Yoyote anayefahamu jinsi ambavyo nchi ilikuwa inaendeshwa awamu iliyopita anajua kuwa kulikuwa na decider-in-chief mmoja tu
Dhana ya collective responsibility na participatory leadership haikuwepo, kwani mamlaka ilikuwa centralized kwa mtu mmoja tu
Taasisi hazikufanya kazi. Mihimili haikufanya kazi, ni mtu mmoja tu ndiyo alikuwa anaamua kila kitu
Kwa hiyo mafanikio/kasoro za utawala uliopita ni mtu mmoja tu ndiyo alikuwa anaamua direction ya nchi na nini kinafanyika na inategemea ameamkaje siku hiyo
* Miradi ya miundombinu uliyotaja ni kweli ilianzishwa na Awamu ya 5, lakini Awamu ya 6 imeiendeleza na imeongeza kasi ya utekelezaji. Hii siyo kazi ndogo
Awamu ya 6 ilikuta SGR, JNHPP, Kigongo-Busisi na miradi mingine inasuasua kwa kukosa pesa, ikaimarisha uhusiano wa Tanzania na taasisi za kifedha na nchi wafadhili, ikaimarisha sekta binafsi na ukusanyaji wa kodii, pesa zikapatikana miradi ikaenda kwa spidi zaidi
SGR kipande cha Dar-Moro kilitakiwa kikamilike mwaka 2019. Kwa hiyo Rais wa Awamu ya 6 alipoingia madarakani Machi 2021 alikuta mradi huu tayari umechelewa.
Awamu ya 6 ikaongeza kasi ya utekelezaji wa.SGR na sasa unaona trial runs zimeanza Dar-Moro na treni na mabehewa ya umeme yameingia nchini.
Awamu ya 6 ilikuta ujenzi wa JNHPP unasuasua uko 30%, mradi unajengwa bila usimamizi mzuri, bila updated feasibility study (rejea ripoti ya CAG), ikaimarisha usimamizi wa mradi na upatikanaji wa pesa na sasa mradi umeanza kuzalisha umeme na umefikia 97%, unaenda kukamilika
* Awamu ya 6 imeingia wakati nchi iko katikati ya Covid-19 na uchumi wa dunia umedorora, lakini ikahakikisha kuwa miradi yote mikubwa iliyoikuta haisimami na ikaongeza kasi ya utekelezaji wake.
Awamu ya 6 iliikuta sekta binafsi nchini iko taabani kutokana na Covid na sera mbovu za serikali, ikarekebisha sera na mapambano dhidi ya Covid, sekta binafsi sasa imesimama na iko imara
Awamu ya 6 ilikuta wawekezaji wa nje wamekimbia nchi kutokana na sera, sheria na maamuzi yasiyotabirika ya serikali, ikaweka mambo sawa wawekezaji wa nje wakarejea
Awamu ya 6 ilikura kodi inakusanywa kwa mtutu wa bunduki na task force na biashara zinafungwa ajira zinapotea (the economy was shedding jobs), ikaagiza TRA watumie njia za kirafiki zaidi na matokeo yake makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango kikubwa
* Awamu ya 6 ilikuta elimu bure hadi Form 4, ikaongeza na kuweka elimu bure hadi Form 6. Imeongeza pia mikopo ya elimu ya juu kwa kiwango kikubwa
Ilikuta elimu, afya, maji, miradi ya elimu, barabara inasuasua, serikali ikapeleka pesa kwenye maeneo hayo kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu tupate uhuru
* Awamu ya 6 ilikuta kilimo, sekta inayobeba sehemu kubwa ya wananchi na uti wa mgongo wa taifa, ina bajeti finyu, ikaongeza bajeti yake kwa zaidi ya mara 4
* Ilikuta nchi imefungwa, baadhi ya viongozi wa upinzani wamekimbia nchi, mikutano ya siasa na maandamano marufuku, baadhi ya magazeti yamefungiwa, wastaafu, wasomi, NGOs na wananchi hawana uhuru wa kuongea, ikafungua nchi. Waliokimbia nchi wamerejea sasa wanaishi kwa amani na kuendelea na siasa wakiwa huru
Ilikuta mjadala wa katiba mpya umefungwa, ukaanzisha tena majadiliano ya katiba
Awamu iliyopita watu wakivaa t-shirt tu za Katiba Mpya walikuwa wanakamatwa na wengine kusakwa hata ndani ya nyumba za ibada
* Awamu ya 6 ilikuta nchi inatumia miti shamba kukabiliana na Covid-19 badala ya sayansi, haitaki barakoa wala chanjo, inaficha takwimu, ikaipeleka nchi kwenye njia ya sayansi ya kukabiliana na Covid-19 na kuruhusu chanjo, utoaji wa takwimu na kuokoa maisha ya mamilioni ya Watanzania
* Awamu ya 6 iliikuta nchi imejitenga na dunia imekuwa kama kisiwa kisichoeleweka na imepoteza mwelekeo, ikaiunganisha tena Tanzania na jumuiya ya kimataifa na sasa Tanzania imechukua tena nafasi yake miongoni mwa nchi za kistaarabu duniani na kama kinara wa diplomasia kwenye ukanda huu
* Awamu ya 6 ilikuta wananchi wanaishi kwa hofu kutokana na siasa za uhasama na watu wasiojulikana na kesi za money laundering. Ikaiunganisha nchi na kuondoa hofu. Wasiojulikana hawapo tena. Wananchi hawakamatwi tena na kuwekwa indefinite detention kwa kesi za money laundering na kesi nyingine za kubambikiza
* Awamu ya 6 ilikuta maelfu ya wananchi wako jela kwa kesi za money laundering na ujambazi, ikaagiza kesi za kubambikiza zifutwe, maelfu ya watu wakaachiwa. Imeunda tume ya haki jinai ambayo unaendelea kufanya kazi kuweka utawala wa haki nchini
Bado kuna mambo mengi ya kurekebisha, lakini tumetoka mbali kama taifa ndani ya miaka hii mitatu
- Mkazi mmoja wa Dar alisema