Hongera Kenya kwa mrejesho wa kazi za Infrastructure

Hongera Kenya kwa mrejesho wa kazi za Infrastructure

Inanambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
4,039
Reaction score
2,840
Leo asubuhi nimebahatika kuwatch Citizen TV
Nikakutana na Live Kipindi kutoka State House yao kinaitwa Infrastructure Summit. Nikavutiwa kukisikiliza. Waziri wao alikuwa anaongea kuhusu kazi aliyoifanya ya Infrastructure mbele ya wadau. Baadaye kila aliyekabidhiwa kazi ya kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilikishwa akaitwa mbele kujieleza na Moderator Jeff Koinage akawa anawahoji. Kila mmoja alieleza kafanya nini, kapata wapi fedha, amekamilisha kiasi gani, challenge ni zipo. Wadau wanauliza maswali wanatoa mapendekezo yao. Ikiwa private sector nazo zihusishwe, waondoeje traffic jam n.k. Jubilee wametekelezaje ahadi zake wameshindwa wapi yaani hadi raha. Mjadala wote ni English wanaflow hadi raha
naona wengi ni Engineers. My take: Naomba Watz tuige mfano huo wa kukutana kutoa mrejesho wa Majukumu tuliyopewa.
 
Kwa tz thubutu
Yaani wanajadili vizuri Mara Thika highway, Mombasa-Nairobi, Uwanja Wa Ndege Wa JK, Barabara za city centre Na mengineyo. Huyu anasema pale improve hivi, shirikisha hawa. hapo kuna wataalamu na Contractors
Wanasema in future kusiwe Na lawama kwa kushindwa kushirikisha Local Capacity, allocation of maintaince of roads instead of concentrating on new roads
 
N
Nawapongeza wasanii wetu wa bongo flava na movie kwakuiga hcho kipengele cha ku flow kingereza mpaka sasa hivi
Ni kama wako ofisini wanajadili kazi zao. Wanatumia flow ya English kwa kuwa kuna wadau hadi Matatu owners association. Hao wasanii wetu wameamua kujiongeza kilugha wawe Wa kimataifa.
 
N

Ni kama wako ofisini wanajadili kazi zao. Wanatumia flow ya English kwa kuwa kuna wadau hadi Matatu owners association. Hao wasanii wetu wameamua kujiongeza kilugha wawe Wa kimataifa.
Hii ndio maana ya demokrasia : uwajibikaji
 
Hii ndio maana ya demokrasia : uwajibikaji
Safi sana. Sasa wako na presentation wanachukua hotuba ya Rais Kenyatta aliposema atajenga barabara Fulani. Barabara inaoneshwa ilivyoanza kujengwa hadi kukamilika. Naomba muwatch Citizen TV SAA hii mtaona.
 
Hii ndio maana ya demokrasia : uwajibikaji
Kwa uwajibikaji huu na demokrasia hii naona hakuna atayethubutu kula rushwa, kuzembea kazi. Mrejesho kama huu hata Bunge halioni ndani.
 
Nakuambia hata mfanyi kazi yeyote in public and private sectors anafanyiwa appraisal maze
 
Duh, nimekua busy na michakato ila natumai wataweka kwenye archives tufuate huko baadaye.
 
Hongera wakenya, kwa live presentation ya infrastructure zenu,lakini kiingereza sijui kinahusiana VP,kwa sababu, ni kama lugha zingine tu e.g italiano,French, Spanish etc. acheni ushamba,lugha sio kipimo cha werevu wa mtu.ndio maana niliona mtu mmoja akisema Tz haijulikani na CNN.
 
Passer by
Wacha ushamba jifunze Kingereza hutapitwa na mambo mengi ya kisasa. Huu ni uzembe wenu kwamba mkishindwa kujifunza Kingereza mnaanza kuponda kila anayekiongea kwa ufasaha.
Hii mada imeletwa na Mtanzania na yeye ndiye ametaja mambo ya vile anapendezwa na jinsi jamaa wanatumia Kingereza, sasa mbona utuite Wakenya washamba.

