvugu hizi, lakini leo kiurahisi tu watu wanashikana mikono eti wanasameheana, vipi kuhusu waliopoteza maisha? Ni siasa za maji taka hizo.
Hilo ni fundisho sio kufuata mkumbo, ndio maana watanzania wengi sio washamba au waoga wanajitambua kwa hili. Jamaa Kigoma alipigwa kwenye maandamano na kufungwa jela miaka kadhaa kisa Kaburu (rip) baada ya kutumikia kifungo anarudi uraiani anamkuta Kaburu mwenyekiti wa CCM, hii ilitoka humu humu JF, wenzao wapo kimaslahi zaidi Ni kuwapuuza tu.
 
bora jiwe kuliko uhuni wa wakenya mkuu... hao hawajawai na hawatakuwa wapinzani.. watoto wa ikulu hao... wamekuwa pamoja.. ni wasanii tu... Wanatumia ujinga wa watu kuongoza Kenya... Bora ya jiwe kuliko uhuni wao
Jiwe lingeweza kuwa juu sana kama lingeacha shughuli za kidemokrasia za vyama vya siasa ziendelee kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa. Tatizo lake linataka liongee lenyewe tu na chama chake ndio maana linaitwa lidikteta uchwara.
 
Ameelewa somo baada ya kammpuni zake wanachama wa raila kususa kununua bidhaa zake Na kujikuta akila hasara ya uhakika kaona yaishe.Hapo Ni business interest zake zimeguswa akaona isiwe nongwa aombe msamaha yaishe ili wafuasi wa Raila waendelee kununua bidhaa za kammpuni zake
Asante sana
Hapo ndipo watu wengine wanashindwa kuielewa Kenya!
 
Wengi wenu hamjui siasa za Kenya. Siasa za kenya ziko hivi hivi tangu wapate uhuru. Leo huyu anafanya ushirika na yule, Kesho wamekosana, keshokutwa aliyekuwa adui wa fulani ndiye mpiga debe wake mkubwa! Kwa kifupi wanajali matumbo yao na kila kitu wanachofanya wanakuwa wameweka maslahi ya matumbo yao mbele! Hivi nikikumbia kabla Uhuru hajachaguliwa kuna siku alienda nyumbani kwa Odinga wakiwa na familia yake na wakashinda wote huku wakila na kunywa utaamini? Siasa za Kenya siyo za kupigiwa mfano hata siku moja.
Nakuelewa sana Mkuu na hicho ndio kiini cha siasa bahati mbaya, UWONGO, UNAFIKI na FITINA kwa kiwango kikubwa. Ila tunachosema msingi iwe uzalendo kuweka maslahi ya Taifa mbele hivyo kujenga mazingira chanya (Amani na mshikamano) kuweza kujenga nchi. Hali halisi za siasa zetu za dunia ya tatu tunazijua. Lakini kitendo cha mwanasiasa kuweza kusema nimekosea naomba kusamehewa hata kama ni katika kulitumikia tumbo, lakini linaleta mshikamo kwa wananchi na kupunguza uhasama kwa wafuasi wao.
 
Narudia Tanzania hakuna cha kujifunza Kenya ila Kenya ina cha kujifunza Tanzania

Tanzania inaweza isaidia Kenya kwenye usuluhishi wa migogoro ila Kenya haina uwezo huo

Wewe mla githeri huwezi elewa
Fala sana. Sina cha kuzungumza na asiyejielewa
 
Wakenya wanajitambua,wanaondoa tafauti zao za kisiasa kujenga nchi yao,bila Umoja hakuna maendeleo,hawa watu wametupita kwa viwanda,sasa wanatupita kisiasa,wanatupita katika kuitekeleza demokrasia ya kweli,wakati Tanzania ndio kwanza wanaanzisha siasa za kuwaadhibu na kuwauwa wanasiasa wa vyama vya upinzani, Wakenya wao wanapatana kisiasa wanaondoa tafauti zao kwa madhumuni ya kujenga nchi yao..
Hongera Kenyatta..."You are truly politician "
Angeomba huo msamaha ile awamu yake ya kwanza alipopelekwa the hegue ndio ningemuona kamaanisha ila kaomba awamu ya pili anamalizia gwe yake , hiyo ni siasa na biashara ndani yake tu
 
Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza. Haya ndio mambo ambayo nchi yetu ilikuwa inasifika sana. Tanzania ilikuwa ndio nchi ya Africa iliyokuwa kimbilio kwa wale wenye magomvi na kutokuelewana wakaja Tanzania kupatanishwa. Vyama vya wapigania Uhuru kama ZANU na ZAPU viliweza unganishwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere ikatoka Patriotic Front nakumbuka Mwalimu pia alijaribu sana kuweza kuunganisha ANC na PAC vyama vya ukombozi wa Afrika kusini kipindi kile lakini naona pale hakufanikiwa lakini juhudi zilifanyika. Na najua wako wengine wengi wanaweza kuja na mifano mingi ya kuonyesha jinsi gani nchi yetiu ndio ilikuwa muubiri na mtekelezaji wa dhana ya Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu. Tuliimba hizi nyimbo shule za msingi na kweli tulifanikiwa sana kujenga nchi moja yenye mshikamano usiojali dini, ukabila au rangi. Nafikiri hili tunahitaji kuliweka kama ndio msingi Mama kadri tunavyozidi kwenda mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania yetu. Leo Kenya wamegundua kuwa utengano ni udhaifu. Watanzania tufungue macho na masikio tunayaone na kuyasikia haya na bila kuyapuuzia, kwa sababu ukweli hata siku moja haupuuzwi kama una nia ya kweli ya kuboresha na kujifunza.

Baadhi ya walafi ccm wamefanya siasa kuwa ni uadui imefikia mahali sasa hata hatutibiani hatuendi kuwaangalia wagonjwa hatuzikani!kisa ni mwana chadema na sisi ni wana ccm tunamuogopa mwenyekigoda wetu
 
"Nikiwa rais watalimia meno"," atakayenipinga nitampoteza ndani ya dk.5". Mtu hunena yaliyoujaza moyo wake,roho iliyojaa visasi ikeshayo ikijiapiza kufanya uovu inaanzaje kuandaa makongamano ya upatanisho?

Hiiiiiiii!!! Yaya ghete.
"Nyoka akipita shambani kwako lazima umpige umuue hata ukimkosakosa ataenda kufia mbali" hii kauli sitajakaa niisahau maishani

Bujibuji Mshana Jr MSAGA SUMU Lizaboni
 
Kwani Kenyatta ana nini cha kupoteza sasa hivi? Hawa wote si walikuwepo 2007 na baadaye.. kwanini huu "umoja" wanaouonyesha sasa hivi hawakuoonesha wakati wa kabla ya uchaguzi? Of course, sasa hivi wote wana gain... na watu bila kufikiria wanawapa pongezi.. well.. they have nothing to lose now.
 
Jiwe lingeweza kuwa juu sana kama lingeacha shughuli za kidemokrasia za vyama vya siasa ziendelee kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa. Tatizo lake linataka liongee lenyewe tu na chama chake ndio maana linaitwa lidikteta uchwara.
Hata kina odinga wafuasi wao walimtukana sana kenyatta , sasahivi odinga na kenyatta wanakunywa chai pamoja wakifurahi, jifunzeni hapo kutoka kenya , matusi hayana faida yeyote , la muhimu kuchapa kazi kwa maslahi pana ya taifa la watanzania.
 
Hana lolote alishakuwa Rais na hagombei tena kwa mujibu wa katiba.Namuonea huruma Rutto atakavyoachwa kwenye mataa kama alivyoachwa Lowassa.
 
Nakala iwafikie wafuasi wa Lowasa aliyekutana Na Magufuli Na wale wapiga kura wa chadema kinondoni uchaguzi wa 2015 waliohangaika Na mbunge wa UKAWA Mtulia
Pia nakala iwafikie wote waliosusia mazishi ya mbunge mwenzao huko chigoma....
 
Back
Top Bottom