Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
Japo utambulisho bado haujakamilika, ila nimechagua kuja kutoa siri. Nimechagua kuja kutoa pongezi.
Katika nyuzi zilizopita nilitoa angalizo kuwa huwezi hitaji aina fulani ya mpira, then unaenda sokoni kuchukua mchezaji au kocha ambaye hana sifa za aina au falsafa ya kile unachokitaka. Nikatolea mfano yaani unataka mpira biriani, Jogo bonito , Beautiful/Sexy football, alafu unaenda kumchukua José Mourinho then ukategemea Sexy Football.
Hivyo hivyo upande wa wachezaji: Timu inahitaji wachezaji runners kama AS Vita/RS Berkane then unaenda kuchukua the like of Chama/Rally Bwalya then unategemea atakimbia kama the like of Kisinda e.t.c ni ngumu kufanikiwa.
Haimanishi hao wachezaji ni wabaya hapana, bali strength zao ni tofauti na kile unachokihitaji, ambacho ni mbio, vijana wa mjini wanasema mabioo. Nenda kaangalie AS Vita sasa sokoni kila mchezaji anaesajiliwa ni mbio, kama ni timu ya marathon, haha, ila tayari umepata point yangu.
Turudi kwenye Simba, katika misimu miwili iliyopita Simba ilikua inalia kuwa falsafa ya mpira wao imepotea, lakini angalia Makocha waliokuwa wanaletwa Zolan, Mr. Objective, hata Benchikha mwenyewe. Ikafika kilio ikawa timu yetu haina kasi, lakini kwenye Kikosi ambaye wenye uwezo wa kutoa hiyo energy ni Kibu, Mzamiru hadi pale tulipo waona wale watoto kama Chasambi n.k., Wengine kuhitaji kuwaona wanatoa kasi basi ilikuwa ni kuwa punguzia umri wa kuishi kama Chama, Ngoma, Sarr, Luis, bora hata Saidi etc. Mchezaji hawezi toa kile ambacho hana.
Ila sasa leo, angalia nature na sifa ya wachezaji wanaosajiliwa? Ukitoa kwa wale ambao tayari wametambulishwa kama Vile Mukwala, Mutale wote ni sharp, fast, utulivu wa hali ya juu, na skills zote kwenye nafasi zao, wana energy kubwa wakiwa na mpira pia wasipokuwa na mpira. Energy, njaa ya mafanikio, Skills na Umri. Hivi ndivyo vimeweka kwenye ramani ya kuijenga Simba mpya. Ndio maana hata upande wa Kocha japo sikubaliani nao, ila naelewa kwanini wamefuata kocha msaidizi wa Raja Casablaca. Lengo ni kutengeneza Raja Casablanca ya chini ya Jangwa la Sahara.
Kwa wale ambao mmebahatika kuona hata wale wachezaji ambao bado hawajatangazwa basi utakubaliana na lengo lao la kuitengeneza Simba katika falsafa ya uchezaji wa Raja Casablaca. Naamini hata kama itachukua muda mrefu lakini hii project itaenda kufanikiwa maana kile wanachokizungumza kinaendana na utendaji.
Hivyo basi natoa poangezi kwa wale wote wanaohusika katika ujenzi wa Simba mpya. Hata kama hii project haitafanikiwa katika msimu ujao, maana project kubwa kama hii huwezi ijenga usiku mmoja. Basi katika Msimu 25/26 hii Simba itakua bora sana.