Hongera sana Mbowe kwa msimamo wa kubaki CHADEMA. Tambua kuwa mpango wa kukuondoa ulikuwa kuua Chama. Nashkuru umegundua hilo

Hongera sana Mbowe kwa msimamo wa kubaki CHADEMA. Tambua kuwa mpango wa kukuondoa ulikuwa kuua Chama. Nashkuru umegundua hilo

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Hongera sana Mh Mbowe kwa msimamo wa kiume wa kubaki CHADEMA, tambua kua mpango wa kukuondoa wewe ilikuwa kuua chama nashkuru umegundua hilo.

Mh Mbowe hongera sana ufahamu wako umefunguka kama nilivyokuombea.

Mh Mbowe mpango wa kukuondoa CHADEMA ilikua kuua chama kwasababu Lissu ni mharibifu
Amekuwa akiharibu Serikali ya CCM kwa muda mrefu bahati nzuri wakafanikiwa kumdhibiti sasa akaona arudi kwako.

Lissu ni mwanasiasa mzuri lakini tatizo lake ni mdomo mrefu pia ana asili ya kuharibu.

Hakuna maendeleo yeyote Lissu aliyopelekea watu wake wa Singida tangu apate ubunge zaidi ya kubwabwaja.

CCM wamechoka nae zigo limetupwa CHADEMA ifike mahali na ninyi mumchoke.
 
Ni suala la muda tu, CHADEMA inakufa kama vyama vingine mfu. CCM iendelee tu kutawala hadi ichakae
 
Basi na mpango wa kuitoa ccm madarakani ni wa kuua Nchi.

Mbowe kazingua,akiwa Rais je ataachia Nchi?

CDM mpaka hapa hali yetu mbaya.
 
Lissu hana busara, ni rahisi chama kuanguka kikiwa mikononi mwake.
Mbowe kugombea tena uenyekiti ni salama kwa chama zaidi
 
Lissu hana busara, ni rahisi chama kuanguka kikiwa mikononi mwake.
Mbowe kugombea tena uenyekiti ni salama kwa chama zaidi
Tatizo la Lissu ni mawenge hana utulivu haeleweki pia ana tatizo la kutoa siri jambo ambalo hata Jeshini halitakiwi
 
Basi na mpango wa kuitoa ccm madarakani ni wa kuua Nchi.

Mbowe kazingua,akiwa Rais je ataachia Nchi?

CDM mpaka hapa hali yetu mbaya.
Wala hazingui mkuu tatizo la Lissu ni mawenge ni mtu wa kutoa siri kitu ambacho ni kosa kubwa
 
Hivi TBC warushe Mkutano wa Mbowe Kwalengo la Kukifanya Chama kuwa ngangali!!
Hahaha Tanzania Yangu ina Vijana Vilaza sijapata kuona
 
Back
Top Bottom