MTANZANIA620
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 105
- 116
Hali ya uzalishaji wa umeme nchini kutoka vyanzo mbalimbali na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa imeongezeka toka megawati 1,601.84 mwaka 2020/21 hadi megawati 4,031.71 April, 2025. Hivyo tuna umeme wa kutosha na ziada.
Pamoja na juhudi za kuongeza uzalishaji, serikali imekua ikitekeleza mradi wa Gridi imara kwa lengo la kuondokana na kukatika kwa umeme hapa nchini. Hii imepelekea hali ya kukatika kwa umeme nchini kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini (EWURA) ya Machi, 2024 imeonesha imepungua kwa asilimia 48 na dakika za kukatika kwa umeme zimepungua kwa asilimia 64 toka dakika 1,536 mwaka 2022 hadi dakika 554 mwaka 2024.
Ripoti hiyo pia imeonesha kukatika kwa umeme nchini kunatokana na sababu za kimiundombinu zaidi ya usafirishaji na usambazaji. Ndio maana serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Gridi Imara.
Kwa mfano Nchi yetu inahitaji vituo vya kupoozea umeme toka kwenye Gridi 216 kujengwa katika kila wilaya nchini ambapo kwa sasa vipo vituo 132, hivyo kuna uhitaji wa vituo 84 na katika bajeti ya mwaka 2025/26 serikali imepanga kujenga vituo vya kupoozea umeme toka kwenye Gridi 14 huku ujenzi wa kila kituo kimoja ikigharimu shilingi bilioni 35, kituo kidogo cha kawaida cha kupokea umeme wa kilovolt 33 ni shilingi bilioni 8 pamoja na ujenzi wa switching stations kwenye maeneo ambapo laini zinasafirisha umeme umbali mrefu na zinahudumia eneo kubwa na wananchi wengi ili kuwezesha wakati wa hitilafu au dharura umeme uzimwe upande na upande mwingine uendelee na huduma.
Serikali imeeleza mipango ya kuzalisha umeme wa megawati 5000 toka joto ardhi (geothermal) pamoja na kufanya mapitio ya bei za umeme kwa watumiaji kwani kwa miaka kumi hazikuwahi kufanyiwa mapitio.
Kesho yetu ni njema kwenye suala zima la umeme.
#TunaendeleaNaSamia #NishatiUhakika