Hongera Ridhiwani Kikwete!!!

Hongera Ridhiwani Kikwete!!!

Kwa uelewa wangu mdogo

Disco ni kifupisho cha discontinued maana yake

  1. To stop doing or providing (something); end or abandon:
  2. To cease making or manufacturing...
  3. To cease subscribing to.....
  4. To terminate
  5. To come to an end....
  6. Stopped permanently
Kwa maana hizo hapo juu haiwezekani ukawa discontinued halafu mwisho wa program uapate cheti, otherwise kama kuna kitu kilifanyika kutengua hilo disco....vinginevyo mkuu Pasko unataka kusema kisicho cha kweli!
 
Unajisifia kudisco, wewe mzima kweli???
M-bongotz, sijajisifia, nimeshuhudia tuu yaliyonikutaga pale chuo, wapenda mizifa au kutaka kuoneka perfect ndio kujikwaa wanaona noma, wanafanya siri, tena nashukuru utawala wa chuo, huo hautoa majina, ni namba tuu, hivyo hata aliyechezea disco, ni siri yake na moyo wake, lakini kwa sisi wengine, kujikwaa, kuanguka, kusimama, kujifuta vumbi na kuendelea na safari, ndio maisha yetu. Kama kukubali udhaifu ndio kujisifu, then, thanks.
 
Mkuu Pasco, rekebisha hapo maana huwezi disco 2nd year na umalize kwenye chuo hichihicho!!!

Rudi fasta mkuu urekebishe......
.
Nyunyu, ndio maana nikasisitiza kuwa jamani, sio kila anaedisco ni kilaza, na pia kuna technical disco, usipofanya paper 3, ni disco outright, kwani disco halina appeal, si una appeal, anatoa sababu zilizopelekea ukashindwa kupiga hizo paper husika, sababu zikikubaliwa, unapewa special exam, unazipiga na unaziclear, whats a big deal jamani?.
 
ukidisco chuo kikuu manake ni home tuu, yaani hakuna disco afu tena uje umalize...either uliapply chuo upya so ukaanza tena..ila kama ulidisco na ukaja kumaliza ndo haya wanaita magumashi, mtu anadisco lakini mbinu zinafanyika, anapewa maksi masomo machache (hata likiwa moja kama litaweza kumuondosha na adha ya kudisco) then anaendelea kudunda....so mkulu pasco huwezi disco afu ukamaliza tena sijui na upper second sijui kitu gani..
,
Kwa LL.B ya UD ninavyoijua mimi, its either you earn it, or not, hakuna magumashi, ndio maana nadhani tunaelekea miaka 15 au 20 hakuna 1st Class pale, huku Mzumbe na Tumaini na Open ni ma 1st ya kumwaga.

Msisitizo tena na bold kabisa, SIO KILA ANAE DISCO NI KILAZA!. ZIKO TECHNICAL DISCO KIBAO TUU NA ZINAPANGULIWA!
 
Kwa uelewa wangu mdogo

Disco ni kifupisho cha discontinued maana yake

  1. To stop doing or providing (something); end or abandon:
  2. To cease making or manufacturing...
  3. To cease subscribing to.....
  4. To terminate
  5. To come to an end....
  6. Stopped permanently
Kwa maana hizo hapo juu haiwezekani ukawa discontinued halafu mwisho wa program uapate cheti, otherwise kama kuna kitu kilifanyika kutengua hilo disco....vinginevyo mkuu Pasko unataka kusema kisicho cha kweli!
.
Masa, ukweli ndio huo, labda tutafute tena prospectus ya miaka hiyo, tusome rules na regulations zinazopelekea mtu kudisco, hivi kwani disco ndio final?, si kuna appeal?, sababu za appeal zikikubaliwa, kama ni disco la low marks si unarudia mwaka?, kama ni disco la technical, si unapewa special exam, ukipasua, unasonga mbele!. Whats a big deal?.

Naombeni tuufunge huu mjadala wa disco usichafue hali ya hewa kumpongeza kijana.

Kuwa advocate jamani, its not a joke, wako majaji kibao sio ma-advocate na wakisha staafu ndio wanaomba na wengine hushindwa mitihani!

