Ni vizuri kutumia mbinu zote kudai haki.. lakini hii mbinu ya kunyenyekea ina gharama pia..
Na gharama yake ni hii: Kutukanwa, kubezwa na kudharauliwa na ndugu zako mwenyewe...
kumbuka mikutano ikianza inaweza kuwakera ccm(Samia ) wakaifuta Tena..maana inaonekana mikutano Ni utashi wa Rais aliyepo madarakani..
Kwa mfumo wa utawala wa kikatiba na kisheria wa nchi yetu, hili linawezekana na ndiyo maana hata mwanzo (2015 - 2022) liliwezekana na kufanywa na Magufuli na Samia kuliendeleza mpaka dakika chache zilizopita....
Waliompinga mbowe hoja yao Ni kwamba..kwanini tunabembeleza kufanya Jambo la haki kikatiba..
Usipobembeleza katika mazingira haya ya kikatiba na kisheria unadhani kuna njia nyingine? Ipi? Mapambano?
Ukitumia njia ya mapambano utakuwa umekosa BUSARA na HEKIMA maana wewe na wenzako mtakufa tu na mnaopigana nao wataendelea kuishi.!!
Tazama Konyi wa Uganda na waasi wenzake dhidi ya serikali ya Uganda. Je, wamefanikiwa kuiangusha serikali ya Museveni..? Nenda Kongo DRC nk nk..
Kina Mbowe na wenzake wako kwenye njia sahihi kushughulika na utawala huu wa kimla chini ya CCM Kwa katiba ya JMT ya 1977...
Ni njia ya mwendo wa taratibu sana lakini ni salama na effective kuliko wengi wanavyodhani...
Tukumbuke mabadiliko yoyote ya kweli katika nchi yoyote ni mchakato unaotumia combination ya njia nyingi kwa kuipima Kila moja..
Hii ni hatua ya kwanza. Imefanikiwa hata kama Kuna wasiwasi huo uliouonesha hapo juu. Lakini at least kwa sasa kuna hatua iliyofanikiwa...
Next ni kushughulika na msingi wa utawala huu mbovu na wa kimla, yaani KATIBA na SHERIA mbalimbali za kukandamiza demokrasia na uhuru wa watu..
Tutafika tu maana hakuna lisilo la mwisho. Muhimu ni uvumilivu na kuchukuliana. Hata kama mabadiliko haya hatutayafaidi sisi, watoto na wajukuu wetu watayafurahia na kuikuta historia ya wapambanaji Hawa...