Hongera Rais Samia Kwa Ukusanyaji wa Mapato kwa Asilimia 99% kupitia TRA

Hongera Rais Samia Kwa Ukusanyaji wa Mapato kwa Asilimia 99% kupitia TRA

Kinachoongelewa na hali ilivyo mtaani vinapishana tunadanganya kumfurahisha nani sasa?Watu wakisema mseme wanapinga kila kitu?
Mtaani Hali ikoje? Hizo pesa zimekusanywa kutoka mbinguni? Kwani Serikali ikikusanya inawagawia wananchi?
 
Kama hizi taarifa ni za kweli basi pongezi zimfikie mama Samia Suluhu kwa kuyafanikisha haya bila kumteka hata msemaji wa timu ya mbeya kwanza
 
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha nusu ya kwanza wa fedha 2022/2023 kuanzia julai hadi disemba mwaka jana, imekusanya sh trilioni 12.46 sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 12.48.

Kwa mujibu wa Kidata makusanyo hayo ni ongezeko la sh trilioni 1.35. kwa namna ya pekee TRA inatoa shukrani kwa Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kusaidia katika utekelezaji wa mikakati ya kiutendaji.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT..

Nitoe pongezi zangu za dhati kwa Mh.Samia SS na Serikali yake kupitia TRA kwa kuweza kukusanya mapato kwa Asilimia 99%..

Kiwango hiki kimeiwezesha Serikali kutekeleza ajeti yake ya mwaka 2021/2022 kwa zaidi ya asilimia 95%..

Bila shaka Rais Samia anazidi kuonesha uongozi wenye matokeo na sio maneno ya kujigamba na vitisho..

Nitoe wito kwa TRA kuendelea kukaza zaidi maana bajeti mpya ni kubwa zaidi ya iloyoisha hivyo mapato ni lazima yapatikane Ili kutimiza kiu ya mh.Rais ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Mwisho niwapongeze walipakodi nikiwemo mwenyewe kwa uzalendo huu, tuendelee kuchapa Kazi Ili Kazi iendelee.👇

View attachment 2279047View attachment 2279048
Hili halina mpinzani
 
Upuuzi mtupu

Yaani tunafurahia makusanyo ambayo haiwezi kukidhi bajeti ya nchi

Mfano una bajeti tshs 10 kwa mwaka halafu uwezo wako wa kukusanya ni tshs 4 kwa kutumia vyanzo vya kukariri sio vipya,nakshi(surplus) ya kufidia bajeti yako tshs 6 ni mkopo unaokuja na kila aina ya masharti,unajisifia nini hapo?

Eti tunashangilia tumevunja record, watanzania tumerogwa na nani?
 
Nawasalimu kwa jina la JMT..

Nitoe pongezi zangu za dhati kwa Mh.Samia SS na Serikali yake kupitia TRA kwa kuweza kukusanya mapato kwa Asilimia 99%..

Kiwango hiki kimeiwezesha Serikali kutekeleza ajeti yake ya mwaka 2021/2022 kwa zaidi ya asilimia 95%..

Bila shaka Rais Samia anazidi kuonesha uongozi wenye matokeo na sio maneno ya kujigamba na vitisho..

Nitoe wito kwa TRA kuendelea kukaza zaidi maana bajeti mpya ni kubwa zaidi ya iloyoisha hivyo mapato ni lazima yapatikane Ili kutimiza kiu ya mh.Rais ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Mwisho niwapongeze walipakodi nikiwemo mwenyewe kwa uzalendo huu, tuendelee kuchapa Kazi Ili Kazi iendelee.👇

View attachment 2279047View attachment 2279048
Data za kupika hizo😠😠😠😠😠

1. Makusanyo ya 99% umeyatoa wapi wakati Vituo vya mafuta vya wakubwa vyote havitoi EFD?

2. Matching guys hawalipwi zile 20,000 zilizokuwa zinaipa Serikali pesa chap chap, makusanyo ya 99% yatoke wapi?

3. Tanzanite na raslimali za Nchi zinaripotiwa kutoroshwa kimagendo Kila uchwao, hiyo 99% unaitoa wapi?

4. Watumishi wa TRA wanakaa mezani na walipakodi waovu kukubaliana kukwepa Kodi Kwa manufaa binafsi, unaitoa wapi 99%?

5. RUSHWA ktk Nchi imeongezeka maradufu ktk Nchi, unapata wapi takwimu ya makusanyo ya 99%?

Huu ni mwaka mpya 2023, Siri nyingi zitakuwa wazi kabisa, jiandae kutafuta pa kufichia aibu.