Kijana mdogo huyu, kasoma juzi juzi tuu, amepetition na kupata uwakili, ni jambo la kustahili pongezi. Hizi ni personal success, has got nothing to do na baba ni nani, labda tuu kwa sababu ni yeye, mtoto wa fulani, ndio basi hizo kamera, na hao waandishi wakakomelea hapo hapo kwenye big names makes news, plus prominance, kwenye sekta ya habari ndio kwao.

Lazima tufike mahali tukubali unaweza kuwa ni mtoto wa fulani mwenye prominance yake, ukajikuta unakuwa popular on your own na sio kwa mgongo wa prominence ya baba, lakini hatimaye ukaibuka kuwa celebrity kuliko hata mwenye prominance yake.

Pongezi tumpe na kurudi kwenye mijadala ya maslahi ya taifa.
Asanteni.
 
.
Mwanamayu, DISCO UDSM. mbona ni kitu cha kawaida, mimi pia nimesoma sheria hapo UD, nimejiunga na chuo na DIV II, wakati bila DIV 1 Sheria hupati.
Tulijiunga na vichwa vyenye DIV 1 kali toka haya mashule ya Academic na ma-international, mwisho wa siku, kuna wengi tuu walio Disco na Div I zao, na kuna wengi waliopata Upper 2nd na Div II zao.

Hata mimi binafsi niliDisco 2nd-year, na kutoka na upper 2nd mwaka wa mwisho. Kudisco Chuo, hakuna maana ndio kilaza, kuna maprofesa wazuri tuu hapo hapo chuo, vichwani akili nyingi, kwenye kufundisha ni vilaza tuu. Na kuna wanafunzi wa kawaida tuu, maksi za kawaida, ili hali ni vichwa kiukweli ukweli.

Tusihukumu watu for what they did/were, bali tuwahukumu for what they do now and in future.

Nawapongeza wanasheria wote waioukwaa uwakili, kusoma sheria ni kitu kimoja, kuwa wakili ni kitu kingine, ila kuwa wakili mzuri, ni kingine kabisa na hakina uhusiono ulikuwa mzuri vipi darasani, ndio maana mawakili wengi wazuri, wamepata pass tuu kama kina Mkono, na vile vichwa haswa vya sheria, vyenye Ist Class, kama kina Prof. Kabudi, huishia kwenye chaki ubaoni, na wakisimama mahakamani, ndio kama vile "amicus curiae", yaani friends of the court!.

Pia naomba msiwashangao, waandishi kumshobokea kijana wa Mzee, big names, makes news as well as prominance makes news, kijana ana both, silver spoon from 1st familiy, his own merit kwenye UV-CCM, sasa personal achievement as a member of the Bar from his own brain. Kati ya degree za kupewa pale UD, LL.B haipo, kila aliyesoma LL.B na kumaliza ni mwanasheria, ila sio kila aliyesoma LL.B na kuhitimu ni wakili.

Kwa hili la uwakili jamani, hongera zake mpeni!.

Unajisifia kudisco, wewe mzima kweli???
 
Pasco,

Nimekuelewa, kwenye ukilaza, hons, wakina nani mimi simo nilitaka tu uweke mistari sawa. Ukimwambia mtu ulidisco the ukamaliza kwa 2nd upper bado utakuwa umeacha maswali.

Kule kwa engineers kuna namna ya kupata professional credits, nahisi you must have 3 years field work experience.. Vipi law inakuwaje wakuu?
 
Unajisifia kudisco, wewe mzima kweli???
M-bongotz, nilikuuliza, kukubali udhaifu/mapungufu ndio kujisifia?. Mambo mengine ni kuwa na guts to speak nothing, but the truth no matter what. Inawewzekana kuna wengine walio disco chuo kama mimi, ila kwa vile ni siri ambazo wamezihifadhi ndani ya mioyo yao, then "wanajiplease, bora mimi sijadisco".

Kwa hizi zama za ukweli, na uwazi, see through crystal clear transparency inahitajika sana ili tuweze kuona mbele/mbali with nothing to hide.
Ila pia kama binadamu, tunamadhaifu mengi, inawezekama kabisa kukubali udhaifu nako ni udhaifu na sio ushujaa, in this case, nakiri, mimi nitakuwa sio mzima!
 
