Kumbe Tanzania hatukufanya makosa ya kiufundi ya kuwa na wabunge na pia hata Naibu Spika ambao ni wenye asili ya watu wa Asia. Na tena kumbe siku moja inaweza ikatokea uwezekano wa kumpata kiongozi wa juu wa muhimili mmoja wa mchi ambaye atakuwa na asili ya watu wa Asia.
Hali ikizidi kuwa ngumu kiuchumi, kisiasa na kijamii, na Watanzania weusi wakizidi kuboronga katika mambo ya menejimenti na utawala, basi ifike wakati sasa tuzidi kuwaamini watu hawa. Kama Watanzania wenzetu hawa wenye asili ya Asia wametuzidi maarifa katika mikakati thabiti ya kuendesha taasisi binafsi zilizo imara na makampuni makubwa kwa mafanikio makubwa, basi tusisite kuwaamini kuongoza nafasi mbalimbali za juu zilizopo katika mihimili mitatu ya dola.