Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Stars imeifunga Zambia ikiwa nyumbani kwake, narudia nyumbani kwake.Binafsi, sikuwa na shaka na uwezo wa makocha hao isipokuwa shaka yangu kubwa ilikuwa kwa wachezaji, kwamba wachezaji tuliokuwa nao hasa wale walioanza sikudhania kabisa baadhi yao kama wanaweza kupambana kiasi kile hasa kutokana na namna nilivyokuwa nawaona katika ligi ya ndani.
Ila lazima tukubali watanzania kuwa Ligi yetu imesaidia sana kuwakomaza wachezaji na kuwapa confidence, striker kama Wazir Junior japokuwa hakucheza vizuri lakini alionekana kuwa na afadhali kule mbele, kwa sababu alikuwa anajiona anaweza.Waziri Junior kama aliweza kupambana na madefender wakubwa hapa Africa kama Che Malone Fondoh, Inonga Baka, yule beki wa Colombia anayecheza Azam, Ibrahim Bacca kitasa cha maana kabisa hiki kikinikumbusha enzi za Seif Bausi pale Small Simba, hakika aliona hana tofauti na alipokuwa akicheza ligi ya nyumbani.
Wachezaji kama akina Feitoto, Mudathiri, Shabalala, Bacca, Mwamnyeto wamecheza na washambuliaji wakubwa hapa Afrika na duniani hivyo hawakuona taabu kucheza na Zambia wala kumhofia mzungu mchovu Avram Grant.
Stars inahitaji marekebisho kidogo eneo la ushambuliaji ili kumaliza shughuli kabisa maana wakati mwingine unaweza kuwa na timu nzuri lakini kama huna strikers wazuri mbele, itakuwa kama unatwanga maji kwenye kinu.
Nimevutiwa sana na uwezo wa kipa Ally Salim, alikuwa hana wasiwasi kwa sababu aliona kama aliwahi kupangwa dhidi ya Al Ahly, Wydad vipi awaogope Zambia?
Lakini pia kubwa zaidi Stars hii naiona kama inajengwa upya, imeweka vijana wenye mbio sio kawaida, Balua, Sopu, Mzize hakika naiona timu ikisonga mbele.
Hongera sana Hemed Morroco kwa kazi nzuri, watu walikuwa wanasubiria Stars ifungwe wahamishie mjadala kwako lakini wamenoa.Kazi iko kwa Mo Dewji sasa na bodi yake ya wakurugenzi, wabaki au waondoke.
Umepata msaidizi mzuri sana Juma Mgunda.Ile sub ya Edwin Balua na Lawi ni ushauri wa Mgunda ule, kwa sababu Balua hakuwa anajulikana hadi Mgunda alipopewa Simba na kumuibua, sio kazi rahisi kumshauri kocha mkuu na akakubali ushauri.
Angekuwa kocha wa kigeni ambaye hawajui wachezaji vizuri ungesikia Himid Mao anacheza namba tatu, sijui Haji Mnoda namba mbili, sijui Feitoto namba tatu, wizi mtupu makocha wa kigeni.
PIA SOMA
- FT: Zambia 0-1 Tanzania | Kufuzu Kombe la Dunia | Levy Mwanawasa Stadium | 11/06/2024