Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 2,091
- 1,918
SalaamJf,
Hope wote bila kujali itikadi za vyama vyetu vya siasa tunamfahamu fika CDE Hamphrey Polepole ambaye ameteuliwa kuwa mbunge.
Aidha, kwa mtizamo wangu kiongozi huyu tangu kuasisiwa kwa vyama vingi vya siasa huenda ndiye kafanya kazi kubwa sana ya kuwafanya CCM wafurahi na upinzani unune.
Ubora wake ndani ya CCM ni kama ifuatavyo:-
(i). Kasaidia ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2017. Hapa upinzani ulidhoofishwa sana bila shaka ushindi huo ulishika nafasi ya kwanza ukilinganishwa na chaguzi zilizopita. Sasa kwa CCM ilikuwa furaha ingawa kwa upinzani ilikuwa huzuni kubwa;
(ii). Kusaidia ushindi wa kishindo wa wabunge, wawakilishi, madiwani na wabunge wa viti maalum (wanawake). Hapa pia ni CCM pekee wawezao kufurahi lkn ni upinzani pekee wawezao kuhuzunika - kwamba kwa mara ya kwanza CDM anashinda Mbunge mmoja, kwa mara ya kwanza wabunge wa viti maalum CDM wanajaaliwa na kupewa ubunge - kwa ujumla CCM tunafahamu ulivyoitumia nafahamu ya uenezi ktk ujenzi wa chama kilichokuwa kimepoteza mvuto hapo awali - sasa na uendako hebu ng'aa kwa hoja na vitendo;
(iii). Ushindi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - CCM wana furaha kubwa, upinzani wanahuzunika. Ushindi uwe ulipatikana kwa goli la mkono au la lkn ushindi huwa ni ushindi tu - sasa mbinu hizo ulizotumia kuleta ushindi wa kisiasa hebu zitumie kuleta ushindi wa kumaliza umaskini nchini. CCM, CHADEMA, NCCR, ACT, CUF na wengine wasiokuwa na vyama wengi wao bado ni maskini - sasa hebu cheza nafasi yako kuutokomeza. Kisiasa nakuona tofauti na nape, chiligati. Hata hivyo wakati ukiongea na wanahabari Shukuru sana waliounga mkono jitihada zote za kujijenga chama, na uombe radhi kwa watanzania hususan wapinzani na Mungu lolote ulotenda kwa matakwa ya kisiasa.
Mwisho:
CCM kuna namna tutakavyokuombea huku upinzani nao wakiwa na namna watakavyokuombea - lkn tubaki kufahamu kuwa Mungu ni mkubwa.
Msakila M Kabende
Kigoma - Tanzania
29 Novemba, 2020