Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Hahaha mkuu chabuso , mawazo ya kiafrika yapoje? Mimi ni muafrika lazima niwe na mawazo ya kiafrika , ndio maana nimesema ni siasa tu alichokifanya uhuru , si cha ajabu hata kidogo ,angekifanya hicho wakati ana kesi , bila kuvuruga mashahidi kule hegue ndio ningemuona ni mfano wa kuigwa lakini sasa , kaona awamu yake imekwisha anaomba msamaha ni tendo lakawaida tu, ajiuzulu basi tujue kamaanisha .na ndio tendo la kishujaa.
Waafrika hisia zetu ndio zinazotuongoza sio uhalisia wa jambo...umetoa maamuzi yako kwa hisia zako,hujaangalia manufaa(benefit) ya hili jambo kwa Kenya kiujumla,Bila shaka labda biashara zake zitafungua lakini vile vile biashara za wengine zitafunguka,kenya itanufaika..Mkuu
 
Mkuu chabuso kwa dhana hiyo ya kuongozwa na hisia , wewe pia ni muafrika halisi , nilipo sema siasa na biashara sikumaanisha biashara zake binafsi za kuuza maziwa , nilimaanisha biashara za kisiasa, kashamaliza muda wake afanyaje auze sasa , mbona mwanzo hakuomba msamaha ? Kapelekwa mpaka hegue kavuruga ushahidi , kapeleka wabunge kule kuimba usiku na mchana , hahaha , shughuli imekwisha anauza , hahaha , chadema wajifunze hapo .
 
Siasa za ukabila!
Tuache unafiki, wapi hakuna ukabila na inavyoonekana huko tuendako Tanzania itakuja kuipiku Kenya kwa ukabila kama hiki chama kikiendelea kutawala.!!

Uhuru Kenyatta, hawezwi kulinganishwa na "Mtawala" yeyote ktk ukanda huu kwani anaweza akaongoza nchi yoyote ya Ulaya.
 
Hakuna watu wepesi kurubuniwa Kama kundi kubwa la watanzania, nimeanza kuelewa ndo maana watu waliaminishwa jamaa fulani ni fisadi miaka kibao halafu ghafla akapitishwa kugombea watu wakashangilia na kudeki lami huku wakizungusha mikono.Kenyatta ameua Sana mpaka alipelekwa ICC,kafanya ufisadi kufuru kuanzia baba yake karibu moja ya tatu(1/3) ya ardhi ya Kenya inamilikiwa na ukoo wake, ni moja ya maraisi matajiri Afrika kutokana na kuwatia umaskini kuwapokonya ardhi wakenya, Leo akipatana na Odinga mnamuona shujaa?,nakubaliana na Mzee Mkapa waliokuwa wakizungusha mikono 2015 nni WAPUMBAVU na MALOFA.Hammjui Kenyatta vizuri, na vile vile hammjui Lowassa vizuri.
Hata hapa watu kibau waliuawa kwa sababu kama hizo unazofikiri eg akina Hanga,Kombe, Memba, Mc Ghee, Mwangosi, Mawazo, Daniel John, Mvungi, Saanane, Azory, yule mbunge wa Kilombero na Lissu, almanusra and the list goes on.

Labda tu nyani haoni kundule lkn hata hao waliotajwa hapo juu nao ni binadamu na walikuwa na haki ya kuishi kama wengine. So, hakuna wa kutupa jiwe la kwanza. Acheni unafiki.
 
Sasa

Sasa mbona mgombea wa upinzani wa upinzani na mjumbe wa kamati kuu CDM mh Edward Lowassa alipokwenda kumuona JPM ikulu mlimshambulia kwa kejeli?,huoni majina aliyowapa Mzee Mkapa ni sahihi?,hamjui mnasimamia nini?, Hamna msimamo wowote.
 
Watanzania acheni kujidanganya. Tunampenda Rais wetu na mambo mazuri anayofanya. Mengi.
Lakini je kwa ukweli bila unafiki kuna mtu anakubali mabaya yanayotokea kwa kuambiwa agizo kutoka juu?
Kuondoa kabusa uhuru wa watu mpaka magazeti siku hizi hayanunuliki, kuwafunga nusu ya wapinzani kwa makosa ambayo siyo ya kisheria, kufukuza wengine na kumwacha mwana, kubomoa nyumba sehemu na kuacha kwingine, kuruhusu vurugu wakati wa uchaguzi wowote, na.kadhalika.
Tutawaveza wakenya lakini nikiongozi gani hata moja Tz amesema nimekosa isipokuwa Nyerere?
 
