Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Katika sehemu ya pili ya Mayalla, ameuliza kuhusu Rais anakopata mamlaka yake ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano na mandamano. Nyie wenzangu mmesikia majibu hapo????
 
Kimsingi mayalla kauliza maswali muhimu siyo yule dada wa TBC ambaye moja ya maswali yake alimuuliza rais baada ya kazi vitu gani vingine anapenda. Rais mwenyewe alicheka akamjibu unataka niseme nakupenda wewe?
 
Mkuu kwahiyo unataka kusema yale ambayo rais hakuyazungumzia basi anayaacha pending si ndiyo?
Mana yote yapo ndani ya shughuli za sirikali
Kaka Magufuli yuko very clear amesema anatekeleza masuala ambayo yapo kwenye ilani, Serikali inaendeshwa kwa kuzingatia mipango yake ya mwaka hadi mwaka ambapo msingi wa mipango hii huakisi yale yaliyo kwenye ilani ya chama husika waliyoombea kura sasa issue ya Tido ukiachilia magufuli kutoiongelea katika Kampeni zake au hotuba zake hata kwenye ilani ya CCM sina hakika kama lipo hilo suala la katiba mpya. Ni ukweli ambao mchungu kuwa kwa Magufuli issue ya katiba tusahau
 

@mods Invisible kweli kabisa mmeunganisha huu uzi na huu wa Pasco.

Hii sasa mmechemsha, mbona topic nzuri kukaa yenyewr, si bora hata mngepeleka kwenye ule uliokua live.

Sasa kuunga mnasave kitu gani, anaongelea points nzuri nyie mnaunga kwa Pasco kabisaaaaaa.

Please tendendeni watu uhuru fulani, kuna threads nyingi humu zina 1 or two posts for years na hazileti tatizo. Duh!!!!
 
Mayalla na Sami wa BBC ndio waliouliza mswali ya msingi!

Wengine wote wababaishaji, bora tu sheria ya media ipite. Hatuna waandishi wa habari, wote makanjanja
 
Mwanzoni mlisema waandishi watakuwa wameandaliwa sasa hivi mnaleta ngonjera mpya Magufuli ni kiboko yenu
Kiboko yetu kwa lipi jipya zaidi ya kukwepa maswali ya msingi. Amejaa ngonjera na Mipasho, kaonesha uwezo wake kuwa Mdogo saana katka kujibu hoja.
 
bila kusahau tangazo la fiesta kesho kutoka kwa mkuu.kumbe naye sio mtu wa mchezo mchezo
 
Yeye kuwa mkuu wa nchi na serikali hakumpi mamlaka ya kusigina katiba other wise aseme ni presidential decree.
 
Pasco alipenyezewa lile swali,hakutafakari kwanza
 
Wallah nimecheka Leo!!! Nilivyoona mkuu akihaha kujibu!! Mara chungu, Mara Hahaahaaa, nilikuwa Nafuatilia nkaona jinsi nafasi adimu ilivyokuwa zinapotezwa na wauliza maswal wasiojua Kitu zaidi ya uogai!!, pasco alinifanya nione sijapoteza muda kuangalia tukio Hilo, I wsh ningejua muda ambao angeuliza Swali ndio muda ambao ningeanza kufuatilia hii issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…