Hongera RC Chalamila Kwa utumishi uliotukuka Kwa Kupambana na biashara haramu ya ukahaba, LAKINI.....

Hongera RC Chalamila Kwa utumishi uliotukuka Kwa Kupambana na biashara haramu ya ukahaba, LAKINI.....

Hii biashara ihalalishwe watu walipe kodi. Ulaya wanalipa kodi na hizo kodi ndiyo misaada tunayopewa.

Ulaya ukienda naye malaya anakupa na risiti.
Acha basi,

Yaani mvua zinanyesha, watu waache kulima wakakodishe miili?

Laanatul!!
 
Hii biashara ihalalishwe watu walipe kodi. Ulaya wanalipa kodi na hizo kodi ndiyo misaada tunayopewa.

Ulaya ukienda naye malaya anakupa na risiti.
Kweli kabisa amsterdam na brussel wamejenga km hivyo sema wenzetu wameeka vioo tu😂😂
 
Salaam, Shalom!!

Ulichokifanya ni WAJIBU wako kama kiongozi, ila Si vibaya kukupongeza sababu wamekuwapo wakuu wa mikoa wengi tangu uhuru lakini hawakupata mafanikio kama uliyofikia Hadi sasa!! Kongole!!!🙏

Kupambana na biashara ya ukahaba inahitaji mtu kuwa na akili kama ya Mwendawazimu, katika hili nakupongeza sana.

Umetumia GIA kubwa, ya kubomoa nyumba zilizotumiwa kufanya biashara ya madanguro, baadhi ya nyumba,milango imengolewa MADIRISHA nknk ,Na nyumba zilizokumbwa na kadhia hiyo ni nyumba za uswahilini.

Naamini hujakurupuka kuchukua hatua hizo, naamini unazo SHERIA zinazokulinda kufanya hivyo, kwamba ikitokea wamiliki wa nyumba hizo wakifungua kesi mahakamani kudai nyumba zao, una pa Kutokea, naamini zipo SHERIA zitakulinda kwamba, iwapo nyumba yenye leseni ya makazi ikitumika kufanya biashara haramu nyumba inavunjwa....

Tumeona, magari au marori yaliyobeba mihadarati yakitaifishwa bila kujali mmiliki alihusika au hakuhusika kubeba mihadarati hiyo.

Umeenda mbali na kupiga MARUFUKU mabaa kutowakaribisha wadada hao haramu.

FAIDA ZA KUTOKOMEZA MADANGURO NA BIASHARA HARAMU YA UKAHABA.

1. KUDHIBITI VITENDO VYA USHOGA .

Madanguro pia yalikaribisha mashoga, hivyo umepiga ndege wawili jiwe moja.

2. KUONDOA AJIRA HARAMU YA WATOTO.

Ukahaba ulifanywa Hadi na watoto chini ya miaka 18, hili lingetufikisha pabaya sana.

3.KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA.

Ukahaba na uuzaji na Ununuzi madawa ya kulevya ulienda sambamba hivyo kudhibiti ukahaba ni kudhibiti biashara hiyo pia.

4. KUIMARISHA MAADILI KATIKA JAMII.

Madanguro yaliondoa Heshima ya mzazi mbele ya JAMII maana vitendo hivyo haramu vilifanyika hadharani katika nyumba za familia watoto wakiona.

5. KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.

MAKAHABA na majambazi hushirikiana kuumiza familia nyingi, kudhibiti madanguro itapunguza uhalifu huo.

6. KUIMARISHA NDOA.

NDOA nyingi zilivunjika sababu ya tamaa ya wanawake kutamani pesa haramu Kutoka biashara haramu ya kujiuza, umesaidia NDOA nyingi zitaimarika.

7.PANYA ROAD& WATOTO MITAANI WATAPUNGUA.

Ukahaba ni chanzo Cha kutupwa hivyo watoto, utoaji mimba na kuzagaa hivyo watoto wasio na malezi ya wazazi.

KUDHIBITI ukahaba, kutusaidia kuinua malezi ya watoto, Panya road pia WATAPUNGUA.

ANGALIZO: Hatua ulizochukua Kwa madanguro, kamwe usijethubutu kufanya kwenye nyumba za Ibada zisizo na KIBALI au usajili. Nimewahi kukusikia ukisema unaweza siku moja kufuta makanisa.

Njoo Polepole, Angalia Rungu ulilolishika lisirudi kukuponda. Hayupo mwenye mamlaka na uwezo kufuta Kanisa, kujaribu kufuta makanisa ni kutunishiana misuli na Muumba, mshindi katika Hilo anajulikana.

Lakini Kwa hatua ulizochukua kuhusu madanguro nakupa kongole 🙏.
Tofauti yako na Lucas Mwasambwanda nikutochomeka nambari ya simu mwishoni ila ulefu na kila kitu same size.
 
Tofauti yako na Lucas Mwasambwanda nikutochomeka nambari ya simu mwishoni ila ulefu na kila kitu same size.
Vp nawe ni mteja wa hao walofukuzwa?

Penye Kweli lazima usemwe UKWELI ulivyo, pa kukosoa tunakosoa.
 
Mm kwa mtazamo wangu hakuna mkuu wa mkoa alie iweza dar kama Makonda yule jamaa acha kabisa alikua na vibe sana .Huyo jamaa aliepo anatakiwa awe huko polini hana vibe.Dar inataka watu wababe wajanja janja km walivo watani zangu wazaramo.
 
Hivi vibe na mihemko, ni kitu kile kile au tofauti?
 
Hii vita ikisimamiwa na mwanamke inaweza kufanikiwa. Wanaume wote hushindwa vita hii maana wengi wao pia huwa ni wateja wa biashara hii haramu!
 
Hii vita ikisimamiwa na mwanamke inaweza kufanikiwa. Wanaume wote hushindwa vita hii maana wengi wao pia huwa ni wateja wa biashara hii haramu!
Doroth Gwajima ni Waziri tena mwanamke,

Amesaidia kiasi Gani KUTOKOMEZA tatizo hili nchini?
 
Afadhali wadhibitiwe, wamezidi sana UOVU!!
Uovu huko palepale sema walikokuwa wanafanyia huo uovu wao ni pachafu sana, kwa sasa watakuwa wanapatikana fb kwa wingi na zitakuwepo guest house maalum na mambo yataendelea kama kawaida, kilichozuiwa ni nyumba binafsi kugeuzwa kuwa danguro, hii ni sawa na kuwafungia mama ntilie unadhani watu kweli watashinda na kulala njaa, kwa hali yoyote ile watakula tu hata kwa gharama.
 
Serikali haipaswi kudhibiti au kupambana na ukahaba, haya ni mambo yo dini kupambana nayo.
 
Mm kwa mtazamo wangu hakuna mkuu wa mkoa alie iweza dar kama Makonda yule jamaa acha kabisa alikua na vibe sana .Huyo jamaa aliepo anatakiwa awe huko polini hana vibe.Dar inataka watu wababe wajanja janja km walivo watani zangu wazaramo.
Makonda alifanya nini kama alama ?
 
Kuna madanguro ya ukahaba kwa gia ya Massage!! Asilimia 99 ya sehemu wanakodai kufanya massage ni ukahaba mtupu!! Hasa Sinza ndo kumejaa madanguro hayo yafanyayo ukahaba kwa gia ya massage!!
 
Na makanisa yaliyojengwa hovyo na hayana vibali ni lazima yabomolewe.
KANISA na danguro ni vitu viwili tofauti.

KANISA linapeleka watu Mbinguni, Madanguro yanapeleka watu Kuzimu!!
 
Back
Top Bottom