Watanzania lazima mjifunze Kingereza, muache uzembe. Kila nikihusika kwenye mradi Bongo unaohusu wataalam kutokea nje, huwa mnatia aibu sana kwenye vikao. Mnang'ang'ana na Kingereza hadi hamueleweki, inabidi niingilie kati kutatua ugomvi. Unakuta Mtanzania amepandwa na hasira kwa jambo fulani, kumbe tatizo ni kwamba hakuelewa kauli za mgeni na akatafsiri kivyake. Inabidi niingilie kati kumwelewesha kwamba anachokisema ndio hicho hicho mgeni alichokua anakisema hivyo wote wanaongea kitu kimoja na wana msimamo unaowiana, tatizo lugha inagongana.

Kiswahili ni lugha muhimu sana kwenye shughuli zetu za kila siku baina yetu, lakini Kingereza kina umuhimu mkubwa sana maana kinaunganisha dunia.

Leo hii kuna mradi naufanya ambao unahusisha wataalam kutokea Mauritius, Botswana, Tanzania, Nigeria na mimi Mkenya, sote tumeunganishwa na lugha moja ya Kingereza na mambo yanakwenda. Hivyo Kingereza hakina mbadala kwa dunia ya leo, aidha ujifunze au ubaki nyuma ukiwaogopa ogopa wageni. Hutaki kuwalaki au hutaki kusafiri na kwenda kwenye vikao vya kimataifa.
 
Nakuambia hata mfanyi kazi yeyote in public and private anafinyiwa appraisal maze
Appraisal niliisikia tu Darasani kwenye Module ya Performance Appraisal. Kwenye practice sijapata kuona japo kazini najaza form yake Mara 2 kwa mwaka. Inaitwa OPRAS. Nazidi kuwapongeza kama pia mna Public appraisal.
 
Duh, nimekua busy na michakato ila natumai wataweka kwenye archives tufuate huko baadaye.
enda twitter uulize citizen tv ama ktn kama wako na full complete proceedings ya hiyo confrence waweke youtube kwasababu ni muhimu kila mkenya ajue pesa zao zinatumika kwa project ghani, si kila mtu ataweza angalia live kwani watu wengi walikua kazini
 
N

Ni kama wako ofisini wanajadili kazi zao. Wanatumia flow ya English kwa kuwa kuna wadau hadi Matatu owners association. Hao wasanii wetu wameamua kujiongeza kilugha wawe Wa kimataifa.

ni vizuri kupongeza katika kila jambo ambalo mwenzio amepiga hatua ( nakuunga mkono kwa asilmia zote) ila unaweza kunisahihisha kwa hili nitakalokueleza...

1. kupitia comments zako nimejua kuwa kitu kilichokuvutia ni matumizi ya lugha ya kiingereza zaidi ( inaonekana ni lugha unayoihusudu zaidi ).

2. Ni dhahiri kuwa huzitilii maanani sana habari za ndani ya nchi yako na pia si mtu wa kutembelea maeneo tofauti ya nchi yako katika makuzi yako kwa kuwa comments zako zimeegemea katika uelewa hafifu wa maendeleo ya nchi yako.....

yote kwa yote ,pongezi ziwaendee wakenya maana wapo vizuri katika urban planning na pengine ni zaidi yetu
 
Hongera wakenya, kwa live presentation ya infrastructure zenu,lakini kiingereza sijui kinahusiana VP,kwa sababu, ni kama lugha zingine tu e.g italiano,French, Spanish etc. acheni ushamba,lugha sio kipimo cha werevu wa mtu.ndio maana niliona mtu mmoja akisema Tz haijulikani na CNN.
Kwani alisema uongo?
 
Twitter5c8878d.jpg
Twitter511ae2e.jpg
Twittere3d78a5.jpg
 
Back
Top Bottom