Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KwakweliHongera pia Binti.
Hii ndio maana halisi ya sikio halizidi kichwa
This was strategic.
Ili kuzidi kupaisha umaarufu wa Kigalula. Na kuendeleza porojo za wavaa makobazi na Hamas.
Dah mjuba😀😂, uta sikia kwanini nampenda Lee 😀😂Genta ana shobo tu. Nina uhakika kawekwa ignore list.
Faiza hana lolote kabebwa na pro palestinians.
Hii ndiyo sababu mpaka leo maendeleo yetu ya mwendo wa konokono, kama kizazi hiki ndiyo kingekuwa kipindi cha ukoloni ni hakika mpk leo sisi ndiyo tungebaki tunatawaliwa mpk leo barani Afrika
Ajuza ndiye kashinda.😂😂😂
Matokeo yalikuwa wazi.Mnauhakika kura hamjachanganya ID...?
Eti taarifa hii imeshamletea mtu stress😂😂😂
Sijawahi hata kuwaza kitu cha namna hii!
Danga la toka awamu ya kwanza ya Mwl leo liwe Miss wa kitu fulani?hizo kura aliyempigia nani kwanza?
Hongera sana Miss JF
Huu uchaguzi ni batili. Tunaitaka Tume ya Uchaguzi ya JamiiForums itangaze uchaguzi upya na waangalizi wa Kimataifa wakaribishwe kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi!
Basi ikawe kheli kwake mlimbwende wetu🌹Matokeo yalikuwa wazi.
Kila aliyempigia mhusika alionekana dhahiri
Mimi nilivyoshinda Mwanachama Bora Jukwaa la Michezo ( Sports ) JamiiForums Msimu wa mwaka 2022/2023 huku nikiwaacha mbali mno Wapinzani wangu nilipata Zawadi ya Hela na Kitu kingine cha Kihistoria na Kumbukumbu Kwangu je, huyu Mshindi wako Yeye anapata / atapata nini labda?Kheri ya Mwaka Mpya Wakuu!
Kama mjuavyo dunia inabadilika. Na Uwepo wa JF ni moja ya vithibitisho hivyo kuwa Dunia ya sasa imebadilika.
Hatujuani kutokana na wengi kutumia Anonymous ID lakini hiyo haimaanishi kuwa hatujuani kifikra, kimawazo, kiitikadi, kiimani, kihisia na mambo mengineyo.
JF utaficha Physical body yako lakini hiyo haimaanishi utaficha Inner body. Kwa Sisi Watibeli. Inner Body ndio ina Matter kuliko Physical body.
Shindano la U-miss JF lililenga zaidi kwenye Inner body Kwa Sababu kama ni Physical body wengi hatujuani humu.
Mvuto wa ndani kabisa ndio uliopelekea Watu kupiga kura pasipo kujua Physical body ya wahusika.
Huenda mhusika akawa ni mzee kiumri katika Physical body lakini umbo la ndani akawa kigoli mwenye umbo la mdoli asiye huna.
Huenda Physical body ya wagombea zimechoshwa na shida na asili ya ulimwengu, uzee na magonjwa vimevikongoroa na kuvifanya viungo vyao kuwa dhaifu na vilivyokosa mvuto kama wapiga kura wengine walivyotoa maoni na mtazamo wao lakini ukweli utabaki kuwa upo mvuto wa ndani kabisa ambao unaweza kuvutia Watu na kutofautisha mvuto baina ya mtu mmoja na mwingine.
FaizaFoxy kwa mwaka huu ndiye Mwanamke mrembo zaidi ndani ya JF, bila kujali wapo watakaokataa au watakaokubali lakini kama mlivyoona kura ndio zimeeleza hayo.
Tofauti ya kura tano tuu zimemuibua FaizaFoxy kama kigoli na mrembo ndani ya JF.
Hongera Sana Miss JF FaizaFoxy kwa mwaka 2023/2024.
Nawapongeza Washiriki wengine hasa mshindani wake aliyeshika nafasi ya pili Leejay49
Nawapongeza pia Wapiga kura kwa kutoa muda na maoni yenu kuhusu Mrembo mnayevutiwa naye.
Nampongeza Mpiga Kampeni GENTAMYCINE AKA Popoma kwa kufanya kazi kubwa ya kupiga Kampeni kwa mgombea wake. Bila shaka kushika ya pili kwa Leejay49 kumechagizwa na Popoma.
Hata hivyo jitihada zao zimegonga mwamba kwa kisiki cha mpingo, Mama wa Hamas, Bibi Kamusi, mwalimu wa usiku, Ostadhat mwenye kupenda dini yake FaizaFoxy
Kwa wale walioona jambo hili lilikuwa ni ujinga pia tunawashukuru kwa muda na mtazamo wao.
Kuwataja hapa Washindani hao ni zawadi tosha. Hakuna jambo zuri kwenye maisha kama appreciation na Recognition.
Wale ambao hawajawahi hata kufanyiwa appreciation na Recognition hata na Wake/waume zao, wazazi wao, watoto wao au marafiki zao hawawezi kuelewa kitu hapa. Zaidi nawapa pole.
Nawatakia Mwaka mpya Mwema.
Yeyote ambaye nimemkwaza kwa namna yoyote ile anisamehe. Mimi sinaga msamaha kwa sababu hakuna anayenikosea humu.
Kauli mbiu ya mwaka 2024 " Adui atanyooka"
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ety mrembo wa haja[emoji16][emoji16]Hongera kwa dada yangu FaizaFoxy.
Binafsi ni miongoni mwa waliompigia kura licha ya kupishana mitazamo.
Namfahamu Faiza ni mrembo chotara mmoja wa haja licha ya umri kumtupa mkono.
FaizaFoxy, umepata habari Mhando kumbe alifariki miezi kadhaa nyuma mwaka huu na mwili uliletwa toka US. Mara ya mwisho uliuliza nikakueleza yu Canada. Alale pema peponi Mhando!