Hongera Mwamba Freeman Mbowe Mwasisi wa Maridhiano

Hongera Mwamba Freeman Mbowe Mwasisi wa Maridhiano

Mbowe kusema kweli ni mtu wa kipekee kabisa;
Ameumizwa sana lakini hajawahi kuhimiza ubaya.
Amesingiziwa mengi lakini yeye hakuwahi kumsingizia yoyote.
Amenyanyaswa sana na kudhalilishwa lakini yuko kimya tu.
Huyu ni mzalendo na mpenda nchi yake kuwa na ustawi kwa faida ya wote na sio wachache.
Bravo Kamanda Mbowe

Historia itamkumbuka
 
It’s a process not an event bro.

“Katiba ni ya Watanzania siyo ya vyama vya siasa. Nataka kuwapa faraja kwamba mda si mrefu tutaanza.

Kamati itakayoundwa kwa ajili ya Katiba itaundwa na watu wa aina mbalimbali, itafanya kazi zake kwa maelekezo tutakayowapa, tutawapangia vizuri lakini siyo ile ya vuguvugu”. Rais SSH.

Kaongea vizuri Sana.
 
Mabadiliko au Uhuru wa kweli auletwi kwa njia ya kubembelezana kama alicho fanya Nyerere na sasa anacho fanya Samia hakuna kipya Tanzania tutapata tukiendeleza mtindo huu wa kunyenyekea na kubembeleza watawala .

Ndugu yangu tufanyeje?. CHADEMA walitangaza UKUTA JWTZ na Polisi wakaingia mitaani kufanya mazoezi na kitishia watu. CHADEMA haipambani na CCM inapamaban na dola lazima uelewe.
 
Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..

Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..

Usisahau UKUTA aliitisha Mbowe, JWTZ na Polisi wakaingia mitaani kufanya mazoezi. Tujifunze yaliyotokea Zanzibar, uchaguzi ulifutwa jeshi likaingia na vifaru, Maalim angefanya?. Tatizo tunakosoa tumelala vitandani wakati akina Mbowe wanalala magreza miezi Saba.

Halafu, ni Rais samiah ndio kamwita Mbowe ikulu siku ya kwanza na Hapo ndipo majadiliano yalipoanza.
 
Ndugu yangu tufanyeje?. CHADEMA walitangaza UKUTA JWTZ na Polisi wakaingia mitaani kufanya mazoezi na kitishia watu. CHADEMA haipambani na CCM inapamaban na dola lazima uelewe.
Wananchi kwa asilimia kubwa hawapo tayari kugharamia uhuru wa kweli, bali wana taka uhuru wa kweli kwa njia isiyo leta uhuru wa kweli hapo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Kupambana na dola lazima nguvu itumike hatuwezi kuishinda dola kwa maridhiano ambayo hayaitikisi dola bila kupigana dhidi ya dola kamwe hatuwezi kuishinda dola hii ni sheria dunia kote lazima ifuatwe.
 
Mabadiliko au Uhuru wa kweli auletwi kwa njia ya kubembelezana kama alicho fanya Nyerere na sasa anacho fanya Samia hakuna kipya Tanzania tutapata tukiendeleza mtindo huu wa kunyenyekea na kubembeleza watawala .
Sasa unamwambia nani? Wenzako wameona watumie hiyo approach kama ilivyokuwa kwa South Africa na hata Tanzania wakati zikipigania uhuru wao. Kama unaona njia hii haifai, una uhuru wa kuja na njia zako unazoona zinafaa na uzisimamie front kabisa na si kujificha nyuma ya keyboard na kutaka wenzako wafanye kwa niaba yako.
 
FB_IMG_1589397986327.jpg
 
Sawa
 
Ndio maana Lema alikuwa kimya, inawezekana alishapenyezewa nyepesi..
 
Rais kutoa zuio haram la mikutano ya hadhara.
Yeye ni nani hadi awe na mamlaka ya kitu kilichomo kwenye katiba?

Kitoa tamko lingine la zuio mnaanza kutafuta tena maridhiano?
 
Yeye ni nani hadi awe na mamlaka ya kitu kilichomo kwenye katiba?

Kitoa tamko lingine la zuio mnaanza kutafuta tena maridhiano?
Sukuma Gang mnaumia sana rudini kwenu Burundi mkachinjane huko,sisi tunataka amani
 
Back
Top Bottom