Hongera Samia kuanza kampeni kwa kishindo lakini rekebisha mahusiano yako na taasisi hii

J_Okay

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
319
Reaction score
196
NA J_Okay

Hatimaye kampeni zimeanza, huku Rais Samia Suluhu Hassan akitafuta miaka mitano mingine ya kukamilisha kazi yake. Ionekanavyo, Rais Samia atapita kwa urahisi, ingawa idadi ya wapiga kura inaweza kuwa ndogo. Ukweli usemwe, ukizingatia namna alivyoingia madarakani kwa bahati tu, na akiwa ni mwanamke alichofanya katika miaka minne yake ya mwanzo ni juu ya matarajio.

Tishio lipo lakini nguvu ya Chadema si hoja za kisiasa bali inatokana sehemu ndogo ya taasisi nyeti iliyojeruhiwa na ambayo kwa tathmini yangu serikali yoyote inayotamani ifanikiwe yafaa ichunge namna inavyohusiana nayo. Taasisi hiyo ni kanisa.

Usinambie ufisadi, kukosekana utawala bora, sera mbaya za kiuchumi za Rais Samia zimechosha ndio sababu ya nguvu ya Chadema kwa sababu nitakuuliza: Lini huko nyuma hali ilikuwa boa kuliko sasa? Kiuhalisia, mafanikio ya awamu hii ni makubwa kuliko awamu nyingi za huko nyuma,

Kanisa ni moja ya taasisi muhimu za kidini Tanzania ambayo umuhimu wake si tu katika kuwapa matumaini ya kulala pema poponi katika maisha ya milele huko mbinguni lakini pia kanisa ni muhimu katika kutetea maslahi ya wanyonge mbele ya Serikali.

Nadiriki kusema kanisa linaifanya kazi ya kuwasemea wanyonge kwa ufanisi mkubwa. Kama vilivyo vyombo vya habari na taasisi za kiraia, kanisa nalo linafanya jukumu muhimu la ukosoaji (oversight role). Na pengine ukilinganisha na hizo taasisi nyingine, kanisa lina ushawishi zaidi na hivyo sauti yake inapopazwa kwa sauti ya juu huweza hata hutikisa serikali hapa Tanzania.

Kutokana na ushawishi wake, tawala zote zimekuwa makini katika uhusiano wake na kanisa. Rais Samia naye amejitahidi, lakini ana mengi ya kuboresha katika eneo hili. Matukio matatu yaliyohusisha makanisa na ambayo yalimsumbua yananijia akilini harakaharaka.

Masuala hayo matatu yalihusisha kwanza, suala la DP World ambalo lilitikisa utawala wake baada ya kanisa kuweka msimamo wa kupinga mkataba za zabuni ya kuendesha bandari ambao Serikali iliingia na kampuni hiyo. Kisha likaja suala la kushambuliwa kwa Padri Dkt.Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) na tatu Sakata la kufungwa kwa kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima.

Sisemi kuwa serikali ilikuwa katika msimamo wa makosa katika masuala hayo matatu lakini pengine ingeweza kuyashughulikia kwa hekima na busara zaidi kwa kuonesha uvumilivu. Kwa mfano, kutokana na unyeti wa masuala ya dini na hususan kanisa, nina hakika suala la kufungiwa kanisa la Gwajima lingeweza kuepukwa, lakini pia suala la kupigwa kwa Kitime lingeweza kushughulikiwa vema zaidi kwa kuhakikisha wahalifu wanatafutwa ili kuiondolea serikali lawama.

Ikumbukwe kuwa tayari msimamo wa Kitime ulishaonekana kuwa mkali, pengine, kuliko hata ule wa kanisa lake kwa hiyo ilikuwa rahisi watu kuhisi amelengwa binafsi. Na kwa kuwa padri huyo alikuwa akiwakilisha kanisa (pamoja na misimamo yake mikali) hakuna namna shambulio dhidi yake lisingeonekana kuwa ni shambulio dhidi ya kanisa. Ulikuwa ni wajibu wa serikali kujisafisha.

Ushauri kuntu

Kwa faida ya Rais Samia ya sasa na miaka yote iliyobaki ya utawala wake, kama nikiambiwa nimshauri nitamwambia kaa vizuri na kanisa.

Ni ngumu sana utawala wa CCM kudondoka lakini kama ipo taasisi moja tishio inayoweza kutikisa utawala wowote hapa Tanzania ni kanisa kwa sababu tofauti na misikiti, makanisa yako kitaasisi na ni rahisi sana msimamo uliowekwa na uongozi ngazi ya taifa kufikishwa kwa waumini na kuwageuza nyoyo zao dhidi ya serikali.

Wakati kila kanisa lina mtiririko wa uongozi (hierachy) unaowezesha taasisi kuzungumza kwa sauti moja, ukweli mwingine ni kuwa makanisa yenyewe pia yanaongea na hivyo kwa jambo lenye maslahi kwao wote ni rahisi kukubaliana. Jambo jingine la muhimu kuzingatia ni kuwa yanapokuja mambo ya imani, hasa kwa wakristo, siasa inasubiri, na hasa ikiwa ni jambo nyeti linalotishia ustawi wa Ukristo.

Katika Uislamu, hali haiko hivyo. Kwanza, ni asilimia chache sana ya Waislamu wenye mafungamano na misikiti, ukiacha nyakati za Ramadhan. Pia, kila msikiti unaouona mambo yake huishia hapo – hakuna muunganiko na taasisi kubwa ambayo kwake msikiti unawajibika ngazi za juu hadi taifani. Hii hufanya ngumu kuweka msimamo. Kwa upande mwingine, kama kuna dini ambayo, wengi wa waumini wake wanaamini katika utenganisho wa siasa na dini ni Waislamu.

Yote kwa yote, kanisa lina nguvu kubwa mno kiasi kwamba mwanasiasa mwerevu anayejali mustakabali wake hawezi kulikorofisha.

Ni kwa msingi huu ndio natoa nasaha kwa Rais Samia, akae vizuri na kanisa. Asili yake ya Uislamu, Uzanzibar inamnyima zaidi faida mbele ya kanisa ukilinganisha na ilivyokuwa kwa mwenda zake Rais aliyepita, John Magufuli. Yeye kwa sababu analijua kanisa ilikuwa ni rahisi kushughulika nalo, kama ambavyo Samia naye Waislamu hawampi shida.
 
Kuna taasisi

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

Sakata la kufungwa kwa kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima limechukua sura mpya baada ya vyombo vya usalama kuzingira kanisa hilo.

Vyombo vya ulinzi na usalama vilizingira kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima. Kanisa hilo limezingirwa ikiwa ni siku moja baada ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emanuel Kihampa, kulifungia kanisa hilo kwa madai ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa kwa nia ya kuichonganisha serikali na wananchi.

Hata hivyo, wakati usahihi wa barua hiyo ukiendelea kutafutwa, polisi walikwenda kulizingira kanisa hilo. Askofu Gwajima alirekodi video fupi na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii ikieleza hali ilivyokuwa katika kanisa hilo usiku wa jana:

"Ni saa tano na robo usiku, na hawa maaskofu unaowana wamekuja hapa usiku huu baada ya kusikia taharuki, Kwamba tunaona hapo polisi wamekuja kuzunguka kanisa la ufufuo na uzima, hapa Ubungo," alisema askofu Gwajima.
Kuna siku yatajulikana yote
 
Back
Top Bottom