Hongera Lema, ukweli hata kama mchungu shuruti usemwe

Hongera Lema, ukweli hata kama mchungu shuruti usemwe

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu:

IMG_20221212_082942_989.jpg


Mkwamo wetu uko hapa. Uhai wetu utarejea kwa kujikwamua kutoka hapa.

Ukweli huu ni mwiba mchungu mno kwa ule upande mwingine uliojaa ulaghai na ubinafsi uliopitiliza.
 
Nimemsoma Mbowe alipokuwa akiongea na diaspora, wakati akilalamika watu kusema amelamba asali akidai kauli hiyo inamuumiza, amesema amekuwepo kwenye siasa miaka 30, hivyo kwake hawezi kudanganywa kwa chochote.

Amesema wakati mwingine anaamua kukaa kimya ili awaache wengine nao waongee, kina Lema na Lissu. Hapo alichosema Lema ni sahihi kabisa, namuunga mkono.

Wanachokifanya CCM kwenye vikao vya maridhiano ni utapeli, haiwezekani Kinana, Chongolo, na Shaka, wanazunguka nchi nzima kufanya mikutano ya kisiasa, lakini kwa wapinzani bado wanatakiwa wakakae kwenye vikao vya maridhiano, huo ni utapeli.

Mbowe amedai watu wana uchungu kwa yale waliyofanyiwa, wengine walipigwa risasi, wapo waliokimbia nchi kwa kuhofia usalama wao, hivyo kuna wakati anaamua kukaa kimya ili hao nao watoe yao ya moyoni, asiwe yeye pekee ndie mzungumzaji kila wakati.
 
Wajinga hawaelewi kuwa katiba na sheria vinaruhusu mikutano ya siasa, hivyo ni swala la kufuata katiba na kutii sheria tu na si kukaa vikao kujadili jambo lililoruhusiwa kisheria na kikatiba na hii ndio hoja ya Lema.

Niliwahi sema humu na leo narudiia, "watu wenye akili za kawaida, sometimes ni vigumu kuwaelewa watu wenye akili nyingi au watu wenye akili za ziada ".
 
Mbowe amesema yuko tayari kumpigia Magoti mwenyekiti wa CCM

Lema anamuuliza Mbowe mnajadili nini kwa mambo yanayohitaji utii wa sheria kwa katiba hii hii ya 1977?

Usiwawekee watu maneno mdomoni:

1. Uko wapi ushahidi wa kuwa Mbowe kasema yuko tayari kumpigia magoti mwenyekiti wa CCM magoti?

Zingatia imendikwa "usiwe na miungu mingine ila Mimi."

2. Uko wapi ushahidi wa kuwa Lema anamwuliza Mbowe kinachojadiliwa?

Zingatia Lema haulizi bali kama nabii ana nena!
 
Ujinga wa watanzania ndio unaifanya katiba isiwe na maana yoyote katika kuamua maisha yetu ya kila siku!!. Watanzania wengi tungekuwa na elimu sahihi ya uraia na kuzitambua haki zetu basi viongozi hawa wasingekuwa wanatafuta malidhiano kwenye vitu vilivyowazi kikatiba!!
 
Mbowe anaongezewa points.

NInakazia:

"Ukweli huu ni mwiba mchungu mno kwa ule upande mwingine uliojaa ulaghai na ubinafsi uliopitiliza."

Vipi ndugu wewe ni mmoja wao katika upande huu?
Upande uliojaa ulaghai ni ule wa Chadema kwenye Maridhiano kwa sababu Mbowe amesema hawezi kuwaambia wanachama wake kinachojadiliwa

Wakati Mwenyekiti wa CCM mh Samia ameueleza Mkutano mkuu wa Chana chake kuwa wao ndio Waamuzi kwenye Maridhiano kwa sababu ni Chana Tawala kilichopewa ridhaa ya kuongoza na Wananchi
 
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu:

View attachment 2443641

Mkwamo wetu uko hapa. Uhai wetu utarejea kwa kujikwamua kutoka hapa.

Ukweli huu ni mwiba mchungu mno kwa ule upande mwingine uliojaa ulaghai na ubinafsi uliopitiliza.
Mkimaliza kuparuana mtakuta CCM inaendelea kula maisha huko Ikulu 🏃🏃.

Asali tamu Sana ,safi Sana Mbowe
 
Usiwawekee watu maneno mdomoni:

1. Uko wapi ushahidi wa kuwa Mbowe kasema yuko tayari kumpigia magoti mwenyekiti wa CCM magoti?

Zingatia imendikwa "usiwe na miungu mingine ila Mimi."

2. Uko wapi ushahidi wa kuwa Lema anamwuliza Mbowe kinachojadiliwa?

Zingatia Lema haulizi bali kama nabii ana nena!
Imekwisha Hiyo!
 
Nimemsoma Mbowe alipokuwa akiongea na diaspora, wakati akilalamika watu kusema amelamba asali akidai kauli hiyo inamuumiza, amesema amekuwepo kwenye siasa miaka 30, hivyo kwake hawezi kudanganywa kwa chochote...
Mambo bado magumu.....siasa bhana.Yaan wapo tayari kuumiza tuliochini kwa manufaa yao
 
Kutoa ushauri mbadala sio kugeukwa, ndio maana nyie CCM kina, Ndugai, Bashiru wakitoa ushauri mnawashambulia mnaona kama wanampinga mama kumbe ndio uhai wa chama na serikali yenu.
Wewe umemueelewa Godbless Lema!
 
Back
Top Bottom