Pasco,

Nimekuelewa, kwenye ukilaza, hons, wakina nani mimi simo nilitaka tu uweke mistari sawa. Ukimwambia mtu ulidisco the ukamaliza kwa 2nd upper bado utakuwa umeacha maswali.

Kule kwa engineers kuna namna ya kupata professional credits, nahisi you must have 3 years field work experience.. Vipi law inakuwaje wakuu?
Kwa sheria kuingia kwenye professional, there was only one way, kupractise kwa kipindi fulani huku umepetition kwa CJ, ukipigwa interview, ukifaulu, ndio unaapishwa kuwa wakili. Huu ni utaratibu wa zamani, kwa hawa graduates wote wapya, lazima wapite law school kwa mwaka mmoja, halafu wanaukwaa uwakili straight forward, japo tangu hiyo law school imeanza, huu ni mwaka wa nne, na sijabahatika kuwasikia hao mawakili wa law school, au labda ndio wale wajuzi.
 
pasco naomba kukuuliza
mimi sijui sheria za mlimani zikoje
je maksi za mwaka wa pili si zinajumlishwa na mwaka wa tattu ili kupata final grade
 
Kwani vigezo vya kumteua mtu kuwa wakili wa kitegemea ni nini?

Kitu kingine watanzania wenzangu tuache ku poliiliticise kila kitu mwishowe tukakuwa hatumaa maana tunawalaumu watu kuingiza siasa kwenye mambo ya singi wakati sisi hata kutambua thread hii iwekwe kwenye forum gani tunashindwa .

kwenye hii thread nadhani hoja kubwa ingekuwa ni kuangalia kama mfumo wetu wa sheria utamwezesha na kumdhibiti Ridhiwan kuwa wakili mzuri bila ya kuathiriwa na makandokando ya siasa chafu za kifisadi. Kwa hili la Ridhiwani sina tatizo kwa yeye kuwa wakili lakini ni mfumo ndiyo nina tatizo nao.
TUACHE SIASA KWENYE KILA JAMBO!!
 
,
Kwa LL.B ya UD ninavyoijua mimi, its either you earn it, or not, hakuna magumashi, ndio maana nadhani tunaelekea miaka 15 au 20 hakuna 1st Class pale, huku Mzumbe na Tumaini na Open ni ma 1st ya kumwaga.

Msisitizo tena na bold kabisa, SIO KILA ANAE DISCO NI KILAZA!. ZIKO TECHNICAL DISCO KIBAO TUU NA ZINAPANGULIWA!

Hizo ni sifa za miaka ile ya University. Sasa hivi ni 'Chuo Kikuu' sawa na kile cha Magereza na polisi Kurasini. Kumbuka Vijana wa LL.B walio disco Masters kule Canada na komenti ya Mungai kwamba UD mambo ni mabaya ikaleta ugomvi na VC Luhanga.
 
Taaluma rahisi kabisa hapa duniani ni pamoja na ukahaba, uandishi wa habari na sheria. Hongera Ridhiwani. Kumbe ungeweza lipi sasa.

DUUUU! we ni kiboko! Kama huna PhD naomba nikutunukie U-Doctorate wa JF. Mbona Kikwete kapewa?
 
pasco naomba kukuuliza
mimi sijui sheria za mlimani zikoje
je maksi za mwaka wa pili si zinajumlishwa na mwaka wa tattu ili kupata final grade
.
Kwa zamani hizo nilizosoma mimi, ni marks za mwaka wa kwanza tuu ndio hazimumlishwi kwenye final score, kuanzia mwaka wa pili mpaka final, zina count.

Japo sielewi sababu za kutojumlisha mwaka wa kwanza, kwa maoni yangu binafsi, UD iliiparamia system ya kutoa degree ya LL.B kwa miaka 4 huku academic mechanisim nyingine zimesetiwa kimiaka 3, ndio maana Tumaini na Mzumbe LL.B zao ni miaka 3 tuu.
 