Aamen.
 
Hayo hayahusiani Bali haya makusanyo sehemu yake inatumika kulipa mikopo kutoka Huko Kwa mabeberu wako.
Wanajumlisha Hadi mikopo wanayopokea wanaijumuisha kwenye makusanyo, Wapika data,

Uwe na nakusanyo 99% halafu ukose pesa ya kulipa stahiki za wafanyakazi na malimbikizo ya madai na mishahara, malipo ya uhamisho, nk, nk nani umdanganye???

Rais amekiri kuwa Serikali I Amna ela ndomana Anakopa, hata mishahara saiz Hadi tikakope kulipa watumishi.

Shame on you😠😠😠😠😠
 
Kuwa chawa wa mama raha sana
Chawa King'ang'anizi
JamiiForums3817054.jpg
 
Pongezi kwake Dr. Samia, baadhi ya watu hawakutegemea kama angeweza kufanya mambo makubwa, sasa nguvu, ujasiri na weledi wake unadhihirika na kuwaacha wazandiki midomo wazi!!!
 
Vipi matumizi?

Au huko hakutuhusu?
angalia miradi inavyo songa kwa kasi.

1. Daraja la Busisi
2. Bwawa la nyerere
3. SGR
6. Barabara kuu na za vijijini
7. Hospitali.
8. Elimu bure hadi form 4
9. Mikopo ya Elimu ya juu
10. ujenzi wa madrasa.
11. Upanuzi wa bandari zote nchini.
13. kukamilika kwa ujenzi wa ikulu ya dodoma

14.

n.k n.k
hayo ni baadhi tu ya maeneo fedha hizo zinapelekwa, na mambo tunayaona, mwenye macho haambiwi tazama.
 
angalia miradi inavyo songa kwa kasi.

1. Daraja la Busisi
2. Bwawa la nyerere
3. SGR
6. Barabara kuu na za vijijini
7. Hospitali.
8. Elimu bure hadi form 4
9. Mikopo ya Elimu ya juu
10. ujenzi wa madrasa.
11. Upanuzi wa bandari zote nchini.

n.k n.k
Leteni numbers. Kabati lenye matumizi yote. Tutachambua yapi mnafanya ya maana, yapi luxury za viongozi na ya upigaji pia.

Per diem na ununuzi wa LC300 mmetumia shilingi ngapi katika kipindi kilichopita? Misafara na masherehe ya kitaifa?
 
kazi iendelee.....
Sasa umefika wakati wa kufuta Kodi,ada,ushuru,tozo zote sumbufu(nuisance)kama kweli mapato ya TRA yaridhisha kihivyo.kama bajeti ya serikali imepangwa vizuri na imetokana na mpango kamilifu,hakika hatupaswi kutenda nje ya bajeti na hatupaswi kutoza au kutumia nje ya bajeti.au kuchomeka mradi mpya nje ya bajeti iliyopitishwa mwanzo ,lands kama ikibidi tubadilishe mradi uliokwisha pitishwa kwa mradi mpya.nasema si sawa bajeti imepitishwa ya trilloni 43 alafu ukatekeleza bajeti ya trilioni 90,hapo ni lazima wananchi waumizwe sana.
 
Leteni numbers. Kabati lenye matumizi yote. Tutachambua yapi mnafanya ya maana, yapi luxury za viongozi na ya upigaji pia.

Per diem na ununuzi wa LC300 mmetumia shilingi ngapi katika kipindi kilichopita? Misafara na masherehe ya kitaifa?
Hilo hlina shaka kwasababu Mama ni mwadilifu anaye heshimu utawla wa sheria, ni muwazi na mwenye uchungu wa dhati kwa wananchi wake lakini kubwa zaidi ana hofu ya kweli kwa Mungu.
tunamuamini bila chembe ya mashaka.
 
Back
Top Bottom