THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,950
- 13,527
Friends and Enemies,
Nimeifurahia kauli ya Mh RAIS ya KUTOA pole Kwa Msiba wa Ndug Ally KADA wa CHADEMA kilichotokea hivi karibuni. Inna Lillah waina illay Rajiun.
Rais Samia amefanya jambo jema Kwa kutoa kauli hiyo Kwa wakati na kujiweka mbali na kando na vitendo hivyo vya udhalim na ukatili,hakika Rais Hana Haiba ya ukatili huo.
Sasa basi,Kwa kuwa jambo la kifo halina upande,ni jambo ambalo sote tunapaswa kuliaani haijalishi alieuwawa ni CHADEMA, CCM au chama chochote,wa dini yoyote hata asie na dini,mwenye utimamu wa akili na punguani,kifo Cha dhulma Kwa namna yoyote ile hakina uhalali.
Tunaomba basi na kuwataka Jeshi la polisi watupe MAJIBU ya sakata Hilo kama kwamba huyo marehemu alikuwa ni KADA na mjumbe wa sekretariati ya CCM kama vile ambavyo alikuwa ni mjumbe wa sekretariati ya CHADEMA.
Na Kwa kuwa amri hiyo imetoka Kwa Rais,basi ingekuwa vema sana MAJIBU hayo sisi wananchi tukayapata kwa haraka na uwazi,ili hawa ambao wanafanya ufisadi na kumwaga damu katika Ardhi hii wafahamike na wachukuliwe hatua Kwa haraka kwani Kwa namna Moja ama nyingine wanaweka doa sana katika juhudi kubwa anazozifanya Rais za kudumisha Haki,AMANI na Demokrasia ya kweli ndani ya Taifa letu.
Soma Pia:

- Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao
- Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana