Hongera sana homeboy kwa kumleta Flora (Mbasha) Henry nyumbani

Status
Not open for further replies.
Alafu wewe ulofuta futa kadi unatuharibia kadi, kwnai ulitumwa kuileta huku? na kwa taarifa yako sasa arusi itakua Mwanza kama sikosei kanisa la AIC Makongoro ndani ya weekend mojawapo ya mwezi April, we unafuta futaaaaaaaa mpyuuuuuuuu
Ili kanisa la AIC si ndio liko magomeni pale? Hili ni kanisa la watu wa Mwanza watu wengi wanalitumia kutakatisha ndoa batili.

Hili kanisa kama lingekuwa ni benki basi BOT wangeshalifunga siku nyingi tu.

Kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele napoteza imani kabisa na kanisa na ninejiridhisha hakuna dini ni Man made project tu.

Ukiwa na Yesu atosha hizi dini ni NGO za watu na ndio sababu dini zote na madhehebu yote watapondana na kashfa za kila namna lakini kwenye swala la sadaka hakuna anayepinga sadaka.

Akili kichwani mwako.
 
Watu wana mioyo migumu unaanzaje kumuoa mke wa mwenzako ilihali bado yuko hai
.
.
Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
 
ngoja jopo la wachungaji waje na majibu
Marko 10-12

1 Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.

2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.

3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?

4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.

5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.

6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;

8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.

11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;

12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini
 
Nafkri n mtu kutojitambua na
Kutoheshim kiapo ulichoapa
Pale kanisan mbele ya mungu wako

Watu wana mioyo migumu unaanzaje kumuoa mke wa mwenzako ilihali bado yuko hai
.
.
Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
Unatumia nguvu nyingi sana kwenye hii post. Kaweke pingamizi mkuu
 
Ni kweli zogo (controversy) au hekaheka kubwa inayowagawa watu katika makundi mawili kuhusu talaka inapatikana katika injili ya Mathayo 5:32 na 19:9
Kumbuka Injili ya Luka na Marko pia imeripoti tukio la Mathayo 19:9 Yesu alipotegwa swali na Mafarisayo isipokuwa ni Mathayo peke yake ameandika kuhusu exception ya kutoa talaka ambayo ni kosa la uasherati (tutaangalia baadae kwa nini ni mathayo peke yake ameripoti hivyo).

Kabla ya kufika huko ni Muhimu sana kufahamu mazingira (geography) iliyopelekea Yesu kuulizwa swali na Mafarisayo.
Tukumbuke kwamba Yesu alikuwa Galilaya na alikuwa amemaliza huduma yake na sasa alikuwa anasafiri kupitia eneo la Perea ili kurudi Yerusalemu kwa ajili ya pasaka (yaani kifo chake).

Mafarisayo waligundua kiwamba Yesu atapita hilo eneo ambalo kwa wakati huo lilikuwa chini ya himaya ya Herodi.
Hivyo mafarisayo walijua ni wakati muafaka wa kumuuliza swali (trick question) ili ajichanganye na wapate sababu ya kumuua.
(kumbuka mafarisayo walikuwa wanamfafuta sana Yesu wamuue ila walikosa sababu au shitaka Mathayo 12:14, Marko 3:6)
Kwa hiyo mafarisayo walimuuliza Yesu swali ambalo lengo ni kumtega yeye (test) na si kutaka kujua.

Kumbuka miaka 2 iliyopita Yohana mbatizaji ambaye alimtangulia Yesu alikuwa amefungwa Jela kwa sababu aliongelea suala la talaka ya Herode Antipas ambaye alioa mke wa mdogo wake Filipo ambaye mke wake alitoa talaka kwa mume wake Filipo na kwenda kuolewa na Herodi Antipas (kaka mtu) Soma Mathayo 14:1-12.

Yohana mbatizaji hakubabaika au kujisikia vibaya kumkemea Herodi na dhambi yake hata kama ni ikulu (Math 14:4) matokeo yake akawa arrested na kutupwa jela na baadae kukatwa kichwa.

Kwa kuwa Yesu alikuwa anapita maeneo ambayo ni himaya ya herodi Antipas, mafarisayo walijua fika kwamba Yesu atajichanganya tu na jibu la swali watakaloulizwa na atajimaliza kwa kumtaja Herode na dhambi yake ya kuoa mke wa mdogo wake na kama Yohana mbatizaji kwa kutamka tu aliuawa Yesu Je ambaye anapita kwenye himaya yake?

Swali aliloulizwa Yesu lilikuwa:
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’

Kumbuka wakati Yesu yupo duniani talaka ilikuwa inakubalika kutokana na Musa alivyoamuru hata hivyo kulikuwa na gumzo na utata wa sababu ipi hasa mume anaweza kutoa talaka kwa mke au sababu ipi hasa inaweza kupelekea mume kutoa talaka kwa mke wake na kumbuka pia wayahudi walikuwa hawaruhusu mwanamke kutoa talaka bali mwanaume tu.

Ndipo kukawa na makundi matatu yanayopingana

KUNDI LA KWANZA – SHAMMAI
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ilikuwa ni uzinzi (adultery)

KUNDI LA PILI – HILLEL
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ni pale mke akipika chakula kisichoiiva au kibaya au ovyo.

KUNDI LA TATU – RABBI
Wao walikubalkiana kwamba hata mume akikutana na mwanamke mzuri zaidi ya Yule anaye nyumbani basi anaweza kutoa talaka

Sasa swali kwa Yesu lilikuwa wewe upo upande gani?
SHAMMAI, HILLEL AU RABBI?

Yesu alifahamu fika mioyo ya mafarisayo inawaza kitu gani na akawajibu kwa swali (counter attack) kwa kuwauliza tangu mwanzo Mungu alifanya kitu gani kwa ajili ya mke na mume.

Mafarisayo wakajikuta swali lao limekosewa na kwamba wamekosa point kwani wao walitaka ajibu Kumbukumbu la Torati 24:1-4) na Yeye akajibu Mwanzo 2:24.

Ikabidi wamrukie kwa swali kuhusu Musa kuruhusu talaka ndipo wakajibiwa kwamba Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kukataa kwao design ya ndoa tangu mwanzo na ndipo Yesu akazusha mambo 4 muhimu kabisa

JAMBO LA KWANZA
Hapo mwanzo Mungu aliumuumba mwanaume mmoja kwa ajili ya mwanamke mmoja, kama angetaka Adamu awe na wanawake wengi basi angewaumba akina Sandra, Joan, Jane, Linda wakutosha na si Eva peke yake.
(mwanzo 1:27, 5:2, Marko 10:16)

JAMBO LA PILI
Yesu anatia mkazo kwamba ndoa ndicho kifungo (strongest bond) duniani hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa ni muhimu sana anayehusika kufahamu kwamba anaingia kwenye kitu ambacho huwezi kutoka labda kifo kitokee kati ya wawili.
(Mwanzo 2:24, Marko 10:7)

JAMBO LA TATU
Katika ndoa wawili huwa mtu mmoja, mwili mmoja (one flesh)
(Mwanzo 2:24, Marko 10:8)

JAMBO LA NNE
Yesu alithibitisha kwamba Mungu ndiye huwaunganisha wawili wanaooana na kwamba kile Mungu amekitenganisha binadamu asikitenganishe.

Hivyo swali la mafarisayo
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
Jibu la Yesu ni HAPANA KUBWA
Na kwamba Yesu hakuwa kwenye kundi lolote iwe SHAMMAI AU HILLEL AU RABBI.

Yesu alielezea kudumu (permanency) na kutovunjika (inviolability) ya ndoa hadi wanafunzi wakaendelea kumuuliza jioni yake huku wakipendeleza kwamba kama masuala ya ndoa ni hivyo basi ni busara sana mwanaume asioe kabisa.
 
Makanisa ya siku hizi bana
Anaolewaje wakati mumewe mzima [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

SIKU HIZI KILA ANAYEJUA KUFUNGUA BIBLIA ANA KANISA HENCE USISHANGAE WAKAFUNGA NDOA VIZURI KABISA.

KWENYE MAKANISA HAYA YA MALBORO.
 
Hivi kweli mbasha alimfanyia nini huyu mwanamke mpaka hakutaka kumsamehe?
Ama kweli ndoa zina mambo kweli!
Nadhani hata Flora kuna kitu pia alimfanyia mumewe maana kuna kipindi walisamehana lakini ilikuwa trick ya mwanamume ili lile suala liondolewe mahakamani na kweli liliondolewa kilichofuata mwanamume nae akang'atuka kiaina. Wakati mwingine inaweza ikawa kutokana na haya maisha ya mwanamume unaishi kwa kipaji cha mwanamke alafu unashindwa kujiongeza kwa kuonyesha ubaba maana inaonekana mshikaji alikuwa kama supporter wa kazi ya mkewe na inapotekea changamoto kwenye ndoa alafu mwanamke ndo kama anakubeba huwa wanapata moto
 
That bravoo Roger
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…