Hongera kwako Baba Askofu Mkuu Jude Thaddeus Ruwa'ichi kwa kuteuliwa na Papa Leo XIV

Hongera kwako Baba Askofu Mkuu Jude Thaddeus Ruwa'ichi kwa kuteuliwa na Papa Leo XIV

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
2,919
Reaction score
5,558
Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa wizara (Dicastery) ya Mashirika ya Kitawa ya Maisha ya Wakfu na Mashirika ya Maisha ya Kitume Ulimwenguni kote ofisi zikiwa makao makuu Vatican.

Ni miongoni mwa wa Afrika watano walioteuliwa katika nafasi hiyo muhimu wengine ni Askofu Mkuu kutoka Morocco, Askofu Mkuu kutoka Ethiopia, Askofu kutoka Afrika ya Kusini na Padre kutoka Zambia.

Askofu Mkuu bado ataendelea na utume wake kama Askofu Mkuu wa Dar es Salaam ila safari za Vatican zitakuwa nyingi sana.

Tunakutakia kila jema na utume mwema kwako Baba.

===
ASKOFU MKUU RUWA`ICHI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA DIKASTERI YA MAISHA YA WAKFU NA JUMUIYA ZA MAISHA YA KITUME

- Jumanne Juni 24, 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alimteua Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa`ichi OFMCap, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Wajumbe wa Dikasteri ya maisha ya wakfu na Jumuiya za maisha ya Kitume Vatican.

- Dikasteri hii muhimu ina majukumu ya Kusimamia, kuratibu na kuongoza maisha ya watawa (wanamashirika), yaani:
- Mashirika ya Kike na Kiume ya maisha ya wakfu
- Mashirika ya Kitume
- Kuridhia kanuni, sheria, na mabadiliko ya mashirika hayo.
- Kuidhinisha uanzishwaji wa mashirika mapya ya wakfu, na kuyaongoza katika hatua za mwanzo.

- Baada ya uteuzi huu Askofu Mkuu Ruwa`ichi bado ataendelea na utume wake wa kuendelea kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es salaam.

Source: Radio Maria Tanzania
 

Attachments

  • 1000048211.jpg
    1000048211.jpg
    66.4 KB · Views: 39
Aongezewe Auxiliary Bishop mwingine sasa, baada ya Ask. Musomba kwenda Jimbo la Bagamoyo
Yap lazima ataongezewa watakuwa kwenye mchakato. Jimbo la Dar kubwa sana na majukumu hayo aliyopata uhitaji upo
 
Back
Top Bottom