Wanabodi,
Leo kuna video clip ya Ikulu yetu ya Magogoni imepandisha humu, kiukweli nimekuwa very impressed na ile zoo ya Ikulu na jinsi wanyama walivyopendezea.
Kwenye mazuri wajameni tupongeze:
Wanyama pori waipamba Ikulu, Hongera sana Rais Magufuli
Nimesema kwa upande wa wanyama Magufuli ameipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, kwasababu wanyama Ikulu walikuwepo tangu enzi za Nyerere, kufuatia Ikulu kuwa na a limited surface area na wild animals natural habitat yao ni wilderness, ikaamuliwa wawepo wanyama wachache tuu for leisure kwa rais na wageni wake wakiwemo ndege tausi ambao sasa Ikulu ndio natural habitat yao.
Wilde animals bila kuwa na mazingira ya natural habitat hawawezi ku breed, hivyo kuweka idadi kubwa hivyo ya wanyama kwenye kieneo kidogo kile ni furaha peneza macho na mateso kwa baadhi yao, kumbe domestication of wild animals sasa sio just for leisure, sasa ni kuonyeshea!, hivyo na kwa vile serikali imehamia Dodoma, napendekeza Ikulu iwe Magogoni Zoo, na kwa heshima ya Magufuli, napendekeza Rais Magufuli akae Ikulu muda kama wa Nyerere au zaidi hadi pale Mungu atakapoamua!.
Tena unaweza kukuta uamuzi wa kufuga wanyama wengi hivyo kwenye eneo dogo lile, umefanyika bila EIA, kama tulivyoamua kununua ndege kwa cash huku hatuna business plan!. Sasa tuifanye Ikulu yetu kuwa kivutio cha utalii, vile vizuizi viondolewe, waweke
nominal fee watalii hadi wa ndani tutafurika.
Ni muhimu sana rais Magufuli afanye safari muhimu za nje ili kupata
exposure, akaone Ikulu ya South inavyofurika, pia aende Ikulu ya White House tena akiandamana na Makonda ili kumkomoa beberu Pompeo!, akaone jinsi wageni wanavyo jivinjari kwenye Ikulu ya White houseya Marekani. Hao wanyama na all the beauty ni bure kama watu hawatembelea na kuchangia upkeep cost.
Na kama hoja ya
restrictions ni usalama wa rais, maana naona ulizi wake unakaribia wa Mu7, then Ikulu Zoo iwe open to public zile siku rais yuko Dodoma ambapo pia I hope kutakuwa na Chamwino Zoo. Kiukweli ita-make hata kuliko Chato!
Hongera sana Rais Magufuli kwa kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, pia tunakuombea utawale kwa muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10.
P