Huku kwetu Mamvi alipoenda ikulu chama chake kikaanza kumzodoa.

Seif alipokataa mkono WA Shein akapongezwa kwamba siyo mnafiki.

Leo hii walewale ndiyo wanakuja kujibaraguza eti Kuna kitu cha kujifunza.
 
Ni kweli wamefanya vizuri lakini pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa siasa ni mchezo mchafu sana, wakenya wengi wamepoteza maisha kwa vuguvugu hizi, lakini leo kiurahisi tu watu wanashikana mikono eti wanasameheana, vipi kuhusu waliopoteza maisha? Ni siasa za maji taka hizo.
Kuendelea kutofautiana ama kujenga visasi wengi wangezidi kupoteza mausha.. mbinu moja ikishindwa unageukia nyingine wahenga walisema if u cant defeat them then join them
 
Hakuna watu wepesi kurubuniwa Kama kundi kubwa la watanzania, nimeanza kuelewa ndo maana watu waliaminishwa jamaa fulani ni fisadi miaka kibao halafu ghafla akapitishwa kugombea watu wakashangilia na kudeki lami huku wakizungusha mikono.Kenyatta ameua Sana mpaka alipelekwa ICC,kafanya ufisadi kufuru kuanzia baba yake karibu moja ya tatu(1/3) ya ardhi ya Kenya inamilikiwa na ukoo wake, ni moja ya maraisi matajiri Afrika kutokana na kuwatia umaskini kuwapokonya ardhi wakenya, Leo akipatana na Odinga mnamuona shujaa?,nakubaliana na Mzee Mkapa waliokuwa wakizungusha mikono 2015 nni WAPUMBAVU na MALOFA.Hammjui Kenyatta vizuri, na vile vile hammjui Lowassa vizuri.
Umeeleza vizuri kabisa , mwenyesikio haambiwi sikia
 
Sasa

Sasa mbona mgombea wa upinzani wa upinzani na mjumbe wa kamati kuu CDM mh Edward Lowassa alipokwenda kumuona JPM ikulu mlimshambulia kwa kejeli?,huoni majina aliyowapa Mzee Mkapa ni sahihi?,hamjui mnasimamia nini?, Hamna msimamo wowote.
Tungekuwa na "A really democratic state as well as the vibrant and functioning judiciary", Mkapa angekuwa jela, kwa maovu aliyofanya kama ya Kiwira, EPA, Meremeta nk.

Ashukuru mfumo aliyochangia kuutengeneza ambayo sera yake kuu ni kuukandamiza upinzani na watu wenye fikra huru ila hakuna marefu yasiyo na mwisho.
 
Sasa

Sasa mbona mgombea wa upinzani wa upinzani na mjumbe wa kamati kuu CDM mh Edward Lowassa alipokwenda kumuona JPM ikulu mlimshambulia kwa kejeli?,huoni majina aliyowapa Mzee Mkapa ni sahihi?,hamjui mnasimamia nini?, Hamna msimamo wowote.
umesema kweli kabisa,
wanaomba po sasahivi , hahaha,wanataka kuombwa msamaha , subirini atakapokuwa ngwe yake ya mwisho , chapa kazi magufuli
 
Ni kweli wamefanya vizuri lakini pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa siasa ni mchezo mchafu sana, wakenya wengi wamepoteza maisha kwa vuguvugu hizi, lakini leo kiurahisi tu watu wanashikana mikono eti wanasameheana, vipi kuhusu waliopoteza maisha? Ni siasa za maji taka hizo.
Yaliyopita si mdwele, tugange yajayo!
 
Tungekuwa na "A really democratic state as well as the vibrant and functioning judiciary", Mkapa angekuwa jela, kwa maovu aliyofanya kama ya Kiwira, EPA, Meremeta nk.

Ashukuru mfumo aliyochangia kutengeneza ambayo sera yaku kuu ni kuukandamiza upinzani na watu wenye fikra huru ila hakuna marefu yasiyo na mwisho.
Tanzania kuna wapinzani? Hawa wanaotukana kutwa kwenye mitandao ndio wapinzani? Magufuli anasafisha serikali hawataki , anahimiza uchapakazi na uanzishwaji wa viwanda , hawataki , wanataka nini? Hao ni wapiga deal tu hakuna wapinzani hapa, kumchukua Lowasa alietuhumiwa kua ni fisadi , na kumuosha na kumpa ugombea urais ambao ccm walimkataa ndio nini hiko? Wajinga ndio waliwao , hapo kuna wapiga deal tu hakuna upinzani hapo.
 
Back
Top Bottom