.
Mwanamayu, DISCO UDSM. mbona ni kitu cha kawaida, mimi pia nimesoma sheria hapo UD, nimejiunga na chuo na DIV II, wakati bila DIV 1 Sheria hupati.
Tulijiunga na vichwa vyenye DIV 1 kali toka haya mashule ya Academic na ma-international, mwisho wa siku, kuna wengi tuu walio Disco na Div I zao, na kuna wengi waliopata Upper 2nd na Div II zao.
Hata mimi binafsi niliDisco 2nd-year, na kutoka na upper 2nd mwaka wa mwisho. Kudisco Chuo, hakuna maana ndio kilaza, kuna maprofesa wazuri tuu hapo hapo chuo, vichwani akili nyingi, kwenye kufundisha ni vilaza tuu. Na kuna wanafunzi wa kawaida tuu, maksi za kawaida, ili hali ni vichwa kiukweli ukweli.
Tusihukumu watu for what they did/were, bali tuwahukumu for what they do now and in future.
Nawapongeza wanasheria wote waioukwaa uwakili, kusoma sheria ni kitu kimoja, kuwa wakili ni kitu kingine, ila kuwa wakili mzuri, ni kingine kabisa na hakina uhusiono ulikuwa mzuri vipi darasani, ndio maana mawakili wengi wazuri, wamepata pass tuu kama kina Mkono, na vile vichwa haswa vya sheria, vyenye Ist Class, kama kina Prof. Kabudi, huishia kwenye chaki ubaoni, na wakisimama mahakamani, ndio kama vile "amicus curiae", yaani friends of the court!.
Pia naomba msiwashangao, waandishi kumshobokea kijana wa Mzee, big names, makes news as well as prominance makes news, kijana ana both, silver spoon from 1st familiy, his own merit kwenye UV-CCM, sasa personal achievement as a member of the Bar from his own brain. Kati ya degree za kupewa pale UD, LL.B haipo, kila aliyesoma LL.B na kumaliza ni mwanasheria, ila sio kila aliyesoma LL.B na kuhitimu ni wakili.
Kwa hili la uwakili jamani, hongera zake mpeni!.