Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

🤣🤣🤣🤣🤣leo nimeamini Paskali kuna kitu unatumia sio bure...
Sijui ni mm tu nasomaga nyuzi zako huku macho yana machozi?? Yaani very funny jamani! Dah 🤣🤣🤣🤣🤣
Mkuu Waangari, kwetu ni Usukumani kijiji cha Gambosh, huko sio mchezo!.
P
 
Mkuu, hili umelitendea haki, Mh JPM anaishi na kuboresha zile fikra za JKN . kwa kuwa ile ndoto ya kuhamia Dom imeishatimia na kauli ya Mh Rais ilikuwa baadhi ya Majengo hapa Dar yanaweza kugeuzwa Hotel.

Sioni ajabu, Ikulu yetu nayo inavyoboreshwa ikawekwa kuwa Museum na ikawa ni kivutio kikubwa cha utalii wa ndani na nje ya nchi.

Kutembelea nje ya nchi pia ni Jambo bora kwa faida ya mengi, lkn hili la kuboresha Ikulu yetu hili lifanywe kivyetuvyetu zaidi ndiyo litakuwa na maana kiutalii.

Kutawala zaidi na zaidi kwangu mm sioni shida anapaswa atawale zaidi na zaidi kwa kuwa muono wake ni wa mbali anatuvusha katika njia sahihi ni suala letu kuamua katika sanduku la kura.

Naamini ni kipindi cha muda tu, tuishiyo mijini tayari tumepewa kila kitu na Mh JPM ametumia mapesa mengi kuboresha miji yetu aendelee ili ashuke kwa washangiliaji wa kweli kwa wanasiasa wetu kwenye vijiji.

Naamini akipeleka pesa yote iliyotumika mijini ikaenda kwenye vijiji, maji , afya , umeme Mabarabara , kilimo , masoko shule nk . Vitaimarika na vijana watarudi makwao mambo haya ya UMACHINGA kila Kona yataisha

Wakurugenzi , wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wataibua tena fikra za utendaji zilizokufa vichwani mwao. Kutenga maeneo ya biashara na kuboresha maeneo yote ya wazi.

Kuliko sasa wanavyofikiri Mh rais atawafokea wakiwagusa Machinga. Kiasi ubunifu wa kuwaandalia maeneo bora ya biashara umekufa.( ( Hapa unaotaka waende ulaya kujifunza sawa)
 
Huu utafiti ni wako au umeutoa mahali? hebu weka chanzo cha huu utafiti.
Au ulimbukeni na ufinyu wa kufikiri ndio uliokutuma kuandika huu upuuzi!
 

Nyuzi zako zinakuaga sooo sarcastic mpaka unaboa mkuu. Unaweza kusifiwa na mtu alietakiwa akuponde ama ukatukanwa na mtu alietakiwa akupongeze na hii ni kwasababu nyuzi zako zinachezea sana akili za watu. Lakini anyway pengine mimi ndo nina matatizo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugawaji wa Tausi huu Ugawaji wa Tausi, kabla ya Raisi Hajagawa tausi kwa wastaafu, kuna hotel inaitwa JS imeshapatiwa hao Tausi kitambo,

Ni mmiliki nani na nani hasa aliruhusu wato Ikulu?

Britannica
Mkuu Britanicca, acha uchokozi na uchochezi, tausi ni ndege tuu kama ndege wengine wote na wanapatikana mahali pengi.

Kwa bandiko hili, ikiamuliwa kufunguliwa kesi ya uchochezi, jee utaweza kuthibitisha kuwa hao tausi wa JS Hotel pale Chato ni tausi kutoka Ikulu yetu?, unamaanisha kuna mwizi kaingia Ikulu yetu, akawaiba wale tausi wa Nyerere pale Ikulu ambao ni nyara za taifa, akawapeleka huko JS hotel?.
Au anamaanisha miongoni mwa watu wenye access na Ikulu yetu, kuna mtu ni mwizi kaiba tausi wetu ambao ni nyara za serikali, na kuwauza kwa JS hotel ya Chato?.

This is criminal liability, hivyo kama kuna tausi wa nyara za serikali pale JS Hotel, Chato, na police wetu wanasoma JF, waanzishe uchunguzi hapo JS kuchunguza yafuatayo
  1. Jee ni kweli JS hotel ya Chato kuna tausi?.
  2. Waliwapata wapi hao tausi?
  3. Wana vibali vya kumiliki nyara za serikali?
  4. Kama ni tausi kutoka Ikulu yetu, nani aliruhusu nyara hizo za serikali kuchukuliwa na kupelekwa hotel binafsi?.
  5. Kama ni kweli tausi hao wa JS hotel ni kutoka Ikulu yetu, then huu nao ni ufisadi tuu kama ufisadi mwingine wowote!.
NB. Angalizo: Kufuatia JS hotel kuwa karibu na Ikulu ya Chato, usikute tausi ambao Mkuu Britanicca amewaona ni tausi wa Ikulu ya Chato wakiranda randa mitaani kama wale Tausi wa Ikulu ya Magogoni wanavyo randa randa maeneo mengi, and this being the case, hakuna kesi wala hakuna issue!
P
 
Chato kuna ikulu ? au ni 'ikulu'?
 


Hhaahhaahaha....siku zako zinahesasabika!nimecheka
 
Nimependa angalizo mkuu. Ni bonge la angalizo
 
Hongera sana Rais Magufuli kwa kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, pia tunakuombea utawale kwa muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10.

P
Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…