Hongera Mpina, hoja yako imeeleweka vyema kwa Wananchi Wazalendo

Hongera Mpina, hoja yako imeeleweka vyema kwa Wananchi Wazalendo

uzushi, uongo, kiburi na jeuri inarekebishwa kwa kanuni tu. kawa mdogo kama piritoni..
kutengwa na kukataliwa na kila mtu kwenye jamii fulani panaumiza sana aise [emoji205]

Kukataliwa na kikundi kidoko cha mafisadi hakuwezi kumwumiza mtu anayepigania haki.

Mpina anafurahia uungwaji mkono wa watu wema wenye akili timamu, watu wanaojitambua na siyo machawa wa mafisadi.
 
Kukataliwa na kikundi kidoko cha mafisadi hakuwezi kumwumiza mtu anayepigania haki.

Mpina anafurahia uungwaji mkono wa watu wema wenye akili timamu, watu wanaojitambua na siyo machawa wa mafisadi.
saivi uskute anaongea pekeyake tu kwa majuto 🤣

nyie mambo haya saa zingine ni kujitakia tu 🐒
 
saivi uskute anaongea pekeyake tu kwa majuto [emoji1787]

nyie mambo haya saa zingine ni kujitakia tu [emoji205]

Sitarajii Mpina eti ajutie huo uhayawani wa wabunge wenzake na huyo spika, kwa sababu hili genge la mafisadi, wametenda kama ilivyotarajiwa, na pengine hata pungufu ya Mpina alivyotegemea.

Mpina alijua kabisa kuwa hawa mafisadi ni syndicate inayojumuisha Bashe na baadhi ya wabunge wala rushwa wakubwa, kama Musukuma, na lazima wamejipanga kueteteana, sawa na walivyofanya kwenye kuuza mamlaka ya nchi kwenye masuala ya bandari, ndiyo maana Mpina aliamua kuweka wazi vielelezo vyote vya uharamia wa Bashe na genge lake, kwa umma. Na kwenye hilo alifanya vema, na amefanikiwa sana.

Suala la ufisadi wa sukari, limetoa ujumbe kwa mbunge yeyote mwenye dhamira njema ya kupinga ufisadi, ni vyema taarifa hiyo kuitoa kwa umma. Bungeni aitamke ili tu kuwaona wabunge majizi yaliyomo kwenye syndicate.
 
Mpina amefanya homework yake vizuri

Hakika. Ameifanya kikamilifu sana. Ndiyo maana wabunge wote waliokuwa wakitetea ufisadi wa Bashe, hakuna hata mmoja aliyeweza kupinga hoja ya Mpina kwa vielelezo. Wala hakuna hata mmoja aliyeweza kutamka kuwa vielelezo vya Mpina vilikuwa na ubatili. Wote waliendelea kupiga tu kelele kama mahayawani lakini bila ya kuwa na content.
 
Hakika. Ameifanya kikamilifu sana. Ndiyo maana wabunge wote waliokuwa wakitetea ufisadi wa Bashe, hakuna hata mmoja aliyeweza kuoinga hoja ya Mpina kwa vielelezo. Wala hakuna hata mmoja aliyeweza kutamka kuwa vielelezo vya Mpina vilikuwa na ubatili. Wote waliendelea kuoiga tu kelele kama mahayawani.
Bashe katangulizwa biashara ni ya mapacha wanne mkuu(JK, Rostam, Makamba na Abdul) ndiyo maana umemuona yule Spika hewa alivyokuwa mkali kama pilipili nyuma ake kuna vigogo hatari
 
Yeyote anayeamini matokeo ya kamati za lile bunge la kina Musukuma hana akili.
 
Hao vikaragosi wameona wamemkomesha sana mpina ila wakae wakijua wamemjengea heshima kubwa sana mtaaani tumeshajua ni nini bungeni kinafanyika madudu yote yanayofanyika wasimamizi ni bunge
 
Kilichotokea kwa Mpina Bungeni, ni kile kilichotarajiwa. Na wala hakuna anayeyashangaa maamuzi ya Bunge, zao la uovu wa 2020.

Bunge ambalo nalo ni matunda uovu na uchafu wa mwaka 2020, limeendelea kudumu katika kanuni ya upatikanaji wake. Ni Bunge la waovu:

1) Mahakama kuu ilitoa hukumu kuwa wabunge wanaoitwa wa kupita bila kupingwa, ni wabunge batili. Na hao ndio waliojaa humo Bungeni.

2) Hili Bunge ndiyo lililoidhinisha ile IGA ya hovyo kabisa iliyopokonya mamlaka ya nchi juu ya rasilimali zake. Kama nchi tunazuiwa na IGA kumtafuta mwekezaji mwingine kwenye masuala ya bandari iwe kwenye mito, maziwa au bahari, mpaka tumtaarifu DPW, na yeye aridhie. Hili ni bunge lililopofushwa na malipo ya DP World. Mbunge aliyekuwa nje ya inner circle anasema walipelekwa Dubai, na wakiwa huko walikuwa wakipewa pesa na DPW.

