Hongera sana mwanariadha Gabriel Geay na inabidi serikali ikuunge mkono

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Hii ndo maana halisi ya kurudisha kwa jamii. Kijana baada ya kufanikiwa kwenye mchezo wa riadha kaamua kurudi kijijini kwao na kujenga kambi ya kisasa ya mchezo wa riadha kisha kuwaweka kambini vijana wadogo wenye vipaji anaowahudumia kila kitu. Ila kanishangaza mno kwa uwekezaji anaoufanya anatarajia kutumia Tsh 400m tu. Ingekuwa ni baadhi ya watendaji wetu serikalini hiyo 400m ingeishia kwenye upembuzi yakinifu.

Ninaisihi serikali iguswe na hili jambo iweke hata bilioni moja kwenye mradi wa huyu kijana ili akamilishe kila kitu. Hii ndoto yake ni kubwa sana na ngumu mno kuikamilisha mwenyewe. Nina wasiwasi anaweza kwama katikati. Mama tafadhali msaidie huyu mzalendo hata bilioni 1.

View: https://www.instagram.com/share/reel/_rq_q8dpI
 
Kwani kwa Taifa Gesi hiyo siyo pesa ya mboga tu?
 
Hongera Geay,shirikisho la riadha kazi yao ni kutembeza bakuli tu
 
Mbona kama na Serikali ina mpanga wa kujenga kituo kikubwa na cha kisasa cha riadha hapo Babati
 
Kakumbuka alivo hustle kumake mpaka hapo, kaamua kuwarahisishia vijana, hongera kwake.
 
Back
Top Bottom