Hongera Rais Samia kwa kuendeleza magorofa ya Morocco na Kigamboni

Hongera Rais Samia kwa kuendeleza magorofa ya Morocco na Kigamboni

BMWsimba

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
347
Reaction score
508
Jana nimepita moroco na Kigamboni magorofa ya hifadhi ya jamii yaliyokuwa yametelekezwa yote yameanza kuendelezwa kwa Kigamboni nimeona wanafyeka majani maana kule hata nyoka walishaanza kufanya makazi kwa msitu wa majani uliokuwa umeanza kuota.

Na kwa Morocco ilikuwa ni suala la aibu kutelekeza mradi mkubwa kama ule hata kama watu walikuwa wamepiga pesa wangetumbuliwa na mradi umaliziwe maana yote ilikuwa zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi na faida yake ilikuwa ishakaribia kuanza kupatikana. Sema mawazo ya mtu mmoja ndo yakasimamisha na hatukuwa na cha kumwambia kwa sababu ya propaganda za wakati huo.

Hongera mama kwa kuendeleza miradi muhimu
 
Project ya kigamboni ni hasara somehow
Lakini hili la Moroco square ile ilikuwa AIBU unaachaje project kama ile mji lzm upendeze kwa majengo mazuri ya kisasa bana ....
majengo ya moroco yalikuwa yameshafika stage ya mwisho ila mwamba akaamua tu kusimamisha hata kule kigamboni yalikuwa hayapo pabaya sema mwamba kila mtu alimuogopa hata kama ushahuri ulkuwa una manufaa watu walikaa kimya
 
Wangewauzia watu binafsi miradi hiyo. Wakisharudisha fedha za pension wawekeze kwenye viwanda.

Ile mieradi ingetoa viwanda vikubwa viwili na kuwapa vijana ajira na hapohapo kutengeneza faida kwenye mifuko ya wastaafu.
 
Hivi kile kiwanda cha sukari kimeishia wapi? uzalishaji umeanza? kinazalisha tani ngapi kwa mwaka/mwezi sukari yake mtaani ipo? inaitwaje?
 
na hatukuwa na cha kumwambia kwa sababu ya propaganda za wakati huo.
Ninakubaliana nawe kwa yote uliyoandika huko juu isipokuwa hapa umekuwa mnafiki/mwongo au yote mawili kwa pamoja.

"---hukuwa na cha kumwambia kwa sababu ya 'propaganda'...", hii ni kweli?

Siyo kwa sababu ya 'propaganda'; ni kwamba usingeweza kusema lolote wakati huo kwa kuogopa, kutekwa, kuuwawa, kupotea, kupigwa mabomu (kama ile ofisi ya sheria ya Fatuma Karume), au matukio mengine yoyote mabaya ambayo ungeweza kuyapata.

Hata hivyo usikimbilie kusifu unayemsifu sasa hivi, kabla hujajuwa mambo yake yalivyo. Anaweza asifanye kama hayo unayoogopa kuyataja hapa, akawa amekupa uhuru wote wa kuyatamka huku akikuuza kwa bei cheee bila mwenyewe kujuwa ni nini kimekutokea.
 
Hivi kile kiwanda cha sukari kimeishia wapi? uzalishaji umeanza? kinazalisha tani ngapi kwa mwaka/mwezi sukari yake mtaani ipo? inaitwaje?
Hata kama hakijaanza kuzalisha, hiyo haimaanishi kuwa viwanda visijengwe.
Itakuwa dhana potofu kufikiria kuwa kwa sababu kiwanda fulani kimeshindwa kuanza kazi basi viwanda visijengwe.
 
Hivi Kufanya tu Usafi kwa Watu Kufyeka Nyasi au kuona Watu wanafagia Majengo na Kuondoa 'Tandabui' Ukutani na kuzima Taa Alfajiri na kuziwasha Usiku ndiko kuendelea kwa Ujenzi huko? Kweli sasa naamini kuwa This is Tanzania.
 
Mama hana ule ujinga wa eti kulazimisha pension funds kwenda kulima miwa,hoho,sijui kudhona viatu na upuuzi kama huo.

Haiingii akilini kutumia fedha za wastaafu kwenye industry zenye risks kubwa kama kilimo na kuwatoa kwenye traditional investment zao za kununua bonds, real estates nk ambazo zina risks kidogo sana za kupoteza pesa za wastaafu

Pili hizi pension funds zilikuwa zinapendezesha miji yetu kwa kujenga majengo mazuri.
 
Kwani hiyo ni miradi ya serikali au ni ya mifuko ya jamii? Kikotoo kiliishia wapi?
 
Mama hana ule ujinga wa eti kulazimisha pension funds kwenda kulima miwa,hoho,sijui kudhona viatu na upuuzi kama huo.

Haiingii akilini kutumia fedha za wastaafu kwenye industry zenye risks kubwa kama kilimo na kuwatoa kwenye traditional investment zao za kununua bonds,real estates nk ambazo zina risks kidogo Sana za kupoteza pesa za wastaafu
Project ya kigamboni ni hasara somehow
Lakini hili la Moroco square ile ilikuwa AIBU unaachaje project kama ile mji lzm upendeze kwa majengo mazuri ya kisasa bana ....
Hakuna hasara hapo ni yule jamaa aliharibu uchumi zote hizo zingepata watu.
Mbona watumishi housing imejenga miradi huko Kigamboni na imepata wateja?
 
Wangewauzia watu binafsi miradi hiyo. Wakisharudisha fedha za pension wawekeze kwenye viwanda.
Ile mieradi ingetoa viwanda vikubwa viwili na kuwapa vijana ajira na hapohapo kutengeneza faida kwenye mifuko ya wastaafu.
Akili huna, pension funds iwekeze kwenye viwanda? Uliwahi ona wapi hili?
 
Hivi kile kiwanda cha sukari kimeishia wapi? uzalishaji umeanza? kinazalisha tani ngapi kwa mwaka/mwezi sukari yake mtaani ipo? inaitwaje?
Na cha kutengeneza mabuti kule Moshi 😆😆😆😆 ukiuliza hutaambiwa ukweli
 
Morocco pale haikuwa sahihi sana kupiga chini mradi, isipokuwa NHC wapunguze tu gharama za nyumba zao bei iendane na uhalisia wa maisha ya watanzania walau wa kipato cha kati na juu...

Kigamboni, hivi si kuna wakati serikali ilidai itapiga mnada zile nyumba watu binafsi waziendeleze? Isijekuwa mnada umeshafanyika au lah wanaweka mazingira safi kwa ajili ya mnada kufanyika
 
Mwendawazimu lilikua linafoka tu, eti bila ya ukichaa wake nchi haiwezi kwenda. Na wale legacy wakawa wanashangilia tu, ovyoo...
Nchi inasonga na Samia ,piga kazi mama, tuletee katiba mpya.
 
Jana nimepita moroco na Kigamboni magorofa ya hifadhi ya jamii yaliyokuwa yametelekezwa yote yameanza kuendelezwa kwa Kigamboni nimeona wanafyeka majani maana kule hata nyoka walishaanza kufanya makazi kwa msitu wa majani uliokuwa umeanza kuota.

Na kwa Morocco ilikuwa ni suala la aibu kutelekeza mradi mkubwa kama ule hata kama watu walikuwa wamepiga pesa wangetumbuliwa na mradi umaliziwe maana yote ilikuwa zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi na faida yake ilikuwa ishakaribia kuanza kupatikana... Sema mawazo ya mtu mmoja ndo yakasimamisha na hatukuwa na cha kumwambia kwa sababu ya propaganda za wakati huo.

Hongera mama kwa kuendeleza miradi muhimu
Kwa utaratibu huu ninaomba na jengo la gorofa la hoteli ya Nyota Tano ya NSSF ya Kapri Point Mwanza ikamilishwe mapema ianze kuchangia kwenye uchumi. Rais atupie jicho pale inasuasua sana.
 
Afadhali hata kufanya hivyo kunaleta matumaini,kuliko kwa ROHO MBAYA tu kuamua mambo yasiende,sasa kama watu walipiga,si walishapiga,kuliko kuacha iwe hasara kabisa majengo yaoze,si yamaliziwe tu?

Back
Top Bottom