3) Hata kwenye mjadala wa leo, wabunge hao walikuwa wanapiga kelele badala ya kujibu hoja za Mpina. Wote kelele zao zimebakia kwenye kusema Mpina amedharau Bunge, amemdharau Speaker na Serikali, lakini hawakuijibu hata hoja moja ya Mpina.

4) Hili ndiyo bunge ambalo halijawahi kuchukua hatua zozote dhidi ya ufisadi unaoripotiwa na CAG kila mwaka.

Kwani ni nini cha kushangaza? Hivi kweli unatarajia mwovu aupige vita uovu? Tumeona mshikamano wa waovu. Laiti watu wema nasi tungekuwa na mshikamano kama walio nao waovu, nchi hii tungeweza kuikomboa kutoka kwenye mikono michafu.

KWA MPINA
Usisikitike wala kukata tamaa, bali ufarijike kwa kuwa umeunena ukweli utakaobakia kwenye kumbukumbu, na wananchi wote wenye uelewa na wanaolipenda Taifa lao wamekuelewa.

Haikutarajiwa watu waliofanya ufisadi kupitia sukari eti wangekuja hadharani na kusema kuwa kweli sisi ni mafisadi, kupitia huu uchafu wa mikataba ya sukari, tumetengeneza mapato yasiyo halali bilioni 36.

Kilichofanyika kwa sasa ni kuthibitisha tu kuwa uchafu uliofanyika kwenye mikataba ya kuleta sukari, haukuwa wa Bashe pekee, yumkini Bashe alikuwa mtekelezaji tu.

Huu ni uchafu sawa na ule wa EPA, Escrow na Kagoda, na ule ufisadi unaofanywa kila mwaka na kuthibitishwa na reports za CAG. Waovu wapo kwaajili ya kulinda uovu. Ni jukumu la watu wema kulikomboa Taifa lao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA LAANA IKAWE JUU YA WEVI WOTE WANAOJINEEMESHA KWA MAPATO BATILI.

PIA SOMA
- News Alert: - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Ila Bunge la Mwendazake hapana.
Tulisema lakini.
 
Hao vikaragosi wameona wamemkomesha sana mpina ila wakae wakijua wamemjengea heshima kubwa sana mtaaani tumeshajua ni nini bungeni kinafanyika madudu yote yanayofanyika wasimamizi ni bunge
Cha ajabu na Msukuma yumo.na Gwajima wanamkaanga mwenzao.
 
Ni vyema tukajua hivyo vikao kumi na tano ambavyo Mpina amesimamishwa angepata posho ya sh ngapi kama vipi wananchi wapenda haki tumchangie
 
Sitarajii Mpina eti ajutie huo uhayawani wa wabunge wenzake na huyo spika, kwa sababu hili genge la mafisadi, wametenda kama ilivyotarajiwa, na pengine hata pungufu ya Mpina alivyotegemea.

Mpina alijua kabisa kuwa hawa mafisadi ni syndicate inayojumuisha Bashe na baadhi ya wabunge wala rushwa wakubwa, kama Musukuma, na lazima wamejipanga kueteteana, sawa na walivyofanya kwenye kuuza mamlaka ya nchi kwenye masuala ya bandari, ndiyo maana Mpina aliamua kuweka wazi vielelezo vyote vya uharamia wa Bashe na genge lake, kwa umma. Na kwenye hilo alifanya vema, na amefanikiwa sana.

Suala la ufisadi wa sukari, limetoa ujumbe kwa mbunge yeyote mwenye dhamira njema ya kupinga ufisadi, ni vyema taarifa hiyo kuitoa kwa umma. Bungeni aitamke ili tu kuwaona wabunge majizi yaliyomo kwenye syndicate.
wakati wewe hutegemei,
mwenzako anawaza kama bunge na wabunge wake wamenizodoa namna ile mpaka madudu ya alipokua waziri wa uvuvi kwamba nilitesa watu, Je CCM itamuacha kweli? na adhabu yake si itakua mara 100 zaidi ya hii ya bunge iliyomchukulia huku moyo ukimuuma sana?🤣

uongo na usushi sio kitu kizuri ndugu zangu 🐒
 
uzushi, uongo, kiburi na jeuri inarekebishwa kwa kanuni tu. kawa mdogo kama piritoni.

kutengwa na kukataliwa na kila mtu kwenye jamii fulani panaumiza sana aise 🐒
Mpina ni Nuru waliobaki ni Giza.
Hivi vitu haviwezi Kaa pamoja
 
Ni vyema tukajua hivyo vikao kumi na tano ambavyo Mpina amesimamishwa angepata posho ya sh ngapi kama vipi wananchi wapenda haki tumchangie
hiyo itaitwa waacheni wafu wazikane wenyewe, wazushi na waongo family 🐒
 
Back
Top Bottom