Hongera na pole Balozi Siwa. Je, utaiweza TISS au TISS itakuweza?

Je Unafikiri uteuzi DG MPYA TISS kila wakati una maslahi kwa USALAMA wa TAIFA?

  • Ndio

    Votes: 46 22.1%
  • Hapana

    Votes: 162 77.9%

  • Total voters
    208
Alieteuliwa na kuapishwa jana katajwa hapa.Wakuu mko vizuri tusaidieni tu kuilinda hii nchi hatuna nyingine tunayoweza sema ni yetu
 
Una hoja nzito sana usikilizwe
 
Sina neno mkuu
 
Kwa maoni yangu kuna kitu kimoja
Mkurugenzi wa TISS kabla kuteuliwa kuna maswali mawili yanatakiwa kujiuliza anayeteua la kwanza huyo mtu ana sifa za kushika nafasi kubwa ya usalama wa Taifa jibu likiwa ndio

Linakuja swali la pili je anakubalika kiasi gani asilimia ngapi huko ndani ya TISS kwa viongizi wa juu na chini Lazima hizo takwimu zipatikane kwa njia zozote .Sababu kama hakubaliki huko ndani kwa kiwango kikubwa TISS watamnyima ushirikiano na haraka haraka wataunda mtu wao watakayekuwa wanampelekea taarifa nyeti za uhakika na kuunda TISS mbili ndani ya TISS na hiyo parallel yaweza leta mbeleni

TISS wanajuana vizuri sana ni kama JWTZ kuteua mkuu wa majeshi lazima kuwa makini mno kuangalia hivyo vigezo viwili yasitokee kama ya Kenya baada ya kufa tu Mkuu wa Majeshi Ogola kwa Helkopta visas vikaja kwa maaandamano yaliyomtoa mkuu wa usalama wa taifa wa Kenya.Kuwa hakuwa serious usalama wa mkuu wa Majeshi Kenya

Yale maandamano binafsi naona ni kazi ya usalama wa taifa wa Kenya wa chini ambao hawakuridhika kifo cha mkuu wa majeshi na kutoridhika na Mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Kenya na wakaenda mbali kuwa na aliyewateua must go

Yale maandamano ukienda deep mzizi uko chini sana sio wa generation Z ule
Akili iliyotumika maandamano yale iko beyond generation Z thinking kuanzia planning,secrecy ,execution etc

Katika sehemu zinataka utulivu wa kichwa kwenye uteuzi ni mkuu wa majeshi na Mkurugenzi wa usalama wa taifa

Hao wawili ni serikali huru ndani ya serikali zinazojitegemea zenye mamlaka sawa na Raisi hata kumzidi .Wakiamua aondoke ataondoka tu atake asitake kupitia angle yeyote ya heri au ya shari ya siri au ya wazi

Hizo nafasi za kuwa makini sana na mamlaka za uteuzi

Kuna siku nilimsikia Raisi Samia anasema siku ya muungano alipoona gwaride nzuri kikosi cha bendera kinapita na mwanamke anapiga gwaride zuri akinyanyua kimguu chake sana Raisi akasema huko mbeleni Jeshi lijiandae kupata mkuu wa jeshi mwanamke.Niliangua kicheko cha nguvu Sanaaaaaaaa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…