Hongera kwa gazeti la Mwananchi, mmethubutu

Hakuna chombo Cha habari chochote ambacho kimzuiwa kuandika habari za huyo Lissu, issue inakuja katika hotuba zake anaweza kuhutubia zaidi ya saa usiipate at habari moja zaidi pumba tu! Sa utaandika? Bora uache tu
 
Mwenyewe nimeona fairness kwa Mwananchi. Ukweli wamefanya jambo zuri sana na leo gazeti lao lazima linunuliwe nakala zote. Hadi nimetamani wapandishe na bei kabisa!
 
Umeandika falsafa muhimu sana. Ubarikiwe
 
Ni ngumu sana dreva kuendesha Basi la abiria wakati hajui usukani unakaa wapi ndani ya Basi.
 
Kina lichunga ng'ombe litakuwa limekunja ndita sana baada ya kuiona habari ya Lissu front page na mwaka huu hizo ndita linazokunja litajikuta linaziweka mfukoni
 
Watawala wanataka tuwe na magazeti mawili tu kama ilivyokuwa baada ya uhuru 1961.

Tuwe na gazeti la Uhuru na Mzalendo... Television tubaki na moja tu TBC.

Ukisikia maendeleo ya kwenda kinyume nyuma ndiyo haya!!

Moja ya hatua kubwa sana ya kimaendeleo ni uwezo wa wananchi kupashana habari...ziwe za kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata za michezo... watawala hawalitaki jambo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…