Nyerere alikuwa kidume. Nakumbuka nikiwa mtoto. Jumbe akatua uwanja wa Musoma. Hata akusalimia kamati ya ulinzi mkoa aliwapungia tu mkono na kuingia garini kuelekea Butiama.
Nakumbuka alionekana mtu mwenye mawazo sana. Muda mwingi alikuwa amejiinamia. Japo na utoto wangu nikajiuliza kwanini huyu amekuja kwa ghafla na dhararu wakati ni Makamu wa Rais na pia Rais wa Zanzibar?
Kikawaida wakati ule kila kiongozi anae fika Musoma. Alipokelewa na chipukizi na kuvishwa skafu pia kukabidhiwa mauwa.
Nikiwa wakati huo miongoni mwa chipukizi wa kudumu kupokea wageni wa kitaifa na kimataifa. Nilisogea karibu na kamati ya ulizi na usalama ili kupata umbea.
Wengi hawakuwa na furaha, nilipata habari kuwa anaweza ondolewa au kuvuliwa Urais. Nilirejea zangu nyumbani. Kilichoendelea Butiama hakikuwa cha kufurahisha. Abdu Jumbe aliondoka kimya kimya. Na kurudi Dar. Na ilitangazwa kuwa si tena Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wala si Makamu wa Rais. Ndipo Ally Hassan Mwinyi akateuliwa.
Abdu Jumbe akazuiwa asiende popote. Na kubaki Kigamboni.
Nirudi kwenye mada, kiusalama hasa wa Ikulu na usalama wa Rais, si rahisi na si vizuri kubadili mkurugenzi wa usalama wa Taifa kama ilivyo kwa viongozi wa kisiasa.
Mkurugenzi wa Usalama ndiyo mtu wa kwanza wa karibu kabisa na Rais ambaye anajua mengi si tu usalama bali mfumo mzima wa nchi ulivyo na unavyo kwenda.
Mkurugenzi huyu chini yake ana ma RSO na ma DSO na watumishi wengine vificho kibao. Swali je ameimarikaje ktk kujenga mitandao yake kwa hawa walio chini yake?
Mkurugenzi anawatu wake mpaka huko nje ya nchi balozini. Anawatu wake jeshini, polisi, magereza, na ofisi za umma na hata mashirika binafsi.
Mkurugenzi wa Usalama si mtu mdogo. Uwezi fanya mapinduzi ktk nchi bila kushirikisha watu wa usalama na hasa walio Ikulu.
Hivyo Rais awe makini, aisondoe mtu kisa tu kakataa kukubaliana na unachotaka. Viongozi wetu wanajisahau kuwa Usalama hawapo kutekeleza matakwa ya Rais. Bali wapo kwa matakwa ya nchi na raslimali zake. Watakulinda kiongozi wa nchi kwa sababu upo kulinda maliasili za nchi na kutetea maslahi ya Taifa.
Unapokwenda kinyume na maslahi ya Taifa, au kukiuka Katiba. Wanauwezo wa kutumia namna yoyote kukumaliza au kukuondoa madarakani.
Jumbe aliagiza watu wa usalama kwa mamlaka yake. Lakini hao hao ndo walio mnyang'anya passport na kumuweka chini ya ulinzi. Na kuzuiwa kigamboni.
Rais uwezi ukapewa kila kitu cha TISS. Utapewa habari ile wao watakayo amua ujulishwe. Lakini wanapokuchunguza wewe Rais uwezi pewa taarifa zako. Hizo ni zao wao wenyewe.
Trump aliondolewa na haohao watu wa usalama.
Mama Rais wetu, nakuona unavyojimwambafai, ukidhani huko salama saana. Ukidhani waokupa ushauri wanajua kila kitu. Kuwa makini.
Mageuzi uletwa na watu wa chini kabisa hata kama ni wanajeshi uwa si wale wajuu wenye vyeo, bali wa ngazi ya chini. Na hao wakubwa wanapata info zote toka kwa hawa wa nchini.
Utawabadili sana hao wakurungezi wa TISS, ila fahamu humo humo TISS mama umechokwa. Kwanza unaupendeleo. Kuna namna fulani unawatu wako unao wapa kipaumbele. Kuna watu hawafurahii. Usije muondoa mtu amabe alikuwa kesha jenga mifumo yote vizuri, na pengine ndo angekuwa msaada wako mkuu. Unapo mtoa kuna baadhi watabaki na vinyongo na hasa waliokuwa wanamsujudu.
Si kweli kwamba mtu akistaafu au kuachishwa ndo kwaheri hapati info. Ha ha ha! Hawa watu kumbuka wamekaa wakajijenga wanaelewa nini kinaendelea. Uwezi koswa wafuasi.
Magufuli alipomuondoa Kipilimba roho tu iliniuma ghafla. Nikajiuliza huyu alikuwa tayari kesha jenga mizizi. Anae kuja ni mgeni kwenye ofisi. Mpaka aanze kujijenga, lolote au chochote chaweza tokea. Penye mabadiliko ndo mara nyingi kunakuwa na mianya ya chochote. Matokeo uwa ni baadae.