Hizo ni sifa za miaka ile ya University. Sasa hivi ni 'Chuo Kikuu' sawa na kile cha Magereza na polisi Kurasini. Kumbuka Vijana wa LL.B walio disco Masters kule Canada na komenti ya Mungai kwamba UD mambo ni mabaya ikaleta ugomvi na VC Luhanga.
Muchunguzi, kama hao vijana waliodisco Canada, walipiga LL.B ya UD, then, walidisco kwa mengine huko Canada na sio kwa udhaifu wa msingi walioupata pale UD.

Kwa Tanzania, ni LL.B ya UD tuu ndio mlima, za Mzumbe, Tumaini na OUT ni miteremko, sasa kama hao vijana waliweza kupanda huo mlima pale UD, halafu wakaenda kwenye mteremko Canada na wakashindwa hata kuteremka!, haya yatakuwa ni mengine tuu.

Naomba msilinganishe UD ile ya enzi zile ikiadmit wanafunzi 60 tuu wa sheria, tena 1st Class za nguvu, na UD hii ya sasa inayoingiza wanafunzi 300, na miongoni mwao, sifa za kujiunga ni uwezo wa kulipia!.

Pamoja na matatizo hayo yote ya Kitivo cha Sheria pale Mlimani, bado wahitimu wa LL.B ya UD ambao wameisoma sheria for the love of it, wanaibuka na kuwa a success story, ila kuna wale wanaiosoma sheria ili kupata ajira yenye maslahi manono, ajira wanazipata na maslahi yake manono, practice zao za sheria, huishia kwenye makabrasha kama reseach za Chuo zinavyoishia pale maktaba.
 
Taaluma rahisi kabisa hapa duniani ni pamoja na ukahaba, uandishi wa habari na sheria. Hongera Ridhiwani. Kumbe ungeweza lipi sasa.
WildCard, kuifanisha taaluma ya sheria na ukahaba, sio kuitendea haki hata kidogo, kwa ukahaba unasomewa?. Ama unamaanisha masomo ya sheria ndio marahizi kuliko taaluma nyingine zote, hii sio kweli.

Kwa vile taaluma ya uandishi wa habari imevamiwa na kila Tom, Dick and Harry, yaani kila mtu anaweza kuwa mwandishi wa habari, lakini sio kila mtu anaweza kuwa Mwanasheria.

Lazima tuukubali ukweli kuwa taaluma ya sheria, ni moja kati ya taaluma chache ambazo zinakata across everything, ukiondoa technical professions, ukihitimu sheria, you can be anyone you wish to be, you can be a political leader kama Mizengo Pinda, you can be mkurugenzi wa makampuni makubwa, ka Anold Kileo wa TBL, au unaweza kuwa wakili tuu kama kina Nimrod Mkono.

Advantage ya ziada kwa taaluma ya sheria ni ule uwezo wa mwanasheria, kuwa mtu mwingine yoyote na kufanya kazi ya taaluma nyingine yoyote, lakini watu wenye taaluma nyingine zozote, hawawezi kuwa wanasheria, bila LL.B. Natia msisitizo kwenye LL.B kwa sababu mtu mwenye taaluma nyingine yoyote, anaweza kufanya LL.M lakini bado hawezi kuwa wakili bila LL.B.
 
,
Kwa LL.B ya UD ninavyoijua mimi, its either you earn it, or not, hakuna magumashi, ndio maana nadhani tunaelekea miaka 15 au 20 hakuna 1st Class pale, huku Mzumbe na Tumaini na Open ni ma 1st ya kumwaga.

Msisitizo tena na bold kabisa, SIO KILA ANAE DISCO NI KILAZA!. ZIKO TECHNICAL DISCO KIBAO TUU NA ZINAPANGULIWA!

Pasco yalikukuta nini? Pole kaka ila usijali kubali matokeo jipange upya for if you are not fit in one sphere you fit to the other...Siyo lazima wote tufanye mambo yale yale kwa mazoea. Kibaya ni pale ambapo its clear you dont fit you try to force yourself in; ndo maana hatuendelei kwani we most of the time deny our true identity and try to wear other people's identities/talents.

