Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Katika sehemu ya pili ya Mayalla, ameuliza kuhusu Rais anakopata mamlaka yake ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano na mandamano. Nyie wenzangu mmesikia majibu hapo????
 
Kimsingi mayalla kauliza maswali muhimu siyo yule dada wa TBC ambaye moja ya maswali yake alimuuliza rais baada ya kazi vitu gani vingine anapenda. Rais mwenyewe alicheka akamjibu unataka niseme nakupenda wewe?
 
Mkuu kwahiyo unataka kusema yale ambayo rais hakuyazungumzia basi anayaacha pending si ndiyo?
Mana yote yapo ndani ya shughuli za sirikali
Kaka Magufuli yuko very clear amesema anatekeleza masuala ambayo yapo kwenye ilani, Serikali inaendeshwa kwa kuzingatia mipango yake ya mwaka hadi mwaka ambapo msingi wa mipango hii huakisi yale yaliyo kwenye ilani ya chama husika waliyoombea kura sasa issue ya Tido ukiachilia magufuli kutoiongelea katika Kampeni zake au hotuba zake hata kwenye ilani ya CCM sina hakika kama lipo hilo suala la katiba mpya. Ni ukweli ambao mchungu kuwa kwa Magufuli issue ya katiba tusahau
 
1. Nanukuu: "Sikuja kufukua Makaburi, bali kuanzia nilipoikuta nchi na kuipeleka mbele".
Mwisho wa Kunukuu
Nadhani wale mliokuwa mnaropoka Kama Lowassa ni fisadi apelekwe Mahakamani mmejibiwa. Muhimu ni kutokubali Watu wa aina ya LOWASSA kutopewa nafasi tena nchi hii , matendo yao sasa yanatosha. Tumuunge mkono rais wetu.
2. Nanukuu: " Mifuko ya jamii na Mabenki imefilisika lakini wakopaji wakubwa ni wanasiasa, UKAWA wamo, CCM wamo , lakini utakuta wao ndiyo wapiga kelele na waongeaji wakubwa sana" mwisho wa kunukuu.

Kwa ujumla kama vyombo vya habari kesho havitakuja na headline kuhusiana na mambo haya mawili ujue hatuna wana habari. Mabenki kuwa na hali mbaya na hata kupelekea mengine kuwa chini ya uangalizi wa BOT ni mambo ambayo yamekuwa ni viashiria vya hali mbaya uchumi na ndiyo habari ya mjini hivi sasa, lakini kumbe wale wanaopiga kelele kuilaumu serikali ndiyo hao hao wanaopelekea hali hiyo. Hii ni hatari sana.
Ni tabia ya kutanguliza maslahi binafsi ndiyo iliyotufikisha hapa. Kutoshughulika na Watu waliohusika kuihujumu uchumi wa nchi yetu huko nyuma isiwe sababu ya kuamini kwamba hao watu hawakulihujumu taifa. Jambo la muhimu ni kutowapa nafasi tena watu wa aina hiyo katika taifa hili. Tumuunge mkono rais ili altujengee taifa lenye watu wa kutanguliza uzalendo mbele badala ya maslahi yao binafsi. Kwa kifupi tuseme tunataka taifa jipya na tusema SASA BASI kwa wale waliolihujumu taifa.
NAMUUNGA MKONO RAIS JPM .

@mods Invisible kweli kabisa mmeunganisha huu uzi na huu wa Pasco.

Hii sasa mmechemsha, mbona topic nzuri kukaa yenyewr, si bora hata mngepeleka kwenye ule uliokua live.

Sasa kuunga mnasave kitu gani, anaongelea points nzuri nyie mnaunga kwa Pasco kabisaaaaaa.

Please tendendeni watu uhuru fulani, kuna threads nyingi humu zina 1 or two posts for years na hazileti tatizo. Duh!!!!
 
Mayalla na Sami wa BBC ndio waliouliza mswali ya msingi!

Wengine wote wababaishaji, bora tu sheria ya media ipite. Hatuna waandishi wa habari, wote makanjanja
 
Mwanzoni mlisema waandishi watakuwa wameandaliwa sasa hivi mnaleta ngonjera mpya Magufuli ni kiboko yenu
Kiboko yetu kwa lipi jipya zaidi ya kukwepa maswali ya msingi. Amejaa ngonjera na Mipasho, kaonesha uwezo wake kuwa Mdogo saana katka kujibu hoja.
 
bila kusahau tangazo la fiesta kesho kutoka kwa mkuu.kumbe naye sio mtu wa mchezo mchezo
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
Yeye kuwa mkuu wa nchi na serikali hakumpi mamlaka ya kusigina katiba other wise aseme ni presidential decree.
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
Pasco alipenyezewa lile swali,hakutafakari kwanza
 
Wallah nimecheka Leo!!! Nilivyoona mkuu akihaha kujibu!! Mara chungu, Mara Hahaahaaa, nilikuwa Nafuatilia nkaona jinsi nafasi adimu ilivyokuwa zinapotezwa na wauliza maswal wasiojua Kitu zaidi ya uogai!!, pasco alinifanya nione sijapoteza muda kuangalia tukio Hilo, I wsh ningejua muda ambao angeuliza Swali ndio muda ambao ningeanza kufuatilia hii issue
 
Back
Top Bottom