Hongera Rais Samia Suluhu Hassan, Sasa rasmi, Tundu Antiphas Lissu amekusafishia njia Kimataifa

Hongera Rais Samia Suluhu Hassan, Sasa rasmi, Tundu Antiphas Lissu amekusafishia njia Kimataifa

Hata wewe waweza kuomba hivyo kama usemavyo kwa watu wote, ila mie nimeomba MABORESHO kwa watumishi wa UMMA hasa kwenye "retantion fee" ina maumivu sana
Huu ubinafsi ndo unaleta kutofanikiwa. So, wa private na self employed waachwe nje?!!!
 
Km Mama Samia haleti katiba mpya , basi Hana lolote jipya na yeye kuwa Rais hakuna positive impact yyte kwa maisha ya Watanzania
 
Katiba Mpya tu, kwangu mengine yote kelele.

Naona comments kule juu kila mmoja anavutia kundi lake, kwa mtindo huu tutaendelea kutawaliwa sana na CCM, coz mpaka sasa imeshafanikiwa kutugawa.

Wengine masheikh watolewe gerezani (dini), wengine bodi ya mikopo (wanafunzi), wengine fao la kujitoa (wafanyakazi) nao wanaharakati hawataki kesi za kubambikiziwa, ni vurugu tupu.

CCM kwa ujanja wao watachukua kundi moja au mawili kati ya hayo hapo juu wawape wanachotaka then maisha yaendelea mbele kwa mbele, mnasahau Katiba Mpya itayaleta hayo yote mnayoyataka kwa pamoja, tuamke.
 
KATIBA
KATIBA
KATIBA

Nje ya hapo ni kupoteza muda na kujilisha upepo. Watanzania mtazinduka lini?!!
 
Na awapige stop watu kama Chalamila, Ole Sabaya, DC wa Arusha na wengineo wa namna hiyo waache kuendekeza kiki za kipumbavu.
 
MATAGA watagoma mkuu, maana wanajua KATIBA mpya itawapeleka kule wanastahili kuwa - MUSEUM (a.k.a Makumbusho)
Hii nchi sio ya shangazi yao, ni ya kwetu sote (watanzania).
 
Amani iwe nawe Mama yetu,
Napenda tu kukwambia, kati ya mambo ambayo wadau wa kimaendeleo wanayaangalia juu ya kiongozi ni maoni ya wapinzani wake juu ya utawala wake.

Maoni ya mpinzani wako kwanza yanawapa confidence development partners, pili yanawapa trust foreign investors na tatu yanakujenga vizuri ndani na nje.

Napenda kukwambia Rais wetu, Tundu Antiphas Lissu katika kipindi cha jana katika channel ya Voice of America, amekusafishia njia, sasa ni wewe tu kufanya yale mazuri Yaliyo moyoni kwako.

Najua unaendelea kusafisha nyumba yako ili maono yako juu ya Tanzania Nzuri yenye maendeleo na mafanikio tele yapate kutimia. Naomba Mama yetu usiache kusafisha nyumba yetu hasa kwa wale watu waliochafua taswira juu ya nchi yetu huku nje, Upande wa mashtaka kwa kesi za kubambikiza juu ya raia na wanaharakati, wale walionyanyasa watu kwa kuteka watu, kuwaweka ndani na kuwashtaki kwa makosa ya uongo ,pamoja na wale waliominya uhuru wa vyombo vya Habari.

Kwenye uchumi usiacha kushughulika na tabia zile za kufungia biashara , kufirisi makampuni na kufanya uwekezaji ushuke Tanzania na watu wakose ajira
Rais Samia Suluhu Hassan anafahamu usanii wa wapinzani. Siku ile alisema bila kipepesa macho kuwa Hakuna askari wa jeshi lolote la Tanzania atakayempiga mtu risasi 20 asife. Lisu afahamu huyo ndiye rais wake na anaufahamu usanii wake.
 
Back
Top Bottom