Inawezekana usiwe mzuri kwenye academics, ukawa practitioner mzuri tu kuliko academician then uka put into practice academic materials; waweza usiwe gud politician ukawa policy analyst mzuri tu kuwasaidia politicians; waweza usiwe advocate lakini ukawa hakimu mzuri tu and etc etc

We should learn to respect every humanbeing under the sun for they are God's workmanship wonderfuly created and are brought for a specific purpose; na unapomzarau au kumkwamisha kufikia level yake then you deny yourself of the help/support he/she is assigned to give to you first; thats why you happen to be associated in one way or another and to the entire community that personality is belonging.

Tanzania tunakosa madaktari, ma engineer; wafagizi wazuri kwasababu hatufanyi kile tulichoitwa kufanya. I am the living testmony of this; since my child hood nilipenda kuwa mwalimu na nilipenda to teach something in development by then sikujua what it meant by economics. Lakini in form four waalimu wangu walichana form zangu kwakua niliweka EGM as my first combination they forced me to go for PCB why kwasababu nilikua nafaulu science lakini walisahau pia nilikuwa nikifaulu historia, geography na mathematics. Then there after I was so much depressed that the whole of form five was sick; nabaada ya A-level the same thing was to happen this time with parents thats when I refused and choosed to do things I wanted slowly taking my self to the direction I wanted....Believe me it took me more years to realise my dream other than what was supposed to kwa kulazimishwa ku fit in what I did not believe in; kwa sababu madaktari wanachukuliwa kuwa watu wenye akili so kila mtoto mwenye akili awe daktari na mjinga awe mwalimu what a bad attitude!

And this attitude ya waalimu kuwa watu waliofeli ndiyo iliyokuwa wimbo wa my relatives and everybody who was close to me...I guess I would have made a best teacher kama siyo hiyo attitude ya ku associate waalimu na failing!
 
WildCard, kuifanisha taaluma ya sheria na ukahaba, sio kuitendea haki hata kidogo, kwa ukahaba unasomewa?. Ama unamaanisha masomo ya sheria ndio marahizi kuliko taaluma nyingine zote, hii sio kweli.

Kwa vile taaluma ya uandishi wa habari imevamiwa na kila Tom, Dick and Harry, yaani kila mtu anaweza kuwa mwandishi wa habari, lakini sio kila mtu anaweza kuwa Mwanasheria.

Lazima tuukubali ukweli kuwa taaluma ya sheria, ni moja kati ya taaluma chache ambazo zinakata across everything, ukiondoa technical professions, ukihitimu sheria, you can be anyone you wish to be, you can be a political leader kama Mizengo Pinda, you can be mkurugenzi wa makampuni makubwa, ka Anold Kileo wa TBL, au unaweza kuwa wakili tuu kama kina Nimrod Mkono.

Advantage ya ziada kwa taaluma ya sheria ni ule uwezo wa mwanasheria, kuwa mtu mwingine yoyote na kufanya kazi ya taaluma nyingine yoyote, lakini watu wenye taaluma nyingine zozote, hawawezi kuwa wanasheria, bila LL.B. Natia msisitizo kwenye LL.B kwa sababu mtu mwenye taaluma nyingine yoyote, anaweza kufanya LL.M lakini bado hawezi kuwa wakili bila LL.B.

Pasco,
Sikatai unachokiongea hapa. Nifahamishe zaidi yafuatayo:
-Kwa nini taaluma hizi hadi leo hazina boards za kitaaluma kama vile NBAA ya wahasibu, ERB ya wahandisi,...
-Kwa nini mpangilio wa vyeo na madaraka haufati elimu ya mtu? Kwa mfano, AG au CJ alipaswa kuwa PhD holder ambao Tanzania hii tunao wengi tu.
Kutoa mfano wa watu kama Arnold Kileo haututendei haki Watanzania. TBL sasa hivi iko mikononi mwa nani? Aliisimamia hadi ikauzwa kwa bei ya kutupa kama NBC yetu kisha naye akajigawia hisa. Nadhani pia unaelewa mikataba mbalimbali tuliosaini kama NCHI ilikotufikisha.
 
Back
Top Bottom