Hongera Mwamba Freeman Mbowe Mwasisi wa Maridhiano

Hongera Mwamba Freeman Mbowe Mwasisi wa Maridhiano

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Wengi walikubeza wakasema umelamba asali, lkn juhudi na uvumilivu wako leo umezaa matunda. Hongera sana, pongezi kwa viongozi wote wa Chadema na vyama vingine, ushindi wa leo (kuondolewa kwa zuio la mikutano) ni ushindi wa wa Tanzania wote.

4E05228C-713F-4178-AD84-4C529B9C9608.jpeg
 
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..

Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..
 
Mbowe kusema kweli ni mtu wa kipekee kabisa;

Ameumizwa sana lakini hajawahi kuhimiza ubaya.

Amesingiziwa mengi lakini yeye hakuwahi kumsingizia yoyote.

Huyu ni mzalendo na mpenda nchi yake kuwa na ustawi kwa faida ya wote na sio wachache.

Bravo Kamanda Mbowe
 
Hakuna katiba mpya
It’s a process not an event bro.

“Katiba ni ya Watanzania siyo ya vyama vya siasa. Nataka kuwapa faraja kwamba mda si mrefu tutaanza.

Kamati itakayoundwa kwa ajili ya Katiba itaundwa na watu wa aina mbalimbali, itafanya kazi zake kwa maelekezo tutakayowapa, tutawapangia vizuri lakini siyo ile ya vuguvugu”. Rais SSH.
 
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..

Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..
Mkuu umenena vyema, tuwe na subira tuone huu mwafaka unafikia wapi, ila ccm wanatakiwa kufahamu kuwa hawana hati miliki ya nchi hii.
 
Hapa ndipo hoja kuu ilipo
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..

Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..
 
Nakataa kuwa mjinga.. muda utaongea. Tukutane hapahapa..
 
Mabadiliko au Uhuru wa kweli auletwi kwa njia ya kubembelezana kama alicho fanya Nyerere na sasa anacho fanya Samia hakuna kipya Tanzania tutapata tukiendeleza mtindo huu wa kunyenyekea na kubembeleza watawala .
 
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..
Na gharama yake ni hii: Kutukanwa, kubezwa na kudharauliwa na ndugu zako mwenyewe...
kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..
Kwa mfumo wa utawala wa kikatiba na kisheria wa nchi yetu, hili linawezekana na ndiyo maana hata mwanzo (2015 - 2022) liliwezekana na kufanywa na Magufuli na Samia kuliendeleza mpaka dakika chache zilizopita....
Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..
Usipobembeleza katika mazingira haya ya kikatiba na kisheria unadhani kuna njia nyingine? Ipi? Mapambano?

Ukitumia njia ya mapambano utakuwa umekosa BUSARA na HEKIMA maana wewe na wenzako mtakufa tu na mnaopigana nao wataendelea kuishi.!!

Tazama Konyi wa Uganda na waasi wenzake dhidi ya serikali ya Uganda. Je, wamefanikiwa kuiangusha serikali ya Museveni..? Nenda Kongo DRC nk nk..

Kina Mbowe na wenzake wako kwenye njia sahihi kushughulika na utawala huu wa kimla chini ya CCM Kwa katiba ya JMT ya 1977...

Ni njia ya mwendo wa taratibu sana lakini ni salama na effective kuliko wengi wanavyodhani...

Tukumbuke mabadiliko yoyote ya kweli katika nchi yoyote ni mchakato unaotumia combination ya njia nyingi kwa kuipima Kila moja..

Hii ni hatua ya kwanza. Imefanikiwa hata kama Kuna wasiwasi huo uliouonesha hapo juu. Lakini at least kwa sasa kuna hatua iliyofanikiwa...

Next ni kushughulika na msingi wa utawala huu mbovu na wa kimla, yaani KATIBA na SHERIA mbalimbali za kukandamiza demokrasia na uhuru wa watu..

Tutafika tu maana hakuna lisilo la mwisho. Muhimu ni uvumilivu na kuchukuliana. Hata kama mabadiliko haya hatutayafaidi sisi, watoto na wajukuu wetu watayafurahia na kuikuta historia ya wapambanaji Hawa...
 
Kimsingi, hamna jipya kisiasa kwani tumerudi mwaka 2014 enzi za JK. Kipindi kile mikutano ya hadhara ilifanyika na mchakato wa katiba mpya na Tume Huru ilikua inaendelea.

Alichofanya Mama ni kuturudisha enzi hizo. Tuombee ghliba na ubabe viwekwe pembeni. Busara itumike ili kusonga mbele
 
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..

Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..

Kumbuka Mbowe alikamtwa na kusekwa ndani baada ya kutangaza kufanya mikutano ya kudai katiba mpya nchi nzima, akapewa kesi ya ugaidi na kukaa ndani miezi Saba. Alipotoka tu Rais kamwita wayamalize.
 
Back
Top Bottom