Hongera kwa gazeti la Mwananchi, mmethubutu

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Ni gazeti pekee angalau lilodhubutu kuzungumzia habari za Tundu Lisu mgombea halali wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Azam tv habari pia tuliona habari yenu kumhusu Lissu, inatosha kusema angalau mmethubutu.

 
Hivi hawa viingozi wetu hawaoni aibu kulazimisha mapenzi ya mtu kwa chama fulani au kwa mgombea?

Hata wakizuia habari zinazomhusu Lissu zisitangazwe au kuandukwa gazetini, bado wenye mapenzi na Chadema ama Lissu wataendelea kumuunga mkono. Wakae wakilijua hili.
 
Uko sahihi mno. Itikadi ya Mtu ni kama spiritual beliefs. Hailazimishwi kwa kusikia redioni.
 
Ili kujua na akina nani walimpiga Lissu risasi, inabidi kufanya uchunguzi. Lakini, kujua ni nani aliyewatuma hao waliompiga risasi hapahitajiki uchunguzi. Linahitajika jambo moja tu nalo ni akili timamu (sanity). Yaani usiwe taahira.
 
na hivi mmewasifia hapa inaweza kuwa fontfed ya mwisho
 
Huenda wameanza kugundua hatari ya kumlamba miguu Bwana yule.

Hata hivyo,huenda gazeti likaadhibiwa kwa kuandika habari hii bila ku-balance story kwa kuwahoji watu wasiojulikana!
Hujamsikia IGP? Inaonekana wasio julikana ni Lissu maana polisi wana mtafuta. Watampata akisha pitishwa kugombea Urais maana atakuwa na ulinzi wa polisi.

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Gazeti bila habari za chadema haliuziki.. wanajua siku ambazo chadema ipo kwenye front page biashara inakua nzuri..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…