Kama mzazi na mpenda haki, nmefurahishwa na kuridhika na maamuzi ya kutupa rufaa ya wanamuziki wa Kongo(Nguza na mwanae). Kwakweli naunga mkono hukumu! Takribani juma zima vyombo vya habari karibu vyote vimekuwa vikijaribu kuwasafisha watuhumiwa kwamba walisíngiziwa, eti hawana kosa. Bahati mbaya hakuna miongoni mwetu anaefuatilia majaliwa ya mabinti zetu walioachiwa majeraha watakayoishi nayo maisha yao yote. Ni jambo la kumshujuru Mungu mabinti zetu hawakuambukizwa ukimwi. Nijambo la kusikitisha,kutia aibu,kukatisha tamaa kuona watanzania wenzangu kuthamini umaarufu wa watuhumiwa kuliko ubinadamu. Hivi kweli sauti nyororo za Babusea na papikocha zilipwe kwa unyama kwa mabinti zetu tena wadogo hivi? Je starehe ni bora kuliko malezi na ulinzi na haki ya watoto wetu? Kama tunasema wameonewa mbona hakuna hata mmoja wetu mwenye ushahidi dhahiri aliekuja kudhibitisha? Badala ya kunun'gunika kwa ushabiki nngewashauri wanahabari na watanzania wenzangu mtafute nakala ya hukumu then mueleze umma unyama wa hawa hayawani waliotumia umaarufu wao kudhalilisha watoto na taifa letu. Kwa mzazi yeyote, unyanyasaji huu hauvumiliki hata kidogogo.